Uonevu dhidi ya Waislam UDOM: Msikiti wavunjwa, wafanyakazi wanataaluma 11 wahamishwa

Kwa waliosoma UDOM watashangaa hawa jamaa wanataka msikiti wa nini.Udom imegawanyika ktk college sita na kila college inajitegemea kwa maana kutoka college moja kwenda nyingine hii ni safari ndefu. Mfano kutoka Health wanaita Tiba hadi coed ni safar ndefu, kutoka info kufika humanity au coed ni safar nyingine bado Earth kule. Huo msikiti utajengwa wapi ili kila mtu apate huduma?Kwa kutambua hili kila college kuna sehem zao za kuabudia, mfano COED kuna lecture Room special kwa wao kuabudia, kuwe na masomo au kusiwe na masomo hilo eneo ni special na hukuti watu nje ya waislam huko. So huko jamaa wako free mda wote na ukija mabwenini bado kuna vyumba special kwa wao kuswali. Hii ni kwa college ya education tu.Kila college kuna sehem zao za kuabudia. Huwez mkuta mwanafunz wa COED kaenda humanity kuswali. Kila watu wako sehem yao.Huu msikiti unataka kujenga wa kazi gani?Na utajengwa wapi ili kila mmoja apate huduma sawa?Hata ukisema ujenge info bado mtu kutoka COED,TIBA au Humanity ni mbali sana kwa kuja kuswali na kuwahi na kuendelea na masomo yake.Sioni logic ya kujenga msikiti UDOM. Kwa waliosoma UDOM wanaelewa hili.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Sasa nimeelewa

Shida sio sehemu ya kuswali

Wanataka sehemi itakayo wakusanya ili wapange mipango yao
 
Sawa mkuu umeeleweka kama ni hivo

Lakini umeluka jambo nililoelezea kuhusu nyie waislamu wengi wenu ni wabaguzi na mnajiona sana aisee yani hua mnajiona kua ni the most perfect human being. Mnatuita makafiri nk
Kuna sheikh nimewahi kumuona ana Biblia kaiandika kwa pen mambo yake kwenye zile page

Sent using Jamii Forums mobile app
Andika quran sasa yanavyochafukwa
 
Cha muntu Cha muntu Cha Nzambe Cha Nzambe.

Ya mungu mpe Mungu na ya Kaizari mpe Kaizari.

Kama umeenda kusoma kasome sana ibada popote inafanyika na Mungu wetu huwa anaipokea ktk mazingira yoyote.

Nakumbuka wakati fulani wanafunzi Waislam walijaribu kulazimisha kujengewa Masikiti ndani ya sekondari ya seminary ya Ndanda. Hivi nani aweza vumilia hilo?.

Wenzetu wanapenda sana maisha ya mitego mitego na kutafuta public sympathy ktk mambo yasiyo na tija ktk elimu zao.

 
Huyo Prof katoa kali sana, watu wa aina hiz huwa wanasali ktk nyumba za ibada za matapeli , wanajazwa uongo mwingi na pengne hata dini fulani akikusogelea anakuambukiza mapepo , au ukigusananaye anakuachia majanga , nasema hiv kunadada cjui anasali kanisa gn alimng'ata mfanyakazi mwenzie akisema kwamba ameoteshwa anamroga , hahahahaaaa inachekesha lkn yule mdada ni kavurugika akili na imani kbsa, hata chupa ya maji anachagua anasema hii ya freemason hii hv na hii vile , dunia jamn inaenda extreamly astray nyakati hz. watu wa hv sasa akisikia bintiye kabeba mimba na shekh na anataka kuolewa kabla hajajifungua sindio ataua mtu !!!
 
Ni kweli mliruhusiwa ila baada ya kuona mnaanza kuutumia vibaya uislamu kwa kuwatupia mapepo mpaka wanakufa ikabidi wawapige ban

Kama hamna msikiti mnaua watu mkishajenga si mtawapiga albadir wakristo wote
 
Rais Magufuli leo kasema wazi, UDOM kuwa sawa na UDSM msikiti ujengwe tu.

Nilisema humu, tusubiri.

Wako wapi wale waliokuwa wanabeza Waislam?
Hakika wazungu na waarabu walishatuweza!

Ni jambo la kipuuzi kukaa na kuanza kupigishana kelele kuhusu hizi imani tulizokaririshwa na wageni!

Natamani wanangu wanielewe waepuke huu utumwa wa fikra usiotaka kufutika kwenye bongo za waafrika.

Hivi UDOM imeanza kudahili wanafunzi mwaka gani!? Hao wote waliopitia hapo wao hawakuwa wanaabudu!?

Kwa namna UDOM ilivyojengwa, ni sahihi kweli kuifananisha na udsm!? Msikiti au makanisa yatajengwa wapi kuweza ku accommodate hizo swala tano!? Maana kutoka college moja hadi nyingine lazima upande daladala!! Au hizo nyumba za ibada zitajengwa kila college!?

Kama msikiti utajengwa kwenye college moja, inamaana huko kwenye college nyingine watengewe vyumba maalamu vya ibada pia!?

Navyokifahamu mimi chuo cha UDOM, kila college inavyumba maalum vya kuswalia ambavyo hakuna shughuli yoyote inayofanyika huko!! Hawa wengine waliridhi imani ya wazungu wanasalia kwenye theater rooms ambazo ndo hizo hizo hutumika kusomea na kumbuka haziwatoshi maana wako wengi!! Nani alitakiwa kuwa wa kwanza kutaka eneo maalum!?

Pia kama sikosei sana, nadhani hata kwenye blocks (bwenini) kuna vyumba maalamu vilitengwa kwa ajili ya hawa waliorithi imani ya waarabu!!

Huu utaratibu hautoshi!? Hayo maeneo yote hayafai kufanyia ibada!? Walioyatenga hawakuwa na akili!? Haki gani hapa wamenyimwa!?

Tu assume msikiti ujengwe pale opposite na utawala Mkuu ulipo ambapo nadhani ni eneo la earth science!!, Pata kidhi wanafunzi kutoka hummanities, education, tiba, engineering au kule chuo cha madini kilipo kufika kwa wakati na kurudi chuo kuendelea na taratibu za masomo!? Au demand ni kila college iwe na msikiti/kanisa lake!?

Utaratibu uliopo kwangu mimi naona unafaa kabisa japo ki uhalisia unawaumiza zaidi hawa wenye imani za wazungu maana wako wengi na wanarazimika kwenda kuabudu kwa awamu!

Haya mnayoyaona leo yalianza zamani sana kiasi kwamba kuna mwaka mmoja kuliibuka mgogoro kwenye serikali ya wanafunzi coed iliyopelekea watu kupiga kura za hasira ili hawa wenye imani za waarabu wasishinde uchaguzi maana ilisemekana,narudia tena'ilisemekana"wanafanya kampeni kwenye nyumba zao za ibada wachukue uongozi ili wawe na access na hela za udoso wapate fedha wajenge msikiti....hii ilikuwa ishu kubwa waliokuwepo enzi hizo wanajua vizuri sana hasa coed maana ndiko vuguvugu liliko anzia

MUNGU yupo mahali pote, anatupenda sote haijalishi unamuomba ukiwa njiani, chini ya mti au mahali pazuri, Mungu hutazama zaidi nyoyo zetu kuliko kitu chochote kile, haya mengine hawa wageni walitumezesha tu kwa interest zao



Sent using Jamii Forums mobile app
 
*KADHIA NZIMA YA UDOM NA HAMISHA HAMISHA YA WAISLAMU KUMI NA MOJA (11)*

Hivi karibuni ujenzi wa Msikiti Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ulisitishwa na kisha kuvunjwa ukuta eneo la Msikiti.

Ubomoaji huo ulifanyika Januari 09, 2019, kisha ukafuatiwa na uhamisho wa watumishi 11, Januari 11, 2019, kwa mpigo wote wakiwa ni Waislamu wakiwemo Wahadhiri, Viongozi waandamizi pamoja na Wanasheria.

Chanzo chetu kutoka UDOM kilieleza kuwa amri ya kuvunjwa kwa ukuta huo uliokuwa umezungushwa katika uwanja wa Msikiti ilitolewa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Peter Msoffe, kwa maelezo kuwa ni Amri kutoka ngazi za juu.

" Tumepokea kwa masikitiko uhamisho wa watumishi wenzetu 11 kwa mpigo wote wakiwa ni wa imani moja (Waislamu), uliofanyika Januari 11, 2019, uhamisho huo umekuja siku chache tukiwa bado katika sintofahamu na taharuki, kufuatia Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, kuamuru kuvunjwa Msikiti Januari 9, 2019, uliokuwa unajengwa Chuoni, akidai ni maagizo kutoka juu" Kilisema chanzo hicho.

Watumishi waliokumbwa na kadhia hiyo na kuhamishwa katika Taasisi zingine za Serikali wametajwa kuwa ni Dr. Mariam Khamis, Dr. Yusuph Kambuga, Dr. Masoud , Dr. Ibun Kombo, Khamisi Mkanachi, Mohammed Mwandege, Omari Simba, Subira Issa Sawasawa, Wema Mbegu, Aziz Gendo pamoja na Mwinyikondo Ameir.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja kama watumishi hao kwa namna moja ama nyingine wameondolewa kwa sababu ya kadhia hiyo ya kusitishwa ujenzi wa Msikiti uliokuwa unaendelea kujengwa katika eneo hilo la Chuo.

An nuur ilipotaka kujua kama ujenzi huo wa Msikiti ulikuwepo kihalali katika eneo hilo la Chuo Kikuu hicho cha Serikali ama ulikiuka taratibu za Chuo na Serikali na kupelekea kubomolewa, Chanzo chetu cha habari kilisema hakuna taratibu zozote za Chuo wala Serikali zilizokiukwa. Kwa ujumla ni kwamba vielelezo vyote vya kisheria vilifuatwa na vilikamilika kwaajili ya ujenzi wa Msikiti wa Chuo na hata michoro inayohusu ujenzi huo wa Msikiti Chuoni hapo ilipitishwa na Uongozi wa Chuo. Kimesema chanzo cha habari.

Awali chanzo hicho kilieleza kuwa Januari 27, 2018, uongozi wa Chuo ulikaa na kujadili suala hilo na kuja na maamuzi kuwa Msikiti usijengwe na inaundwa Tume ya kuchunguza namna ya uwezekano wa uwepo wa Msikiti na Kanisa katika eneo la Chuo. Hata hivyo haikutolewa barua rasmi ya kueleza makubaliano hayo. Timu hiyo iliyoundwa iliyowahusisha Profesa Mwakalobo, Profesa Makangara, Profesa Saidi Vywai pamoja na Bw. Mbegu Wema, ambae ni Mwanasheria wa Chuo, kazi kubwa ya tume hiyo ilikuwa ni kupitia Vyuo Vikuu mbalimbali nchini na kuona uwepo na uendeshaji wa Kanisa na Msikiti ndani ya Vyuo unakwendaje.

"Tume hiyo ilipita sehemu mbalimbali ikiwemo BAKWATA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Muhimbili, SUA na vyuo vingine nchini ikagundua kuwa kuna Msikiti na Kanisa ndani ya Vyuo." Kisha walirudi n majibu ya kwamba hata UDOM pia kuna haja na ulazim wa kuwepo kwa Msikiti na Kanisa pia. Kimesema chanzo hicho.

Chanzo hichi kilisema, majibu ya utafiti huo yalikuja wakati wa uongozi aa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Kikula na hapakuwa na tabu yeyote na kisha taarifa hiyo aliikuta Marehemu Profesa Mobofu na kwa kuwa ni suala la utafiti na kiofisi bado ripoti hiyo ipo ofisini chini ya Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo wa sasa Profesa Peter Msoffe. Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kwa hili lililojiri la kusambaratisha na kusitisha ujenzi wa msikiti, haifahamiki tatizo lipo wapi au kama kuna utafiti mwingine umefanywa ukaonyesha haifai kuwepo kwa Msikiti au Kanisa katika Chuo hicho cha Dodoma.

Kabla ya kubomoa Januari 09, 2019, Kilitangulia Kikao baina ya Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa BAKWATA Dodoma, Mwenyekiti wa Dodoma Muslim Association, pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyakazi Waislamu Chuoni hapo. Ni katika kikao hicho ndipo Kaimu Mkuu wa Chuo alipoeleza azma yake hiyo n kuwaeleza wajumbe hao kuwa kapewa maagizo toka juu ya kubomoa ukuta huo na kusitisha ujenzi unaoendelea. Aliombwa awe na subira kwani suala hilo limefuata taratibu zote kisheria na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi kwa taratibu zote kimaandishi na tayari Waislamu wameshaanza juhudi za kuliendeleza eneo hilo, hata hivyo hakubadili msimamo na kuamua kuondoka bila kifikia muafaka.

Imeelezwa kuwa siku hiyo hiyo asubuhi ya Januari 9, 2019 alipeleka askari na vijana wengine ba kuanza zoezi la kubomoa. Imefahamika kuwa, uongozi wa Waislamu chuoni hapo ulitoa tahadhari kuwa wasikubali kuchokozeka na kuingia katika mtego wa kujaribu kuzuia azma ya Makamu Mkuu huyo wa Chuo. Baada ya kubomoa Januari 10, 2019 walipokea barua, lakini barua hiyo inaonyesha imeandikwa Januari 09, 2019 ikieleza kisitishwa kwa ujenzi wa nyumba za ibada Chuoni hapo.

Hii barua imeandikwa baada ya uongozi wa Chuo kuvunja na kuharibu vitu vingine vya ujenzi vilivyo kuwemo eneo la ujenzi, sasa utaona ni namna gani zoezi hili lilivyoendeshwa kihuni. Kimesema chanzo hicho. Katika barua hiyo ya Januari 09, 2019 yenye Kumbukumbu namba UDOM/REF/272/49, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Peter Msoffe, amekiri kuwa UDOM ilitenga maeneo ya ibada kama ilivyo kwa vyuo vingine ndani na nje ya nchi kwaajili ya kuwajenga wanajumuiya kiroho. Hata hivyo Profesa Msoffe katika barua yake hiyo aliainisha kuwa katika kikao cha Januari 26, 2018, Baraza la Chuo lilisimamisha ugawaji na ujenzi wa nyumba za ibada chuoni hapo hadi litakapojiridhisha na kuwa kanuni na sheria zimefuatwa. Ni kwa muktadha huo na maelekezo mahususi ya Baraza la Chuo, tumeagizwa tusitishe shughuli za harakati za ujenzi wa maeneo ya kuabudia ndani ya eneo la Chuo, mpaka pale utaratibu mahususi utakapopangwa kihusiana na uendeshaji wa nyumba za ibada ndani ya eneo la Chuo, mpaka pale utaratibu mahususi utakapopangwa kuhusiana na uendeshaji wa nyumba za ibada ndani ya eneo la Chuo. Amesema Profesa Msoffe kupitia barua yake hiyo. Kupitia barua hiyo ya Profesa Msoffe ambayo nakala yake ilikwenda kwa jumuiya ya waislamu Chuo Kikuu cha Dodoma na CCT - UDOM imesema kwa sasa waumini wa dini zote wataendelea kuendesha ibada zao katika majengo ya Chuo yaliyopo kwenye mabweni na kumbi za mihadhara.

Akizungumzia barua hiyo, mmoja wa viongozi wa jumuiya ya Waislamu, Chuo Kikuu cha Dodoma, alisema Barua hiyo imejaa upotoshaji na suala zima jinsi lilivyo.

Vipi unatoa barua ya kusitisha ujenzi baada ya kubomoa na kufanya uharibifu eneo husika. Hiyo ni katika kujaribu kujiwekea kinga fulani, kisheria kama kuna tatizo angepeleka zuio la kisheria (Stop Order) au hata kuwafuata wasimamizi wa ujenzi na kuwaeleza kwamba wasimamishe ujenzi kutoa sababu anazozojua yeye. Amesema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema,haelewi ni kanuni na sheria zipi ambazo zinatakiwa kufuatwa nje ya zile ambazo zimefuatwa na Waislamu katika kuliendeleza eneo hilo la heka 10, Chuoni hapo.

Katika barua ya Chuo hicho ya Juni 6, 2016 imesema Idara Miliki ya Uongozi wa Chuo (UDOM) imepitia maombi ya ramani, michoro inayohusiana na ujenzi wa Msikiti na kwamba Kamati ya Mipango na Fedha katika kikao chake cha Juni 7, 2016 imeridhia ujenzi uendelee. Imeelezwa kuwa kibali cha ujenzi kilitolewa na kuainisha kuwa kitakuwa katika eneo la nyumba za ibada ambalo waislamu wamepatiwa hekari kumi na kuwataka wahusika wa kiwanja kufuata taratibu walizoainishiwa.

Baadhi ya taratibu hizo ni kufuata hatua zote za ujenzi ikiwa ni pamoja na kueleza hadhi ya Kampuni itakayojenga na mshauri wa ujenzi.

Pia Chuo kilitaka kuelezwa kwa kina mpangilio wa ukamilishaji ujenzi ambao unatakiwa uanze mara moja na kila jengo liwe katika hadhi na kiwango cha kimataifa kimatumizi na kimuonekano. Taratibu zote hizo tumezitekeleza kikamilifu na ndio maana eneo tajwa tukapatiwa na Chuo baada ya kupewa maelekezo hayo, tuliendelea na harakati zaidi za ujenzi kwa kuzingatia maelekezo ya Chuo ikiwemo kumpata Mkandarasi. Amesema kiongozi huyo.

An nuur, ilishuhudia barua ya Mkandarasi wa ujenzi wa Msikiti huo kwenda wa Mkurugenzi Mkuu wa Manispaa ya Dodoma, ikiomba kibali kwa mujibu wa Sheria za ujenzi.

"Chuo Kikuu cha Dodom kina mpango wa haraka wa kujenga Msikiti katika kiwanja chake kilichopo ndani y eneo la Chuo, tunaambatanisha nakala tatu za michoro ya usanifu na nakala tatu za michoro ya uhandisi, ni matumaini yetu kwamba maombi haya yatafanyiwa kazi kwa haraka. Imesema sehemu ya barua hiyo. Aidha katika barua ya Februari 3, 2017 inaonyesha malipo ya kibali cha ujenzi wa Msikiti huo (Biulding Permit) ambayo imelipiwa katika Manispaa ya Dodoma, kiasi cha Shillingi Milioni Nne Laki Moja na Elfu Kumi na Nne. Awali Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kolitoa maeneo ya ibada kupitia vikao maalumu na kupitisha kwamba wanachuo wapewe maeneo ya ibada kwa maana, Waislamu wapewe heka kumi na Wakristo wapewe heka kumi. Tangu kipindi hicho, Waislamu waislamu wamekuwa katika harakati na kufuata hatua mabalimbali zinazotakiwa katika kuliendeleza eneo hilo na kufanikiwa kuanza kwa ujenzi huo huku wakiwa wamelizungushia ukuta eneo lao. Kwa upande wa wakristo eneo hilo la heka kumi limeendelea kubaki kama lilivyokuwa huku ikidaiwa kushindwa kuliendelezwa kutokana na kugawanyika kwa kila dhehebu na kuhitaji kimiliki eneo hilo.

Akizungumzia kadhia hiyo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Mama Gaudensia Kabaka alisema hakuna Msikiti uliovunjwa kama inavyoelezwa. Mama Kabaka alisema kilichopo ni kwamba wamesitisha ujenzi wa Msikiti uliokuwa unaanza kujengwa ndani ya eneo la Chuo bila kibali, huku Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, pia hakuwa na taarifa. Alidai kuwa yeye kama mwenyekiti wa Baraza la Chuo, alipata taarifa kutoka kwa raia wema akiwa Jijini Dar es Salaam wakimueleza kwamba kuna ujenzi unaendelea katika eneo la Chuo unaosemekana kuwa ni Msikiti. Baada ya kupata taarifa hizo nikachanganyikiwa kwasababu kikao chetu cha mwisho hukuhusiana na suala hilo tulisema tusitishe suala hilo ili tusubiri muongozo, sikuamini kwa hiyo ilimbidi nimpigie simu Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo kumuuliza taarifa hizo.
Naye alikiri kuwa ni kweli ikabidi niagize ule ukuta uvunjwe na nikasema hiki kitu ni batili na ni ukiukwaji wa maelekezo ya Baraza la Chuo, Kwa hiyo ukuta huo ambao ni wabati ubomolewe na hilo lilifanyika Januari 9, 2019. Amesema Mama Kabaka. Akieleza historia ya mvutano huo, Mama Kabaka alisema awali Chuo kiliweka utaratibu wa kugawa maeneo ya nyumba za ibada katika eneo hilo la Chuo na taratibu zilikuwa zimekamilika baada ya kujiridhisha. Lakini Mama Kabaka alisema baadae uongozi (Management) wa Chuo ulipata taarifa za ziada na kualazimika kusitisha mpango uliokuwepo ili kuboresha taratibu za awali na kisha zijadiliwe kwa pamoja katika vikao. Alisema katika sakata hilo hakuna kikao kilichokaliwa na kukubaliana kwamba ujenzi huo uendelee kwani wakati wakisubiri taratibu za kikao, kama walivyokubalina, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Mobofu alipata maradhi na hatimae kufariki. Mama Kabaka alizikana barua za Chuo ba ile ya Mkataba zinazoeleza utaratibu na kukabidhiana kwa ardhi na kuanza kwa ujenzi wa Msikiti huo katika eneo la Chuo, akisema kuwa ni feki kwani hakuna vikao maalum vya Baraza la Chuo vilivyokaa na kuidhinisha ardhi hiyo itumike kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti huo.

Kwanza tukumbuke Chuo hiki hakijawahi kutoa ardhi pamoja na kutenga maeneo kwa Taasisi za kidini kama wakitaka kujenga watapewa, lakini hakuna kikao cha Baraza kolichowahi kukaa kabla yangu na wakati wangu kikagawa ardhi kwa Taasisi za Dini, iwe ya Kikristo au ya Kiislamu. Anasema Mama Kabaka. Aidha, Mama Kabaka alikiri uwepo wa barua ya Juni 6, 2016 inayoungumzia maombi ya kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti, hata hivyo alisema baada ya kuinagalia na kuisoma imebainika kuwa barua hiyo ni feki ingawa inaonyesha kusainiwa na uongozi uliopita. Sisi bado tunamashaka kama kweli ilipitishwa na Makamu Mkuu wa Chuo wa wakati huo, lakini pi wale wajenzi (Dodoma Muslim) wanadai kuwa wanamkataba ba Chuo, ambao nimeshindwa kuupata na aliyesaini alipoulizwa alidai hakusaini Mkataba. Sasa baada ya kukaa kikao kutokana na hali halisi iliyopo hivi sasa. Baraza la Chuo limeamua hakuna haja tena ya kugawa eneo la Chuo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za madhehebu ya Dini yoyote mpango huo umefutwa hayo yote yaliyotufikisha hapa ni mambo ambayo yalikuwa yanajiendesha yenyewe Amesema Mama Kabaka. Akizungumzia Uhamisho wa watumishi 11 ambao wote ni Waislamu, Mama Kabaka ametetea hilo akisema hatua hiyo imekuja kutokana na uwepo wa malalamiko ( Bila kufafanua Malalamiko kutok wap) kwamba baadhi ya maeneo nyeti ambayo yalikuwa na utata baadhi ya hayo ni katika ajira (Human Resource Management) Maeneo ya Fedha ba Mengineyo, Amesema Mama Kabaka. Alisem uhamisho huo umekuja pasi ya kutarajia kuwa maeneo hayo yalikuwa yakiongozwa na watu wa dini moja ,japo ni kweli inastua pamoja na hivyo watumishi hao wamehamishwa ili wakatumike sehemu nyingine...!!!!!
 
*KADHIA MSIKITI UDOM YATUA IKULU*

Mheshimiwa Raisi John Magufuli amesema anatambua katika maeneo ya Vyuo Vikuu panastahili kujengwa Msikiti na Kanisa ili kusaidia kuwajenga kiimani wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo.

Kauli hiyo imekata mzizi wa fitna ulioibua sintofahamu hivi karibuni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kufuatia uongozi wa Chuo hicho kusambaratisha harakati za ujenzi wa Msikiti uliokuwa unaendelea kujengwa chuoni hapo. Raisi Magufuli ametoa kauli hiyo katika Mkutano wake na Viongozi wa dini uliofanyika Jumatano wiki hii Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Awali katika Mkutano huo, Amir wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Mussa Kundecha na Kaimu Katibu Mkuu wa Bakwata, Ustadhi Nuhu Mruma, kwa nyakati tofauti walimuomba Mheshimiwa Rais Magufuli kulitupia macho suala la Msikiti wa UDOM na kulipatia ufumbuzi.

"Naomba niliseme hili mbele yako Mhe.Rais. ambalo unaweza kulifanyia kazi. Wiki moja iliyopita tumejiwa na ndugu zetu waislamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, wakilalamika kubomolewa uzio uliozungushiwa kwaajili ya ujenzi wa Msikiti." Alisema Sheikh Kundecha.

Sheikh Kundecha aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kutenga maeneo kwa ajili ya nyumba za ibada katika Chuo hicho kwa Waislamu na Wakristo, kwani ni jambo muhimu katika kuwajenga wananchi wake. Alisema katika hatua hiyo wapo walioanza kutekeleza jambo hilo kwa kuendeleza eneo la ibada, hata hivyo akasema inawezekana utendaji haukuwa mzuri kiasi kwamba Uongozi wa Chuo umesitisha uendelezaji wa maeneo hayo ya ibada. "Mimi niliamini kusitisha huko ujenzi huo kungekuwa katika muelekeo wa kutafuta namna nzuri ya kuliweka suala hilo katika utaratibu mzuri na si kufuta au kusitisha uwepo wa nyumba za ibada chuoni hapo"

Lakini usitishaji huo umekwenda mbali zaidi kwa uongozi kuingiza tingatinga kwenda kuvunja Msikiti na sisi pesa zetu ni za sadaka kwa kuchangishana, Waislamu wamejitolea wakiamini wanampa Mungu, kisha wanaona 'greda' linaingia na kubomoa. Alifafanua zaidi Sheikh Kundecha.

Ustadh Mruma yeye alitanabahisha kuwa migogoro kama hiyo inapotokea ni bora ikatafutiwa ufumbuzi unaokubalika kwa pande zote na kwamba viongozi wa kiimani hutiiwa zaidi na waumini wao na kupokea maagizo kwa jambo ambalo linagusa imani zao.

Alisema mwaka 2016 Mufti Abubakari Zubeir alitembelea Chuoni hapo na kuonyeshwa eneo hilo ambalo lilitengwa kwaajili ya kujengwa Msikiti na akatoa baraka zake na utaratibu ulikuwa ukiendelea.

"Lakini Mh. Rais (Magufuli) kwa bahati mbaya sasa ilitokea sintofahamu ambayo hadi sasa hatujapata maelezo ya kina yaliyopelekea kusambaratisha harakati za ujenzi huo, sasa hali hiyo imeleta tafrani kubwa." Alisema Ustadh Mruma. Alisema, suala hilo pia limefikishwa BAKWATA, lakini wao kama walinda amani wasio kuwa na silaha, wamelituliza ili wapite katika njia sahihi na kulitatua katika njia ambayo inafaa kwa amani ya nchi. Mara baada ya viongozi wa dini kumaliza kutoa maoni yao, Mheshimiwa Rais Magufuli alianza kujibu baadhi ya hoja za viongozi wa dini na nyingine kuahidi kuzichukua na kwenda kuzishughulikia.

Akijibu kadhia ya Msikiti UDOM, Rais Dkt. Magufuli, alisema kwa utaratibu na mwendo unaotumika katika Vyuo vingine kuhusu nyumba za kuabudia (Msikiti na Kanisa) utakuwa kama ule wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Raisi Magufuli alitoa mfano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwamba ndio huo huo utatumika katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

"Lakini natambua pia kwamba katika maeneo ya vyuo vikuu panahitaji kujengwa mahali pakuabudia, panastahili kujengwa kanisa ambapo watu wote wenye imani zao watakuwa wanaingia humo kwa utaratibu maalum na pajengwe Msikiti pia ambao nao utatumika kwa utaratibu maalum."

"Kwa hiyo hata Dodoma (UDOM) mwendo ule ule wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndio utaendelea kuwa pale Chuo Kikuu cha Dodoma na haswa kwasababu wanafunzi wanasoma pale lazima tuwajenge kiimani" Alisema Rais Dkt. Magufuli.

Akifafanua zaidi, Rais Dkt. Magufuli, alisema katika vyuo vikuu, kuna Msikiti na Kanisa.

Alisema, hata alipokuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuna Msikiti ambao unatumiwa na madhehebu yote ya Kiislamu, wanaswalia kwa pamoja katika Msikiti huo.

Kwa upande wa Kanisa, Rais Dkt. Magufuli alisema madhehebu yote ya Kikristo, pia kuna Chapel (Kanisa) pamoja na tofauti ya madhehebu laikini wanawekeana utaratibu wa zamu za ibada, kwa maana wanaingia Wakatoliki (RC) wakimaliza wanatoka na kuingia dhehebu jingine mpaka madhehebu yote yanamalizika.

"Dodoma tunalishughulikia. 'Spirit (nia na dhamira) ile ile ya Chuo Kikuu (UDSM) ndio itaendelea UDOM". Alimaliza Rais Magufuli.
 
SUA Niliwaona ealifikia Department of Engineering Nadhani mwenyeji wa wageni alikua Dr Banda Salum
 
Back
Top Bottom