Uonavyo: Kati ya KWAME NKRUMAH na J K NYERERE. Yupi anastahili heshima ya kisiasa ki mataifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonavyo: Kati ya KWAME NKRUMAH na J K NYERERE. Yupi anastahili heshima ya kisiasa ki mataifa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Mar 17, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Baada ya bongo zetu kugongwa gongwa na mijadala mikali kuhusu ufisadi nk; hebu tupumzishe akili zetu japo kidogo. Tujikumbushe kuhusu hawa wakongwe wetu wa siasa za Afrika. Wote walikuwa wanasiasa nguli katika katika kuhakikisha mwafrika anakombolewa kila mmoja kwa upande wake. Je ukipewa nafasi ya kutoa tuzo ya heshima kwa haki bila upendeleo. Utampa nani kati ya magwiji hawa?
   
 2. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wewe Kwame Nkurumah unamfahamu au ni unataka kutuletea utahira wako, hauwezi compare vitu ambacho kimoja haukifahamu vizuri
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  wewe ambaye humfahamu vizuri ndiyo taahira. Unataka turudi darasani kuanza kujifunza historia na uzee huu?
   
 4. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wote wamefanya mengi kusaidia kimataifa,JKN amefanya mazuri pia ndani,lakini kimataifa kura yangu napeleka kwa Kwame Nkurumah kutokana na falsafa ya afrika kuwa moja,jeshi moja na fedha moja,Jambo lililopingwa na JKN
   
 5. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mazembe sijakuelewa hapo uliposema JKN alilipinga wazo la Nkurumah, wazo lipi mkuu? La kuungana? Jeshi moja ama fedha moja?
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe kama umesoma sekondari ya kata huko Kibakwe imekula kwako. Nani asiyewajua wanasiasa hawa. Mi naona Nkrumah alikuwa na upeo wa juu zaidi. Kwa bahati mbaya aliwahi kututoka duniani.
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Kiongozi gani Duniani ameshiriki moja kwa moja kukomboa nchi nyingi zilizokuwa zinatawaliwa na wakoloni kama Nyerere?
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni katika wazo la kuunganisha Afrika iwe moja. Nkruma alitaka Afrika nzima iungane iwe kitu kimoja kwa mara moja. JKN Yeye alitaka iungane ki kanda kwanza.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Upeo wa kutaka Afrika iungane ghafla kuwa nchi moja? Una umri gani wewe?
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Sasa mwenye upeo zaidi hapo nani? Hizi si akili za kigadafi!
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nkrumah alikuwa juu zaidi, sema naye ana mapungufu yake.Nimebahatika kumsoma Nkrumah na historia yake kutoka Ghana mpaka Marekani alipofanya kazi kwenye viwanda vya sabuni kipindi anasoma . Hakika huyu bwana ana upeo mkubwa sema kama Nyerere naye aalikuwa ana element za kidikteta.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Hizi historia za kusomea tution kwa mwalimu Pdidy!(joke bro!)
   
 13. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani katika hili wote walikua na wazo moja ingawa walikua wana strategies tofauti.
  Wote walilenga kuunganisa Africa hata kama JKN alipenda tuanze kikanda zaidi.
  Unajua Nkurumah alikaa karibu na Pan Africanists kama kina Marcus Garvey na kina Du Bois ambao alitumia strategies zao na kukopy vitu vingi toka kwao.
  Nkurumah ni international figure zaidi na movement zake alipata msaada mkubwa toka kwa Pan Africanism tofauti na Nyerere ambaye movement zake alizifanyia hapa Africa hasa East & Southern na shughuli zake aliwahusisha zaidi Waafrica waliokua hapa Africa.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tupige kura ya afrika nzima tutapata jibu sahihi
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tumie mtandao wa facebook kwa kuanzia
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Du K umemwagia mwenzio matusi lakini,sijui nasie wengineo tunaokuona wewe uko chaka bovu na pumba tupu ungependa tukuite jina gani.Nkrumah alikuwa na brilliant idea,lakini HAKUWA NA VISION,hata Mwalimu alimpenda sana jamaa yule kwa idea zake na ndio maana Tanzania tukawa na memorial site kibao sana kumuhusu huyu jamaa kama plae Chuo kikuu tuna ukumbi maalufu sana Nkrumah.Kosa la Mwana wa Afrika yule ni kukosa VISION ya kutekelezea IDEA zake zifanye kazi.

  Mwalimu alipingana nae kuwa uwezi kuunda Africa moja kwa siku moja,Afrika moja itaundwa kwa kuanza na Kanda,kutokea hapo kanda zikisha imalika basi baadae kila kanda zitaanza kuunda ushirikino wa kikanda,ambavyo vitu hivyo tunaviona sasa.

  Idea ya kuwa Africa ni nzuri na hakika siku moja itafanya kazi,lakini sio leo,wala kesho ni baada ya kizazi fulani kama hapa kwetu wakina kayumba cream kama kama intake kumi na ushee na hapo itakapoungana hakika itakuwa ni strong state na uenda ikadominate dunia kwa muda mlefu sana.

  Lakini Mwalimu kwa busara zake alimchallange sana Nkrumah,tatizo kubwa la bwana mkubwa yule alikuwa na ka uarrogance na ustubborness fulani.Sometimes kwenye siasa hizi hasa zinazocheza na michezo ya kidunia kwa ujumla wake unapaswa kuwa Intellegent na smart pia.

  Mwalimu na ujanja wake wote wa kusurvive mbinu za wazungu lakini bado walimfanyizia kupitia watoto alio walea yeye na kuwakuza yeye.Sembuse na hiyo ya kutaka Africa iwe United states mara moja kuamka asubuhi.Nyerere Hakuna idealist bali he was a Man of Vision.
   
 17. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kimataifa? OAU kuweka ofisi yao iliyohusu ukombozi wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni Dar haikuwa ajali. Ilitokana na mchango wa Tanzania, chini ya utawala wa Mwl Nyerere, kwenya ukombozi wa bara la Afrika. Ainisha alichofanya Nkrumah kimataifa.
   
 18. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wote ni sawa
   
 19. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nyerere ni zaidi siyo tu kwa Nkrumah bali anamzidi hata Nelson Mandela. Simuoni kiongozi wa Afrika kwa walio tangulia mbele ya haki na walio hai ambaye anaweza kufikia hata robo ya nationalism ya JKN.
   
 20. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unakosea mkuu, ni wewe tu ambaye humfahamu. Nkurumah na Nyerere wanafahamika vzr sana kwa wale wenye hulka za kusoma vitabu hasa vya historia. Unajua watz wengi woga wa kusoma makala ndefu, wanapenda kusoma gosip na katuni.
   
Loading...