Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,105
- 18,005
WanaJF,
Nimewaza sana kuhusu hili. Uoga ni kitu kibaya sana. Uoga unawafanya watu wawe wanyonge na kunyong'onyea. Lakini pia waweza kupigwa vita na kuondoka. Kabla Lissu hajarudi, watu walikuwa wanasisimkwa mwili kufikiria tu kuwa atarudi tena Tanzania. Haya Lissu akarudi. Kabla ya kuteuliwa, akaanza mashambulizi - akawa anayapeleka palepale kwenye kitovu ambako watu hawapendi kuongelea hata wawapo wenyewe chumbani. Vyombo vya habari vikawa havitaki kabisa kuongelea habari za Lissu. Vyombo vikaunga juhudi za Rais na chama chake.
Lissu akandelea na uzi ule ule. Baada ya mwezi wa kazi ya Lissu, watu wamegundua kuwa yule self-proclaimed malaika na mungu-mtu kumbe naye ni binadamu anayekula, kunywa na kwenda toilet kama wengine. Sasa hivi naona vyombo vya habari vilevile vya mwezi mmoja uliopita, vinamzungumzia Lissu kama kawaida. Tena vinaweka kwenye taarifa zao hata kauli za kushambulia CCM na mgombea wake! Katika mwezi mmoja, watu wameondoa uoga. Uoga umeondoka ghafla! Watu wanamzomea hata yule aliyejitangaza kuwa ni malaika! Nani alitegemea haya katika Tanzania hii? Hata Membe alikuwa hana ujasiri wa kutaja chama cha kijani na mgombea wake. Akawa anamwita, "bwana yule"!
Tarehe 28 Oktoba 2020, shime Watanzania wenye miaka 18 na kuendelea, tuliojiandikisha kupiga kura, tujitokeze kwa wingi wetu tumpigia kura Lissu. Mfumo kandamizi utoke. Tupate uhuru, haki, amani na maendeleo kwa pamoja. Maendeleo yanaweza patikana bila watu kufungwa jela kwa ghiriba ama kupigwa risasi.
Lissu oyeeeeeeeeee! Yule aliyetaka kukuua anaona kama anapambana na mzimu wako vile. Sidhani kama atapata ujasiri wa kutaja jina lako kwenye majukwaa. Mwenezi wake pia anakuita eti "mgombea wa chama cha Mbowe" ili tu aepuke kukujata jina!
Pia tukumbuke kulinda kura zetu.