Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,178
Watanzania wengi ni watu waoga wasioweza kuhoji au kufuatilia kupata haki zao kwa mambo mengi ya msingi yanayogusa maisha yao mpaka mwisho.Kuna baadhi ya watu ni vigumu hata kumhoji au kujadiliana na daktari anayemtibu afya yake kwa kuamini daktari anajua kila kitu na sio vyema kupendekeza jambo lingine kwake!
Kwa upande mwingine raifa letu linaweza kuwa ni mojawapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuwa na mashujaa wengi walio nyuma ya Keyboard.
Sehemu kubwa ya hali hii ni utamaduni wetu wa muda mrefu ambao
Moja, Umewaaminisha watoto na vijana kwamba watu wazima hawakosei na mara zote watu wazima ni watu wenye busara sana.
Mbili, Umehusudu viboko katika malezi; Malezi ya kuchapa watoto kuanzia nyumbani mpaka shuleni. Kuchapwa kwetu kumejenga halia mbaya sana ya kutojiamini na hofu katika maeneo mengi ambayo tulipaswa na tunakuwa na haki ya kuhoji na kujadiliana katika hali ya kawaida tu na wenye mamlaka.
Tusipochukua hatua mahususi kuondokana na huu utamaduni tutaendelea kuwa taifa la wanyonge kwa muda mrefu sana.