Unywaji wa Maji ya kutosha katika maisha kunaweza kupunguza hatari ya maradhi ya moyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Kulingana na utafiti uliowasilishwa katika mkutano wa 2021 wa Jumuiya ya Urolojia ya Uropa, ilibainishwa kuwa unywaji wa maji kwa wingi husaidi kupunguza hatari ya upungufu wa maji mwilini ambayo inaweza kupunguza hatari ya maradhi ya moyo.

Daktari Natalia Dmitrieva, alisema katika utafiti huo kuwa wamefikia ugunduzi kwamba matumizi ya maji ya kutosha yanaweza kuzuia au angalau kupunguza mabadiliko ambayo yatasababisha kupungua utendajikazi wa moyo.

Wakati inapendekezwa kwa wanawake kunywa kati ya lita 1.6 na 2.1 za maji kwa siku, matumizi ya maji ya kila siku yanayopendekezwa kwa wanaume ni kati ya lita 2 hadi 3.

Utafiti uliofanywa kwa kiwango cha kimataifa unaonyesha kuwa watu wengi hawafiki hata viwango vya chini vya matumizi ya maji ya kila siku.

TRT
 
Link husika tafadhali
 
hv mnajua ukinywa hayo maji na uko sehemu ambayo choo ni ya kulipia utatumia shilingi ngapi kwa siku kwa ajili kukojoa koja baada ya kunywa hayo maji nyie ?
 
Huu utafiti sipingani nao,lakini huwa wanafanya consideration kwa wale watu wanaoishi sehemu zenye baridi?mfano mimi nikiwa sehemu za baridi nikinywa maji nusu lita tu baada ya kuamka nitakojoa mpaka najiogopa,ni kila baada ya nusu saa lazima mkojo utoke,ni mwingi na mweupe,je hakuna madhara kwenye viungo vingine kama kweli utafikisha hizo lita 3 kwa siku?maana hapo sidhani kama figo nazo zitakuwa salama kama utakuwa ni utaratibu wako kwa mwaka mzima! (As drinking too much water can disrupt your body's electrolyte balance and lead to hyponatremia, 3 liters (100 ounces) may be too much for some people)....
 
Wangesema kiwango cha maji kulingana na uzito wa mtu. Hiii ya kusema binadamu. Unaanzaje kunilinganisha Mimi mwenye futi 6 na Inches 9 na mtu mwenye futi 5 na Inches 6.
Lazima tutofautane kwa vitu vingi sana. Nadhani tofauti ipo kubwa sana
 
nakubaliana na utafiti huu,mimi ni mmoja ya watu ambao nakunywa maji sana haijalishi hali ya hewa,hadi nimepata uraibu wa kunywa maji maana nikikaa masaa maweli sijanywa hata nusu lita basi utendaji wa mambo yangu lazima utakuwa slow sana,na pia sijawahi kuumwa chochote tangu 14/10/2000 wanaeza umwa mafua au kikohozi nyumba nzima lkn mimi hata dalili sinaga
 
IMG_20210810_083315-picsay.jpg
 
Hii ni kweli hata hili gonjwa litakupita tuu, mimi nlikuwa na aleji na baridi yaani nisikae sehemu yenye baridi utanionea huruma, tangu nianze kunywa maji naishi maisha ya kujidai yaani na baridi yote ya mwaka huu nipo Arusha mwaka wa pili sijaumwa chochote.
 
hv mnajua ukinywa hayo maji na uko sehemu ambayo choo ni ya kulipia utatumia shilingi ngapi kwa siku kwa ajili kukojoa koja baada ya kunywa hayo maji nyie ?
Unanunua galoni ya lita tano unaitunza unakuwa unakojoa humo then usiku unamwaga
 
hata mimi nilimsikia akisema hivyo tena muda mfupi baada ya daktari bingwa wa figo kuhimiza watu wanywe maji mengi ili kupunguza magonjwa ya figo
 
Huu utafiti sipingani nao,lakini huwa wanafanya consideration kwa wale watu wanaoishi sehemu zenye baridi?mfano mimi nikiwa sehemu za baridi nikinywa maji nusu lita tu baada ya kuamka nitakojoa mpaka najiogopa,ni kila baada ya nusu saa lazima mkojo utoke,ni mwingi na mweupe,je hakuna madhara kwenye viungo vingine kama kweli utafikisha hizo lita 3 kwa siku?maana hapo sidhani kama figo nazo zitakuwa salama kama utakuwa ni utaratibu wako kwa mwaka mzima! (As drinking too much water can disrupt your body's electrolyte balance and lead to hyponatremia, 3 liters (100 ounces) may be too much for some people)....
Hata mimi ndio maana nikajiuliza mkuu.

Watu wa maaeneo ya baridi wakinywa maji the only means ya kupoteza maji kwa kawaida ni jasho na mkojo.

Sasa kwa maeneo ya baridi ni ngumu kutoka jasho jambo ambalo hupelekea kukojoa ndio iwe njia pekee ya kuporeza maji mwilini.

Sasa shida inakuja kwamba kiasi kingi cha maji mwilini kinaweza kuwa sio kizuri kwa sababu kinaweza kwenda kuzimua saaana zile electroyte ambazo ni muhimu sana katika harakati mbalimbali za mwkli na kuupa nguvu.

Sasa lita mbili mpaka tatu kwa mtu ambae ana mwili wa kawaida tu alafu pengine anaishi maeneo ya baridi inaweza kupelekea mtu huyu kuwa na maji mengi mwilini na kuathiri electrolyte katika mwili.

Sijui lakini wataalamu pengine wana majibu zaidi
 
Embu mtu yoyote ambaye amewahi kunywa maji mengi akaathirika aje aweke ushahidi hapa, kama mimi ambaye nimekunywa maji mengi siumwi mahali popote na ninaishi sehemu ya baridi kwa sasa. Suala la kukojoa mara kwa mara unapokunywa maji mengi hutokea kipindi cha kwanza unapoanza kunywa maji kwa sababu mwili unakuwa haujazoea , mwili ukizoea unakuwa kawaida kabisa, au kama unaogopa kukojoa kojoa ukiamka usiku kunywa maji lita moja, hadi ifike muda wa kwenda Kazini unakuwa unadaiwa lita mbili, mchana ukinywa nusu lita unabakiza lita moja na nusu ukifika nyumbani tuu unapiga lita moja, unakuwa umebakiza nusu lita, ukimaliza kula unakaa kidogo unamalizia kale kanusu sasa, maji ni mazuri sana. Mimi nimepata faida zifuatazo kwa kunywa maji mengi.
Nimekuwa mwepesi yaani sisikii uchovu mara kwa mara
Sijawahi kuumwa kitu chochote tangu nianze utaratibu huo miaka miwili imepita(nilikuwa siwezi kuishi sehemu ya baridi nikiishi nakohoa sana)
Nimekuwa na ngozi nzuri ukizingatia nina ngozi kavu sionekani kupauka hata nisipopaka mafuta.
Nimekuwa na nywele nzuri na zinakuwa kwa haraka.
Ukiishi Mkoa wa baridi usinywe maji ya baridi ya kwenye friji kunywa ya kawaida.
 
Natamani ningemuona huyo dr atoe maoni yake kwangu maana nimevuka nusu karne kitambo
Na maji pure water sinywi kabisa nina zaidi ya miaka 40
Ni juice na baadhi ya matunda tu na salad kidogo ila maji hapana
Sio kuwa yananiumiza au vipi ila nimeyakataa tu na sioni faida yake
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom