Unywaji wa Maji, Soda, na Chai Wakati wa Kula... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unywaji wa Maji, Soda, na Chai Wakati wa Kula...

Discussion in 'JF Doctor' started by Dickson Ng'hily, Jun 13, 2011.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Wakubwa naomba mnifunze kitu hapa, nimekuwa nikisikia kuwa unywaji wa maji wakati unakula au mara baada ya kula sio mzuri. Inasemekana unahitajika kupumzika walau saa moja kisha ndo unywe maji...Sasa swali langu ni hili, je unywaji wa chai wakati unakula unamadhara gani! Coz binafsi napenda kimiminika cha moto nikiwa nakula au mara baada ya kula. Au unywaji wa kimiminika cha baridi iwe soda au juice! Kwani tatizo ni maji kwa maana ya maji au tatizo ni kimiminika! Mwenye ufahamu na hili tafadhari anisaidie....
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Chai ni nzuri zaidi,maji yakiwa ya uvuguvugu nayo pia ni mazuri .Soda si nzuri.Faida ya chai au maji ya moto ni kuyeyusha mafuta,ila soda au maji baridi hugandisha na hivyo kufanya umengenyaji wa chakula kuwa tatizo.
   
 3. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Mkuu Mayenga...Nakushukuru sana coz ilikuwa inanipa tatizo sana....
   
 4. MLATIE

  MLATIE Senior Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Na mm nimefaidika shukurani kaka
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160

  Habari kaka Ng'hily, huwa nakufuatilia michango yako kule kwenye jukwaa la siasa, nafurahi kukuona na huku pia!

  Kiukweli maji hayajawahi kuwa na tatizo lolote ukinywa wakati wa kula au soon baada ya kula (provided huna matatizo ya figo ambapo kiasi cha maji ya kunywa kinakuwa limited). Mwili wa binadamu unahitaji lita 2 - 2.5 za maji kila siku, kiasi ambacho wengi wetu ni vigumu kukifikia, chakula ni chanzo kimojawapo cha maji hivyo kunywa maji wakati wa kula hakuna madhara yeyote wala hakukatazwi kiafya. Maji ya moto au baridi haijalishi, inategemeana na hali ya hewa tu. lakini chakula huwa kinakaa tumboni kwa masaa 3 - 4 kikichanganywa na vimeng'enyi mbali mbali katika joto maalum ambalo vimeng'eny hivyo vinaweza fanya kazi vizuri, hivyo hata ukinywa maji baridi bado yatapashwa kufikia kiasi cha joto linalohitajika kunyonywa mwilini. Na maji baridi hayazuii mafuta kumeng'enywa au kunyonywa tumboni/mwilini.

  Chai ningekushauri unywe masaa 2 hadi matatu baada ya mlo mkuu..Chai ina kitu kinaitwa 'tannins', hii kemikali huwa inazuia unyonywaji mzuri wa chakula hasa 'micronutrients' kama madini (iron) na vitamins. Kahawa ina tannins kidogo sana kulinganisha na chai, bora unywe kahawa kuliko chai kama ni lazima muda mfupi baada ya kula.

  Juice pia kama ilivyo kwa maji haina tatizo lolote, iwe baridi au moto haizuii chakula chako kunyonywa vyema.
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Riwa
  Asante sana maana kuna mtu mmoja alikuwa anatangaza kuwa huruhusiwi kunywa maji baada ya kula.
  Asante sana kwa shule hii kaka
   
 7. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Mkuu Riwa, nakushukuru sana kwa kufuatilia michango yangu kule jukwaa la siasa na pia nakushukuru sana kwa darasa zuri ulilonipatia...Unajua kuna watu wamekuwa wakisema kuwa ukinywa maji wakati unakula au mara baada ya kula ni kuloweka chakula na hivyo kukisababisha kisiweze kumeng'enywa inavyotakiwa na matokeo yake ni kuwa na kitambi...Sasa niliogopa coz me ni mnywaji mzuri wa chai/Kahawa lakini pia ni mnywaji mzuri wa maji..japo umesema mtu anatakiwa kunywa lita 2-2.5 za maji kwa siku, mimi ninawuwezo wa kucha mpaka lita 8 za maji kwa siku..Sasa kitumbo kimekuwa na ukweli sikipendi ndo nikaanza kufikilia labda ndo yale yanayosemwa na hii imenisababisha kujizuia kunywa maji kwa wingi.Sasa nakunywa less than 2 litaz kwa siku..Unajua kilichokuwa kinanisukuma kunywa maji ni kuwa nilijijengea tabia kuwa sihitajiki kuhisi kiu so nilikuwa nakunywa maji mara kwa mara...Kuhusu chai au kahawa naweza sema pia ni kama ndo ulevi wangu, coz napenda sana...Nway, nashukuru kwa darasa kaka, ila nikuulize swali jingine, kuna ukweli wowote juu ya kupata kitambi kwa kutokana na kunywa maji mengi!Nitashukuru kwa majibu kaka...
   
 8. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Kumbe na wewe uliwahi kumsikia eeh...Lol..Aliniogopesha sana...Asante Mkuu Riwa kwa darasa...
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kaka Ng'hily
  Nilimsikia na alisema pia kuwa unatakiwa ukae saa kama mbili hivi ndo unywe maji baada ya kula na ilinifanya mpaka hata nikaogopa kunywa maji au juice baada ya kula
  Riwa ametoa darasa zuri sana asante sana mkuu
  Ngoja aje atupe hilo la kitambi ila sidhani kama maji yanasababisha kitambi kaka maana yanachofanya maji ni kusaidia kuregulate mwili na kuufanya ufanye kazi zake vizuri
   
 10. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kaka Ng'hily...hakuna ukweli wowote kuhusu kupata kitambi kutokana na kunywa maji mengi. Kama huna matatizo ya mafigo, kunywa maji mengi lita mbili au zaidi ni nzuri sana kwa afya yako.

  Kitambi au kunenepa kwa ujumla kunasababishwa na mwili kupata (kupitia chakula) energy (calories) nyingi kuliko unavyozitumia na hivyo mwili kuweka ziada, Energy au calories hizo uhifadhiwa katika mfumo wa mafuta ambayo hudeposit kwenye kuta za tumbo, makalio na hips hasa kwa wanawake lakini hata wanaume, ndani ya tumbo na hata kuzunguka moyo...na mafuta mabaya zaidi ni yale yanayojilimbikiza katika damu hasa low density cholesterol.

  Vaykula vyenye calories nyingi kiasi cha kurisk mwili kujilimbikiza mafuta kwa wingi ni vyakula vya wanga (starch) na vyakula vyenye mafuta...Maji hayana starch na wala hayana mafuta, hivyo kwa namna yeyote ile maji hayawezi kusababisha mwili ulimbikize mafuta (energy/calories). Kunywa maji kati ya lita 2 - 2.5 kila siku kwa afya yako.
   
 11. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Kaka Riwa....Nakushukuru sana kwa darasa, ukweli umenifungua sana tena kupita maelezo na Mungu akubariki kaka...Naamini darasa hili limesaidia wengine pia...Kaka me maji nakunywa sana ila nilishituliwa na huyo jamaa kwa radio kuwa haifai kunywa maji wakati wa chakula na baada ya chakula na jamaa alikuwa anatumia lugha mbaya mpaka unaogopa....Hili la kitambi ni hisia zangu coz nilidhani ukinywa maji mengi yanasababisha tumbo kutanuka..Kama nilivyosema me ni mnywaji wa maji na ninaweza kunywa hata lita nane kwa siku coz kwa seating moja huwa nakunywa maji kama lita 1.5 na home nina kikombe cha lita 1.5 ambacho huwa nakitumia kunywa maji...Nway, asante sana kaka..
   
 12. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuna kitu hamjanote nyie watu! amesema, ukinywa maji itabidi yarekebishwe joto ili ifikie ile maalum ndipo vimeng'enya vianze kazi. ninachojua mimi, madhara ambayo yanafanya watu washauri kusubiri ni kutokana muda utakaosubiri maji kupashwa joto ama kupoozwa! kwa maana hiyo bado ushauri uko pale pale, usile na kunywa hapo hapo.
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mkuu wewe kiboko. Lita nane ya maji kwa siku simchezo. Mie lita 3.5 kwa siku na hapo nakimbia kila asubuhi.

  Fanya mazoezi pia mkuu itakusaidia kutoa kitambi na kwa afya lol.
   
 14. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wingi wa maji inategemea yanatumikaje mwilini! kama anaongea sana, anatembea sana, anawakiwa na jua sana ama anatoa jasho sana ni sawa. idadi ya lita alizotaja ni kwa watu wa kazi ngumu sana juani!
   
 15. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Msongoru..2 - 2.5 ni idadi ya lita za maji ambazo mtu mzima anahitaji kupata kwa siku hasa huku kwetu kwenye ukanda wa tropiki, kama una kazi za nguvu na juani unaweza ukahitaji zaidi ya hapo!

  Na pia, unywaji wa maji baridi hauingiliani na mmeng'enyo au kunyonywa kwa chakula tumboni. Yes chakula na maji humeng'enywa na kunyonywa katika joto fulani ambalo ni la juu kidogo, unavyokula vitu baridi hupashwa vinapofika tumboni kabla ya kumeng'enywa na kunyonywa ili kuendana na joto ambalo mwili unahitaji. Sio kweli kwamba ukinywa maji au vinywaji baridi wakati wa kula au baada ya kula basi chakula ulichokula hakitameng'enywa na kunyonywa!
   
 16. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kaka Ng'hily hapo kwenye radio na niongezee tv nadhani Tanzania tunakosa udhibiti, na partly lawama nizielekeze kwetu sisi wadau wa afya, taasisi za afya, chama cha madaktari Tanzania, chama cha wauguzi Tanzania, wizara ya afya kitengo cha elimu ya afya kwa jamii, na zaidi kwa vyombo vya habari. Sources za habari sahihi kuhusu mambo yahusuyo afya yapo ( kwa kuliona hilo sasa hizi mimi na wadau wengine tupo katika mchakato wa kusaidia wizara ya afya kitengo cha elimu ya afya kwa jamii kutengeneza 'digital library' ambapo information nyingi kuhusu afya na tafiti mbali mbali zitapatika kwa easy referrence). Baadhi vyombo vya habari havijishughulishi kupata taarifa sahihi wakati wa kuandaa vipindi, na wanapoalika watu ambao wanatoa tiba mbadala hawawahusishi watu wa kitengo cha wizara ya afya ya tiba za asili/mbadala Muhimbili.

  Hii inapelekea watu kuwa huru kutoa taarifa zisizo na ukweli na zisizofanyiwa utafiti kuthibitisha ukweli wake kwa jamii. Kilikuwa na watu kama kina mama Terry kwenye mambo ya lishe (kuna vitu alikuwa anasema vya ukweli na manufaa lakini vingine si kweli na pengine hata madhara), walikuja akina Ngoka 11 na dawa moja inayotibu magonjwa zaidi ya 100 n.k, na sasa kuna akina Isaac Ndodi na wengine kama huyo uliyemsikia....lakini hakuna udhibiti wa nini wanasema hawa watu hata kama kina athari kwa afya za watu wanaowasikiliza na kufuata wasemayo.

  Taasisi mbali mbali za kitaalam za afya ikiwemo chama cha madaktari Tanzania na wizara ya afya kitengo cha elimu kwa afya ya jamii hawarespond kwa taarifa zisizo za kweli zinazotolewa na watu hawa, na kutoa ukweli uliothibitishwa kisayansi..matokeo yake wanajamii wanafuata na pengine baadhi yao wanaathirika.
   
 17. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Mkuu Riwa, asante sana ndugu yangu kwa darasa...Kwenye red hapo...Me nilimsikia huyo huyo mjamaa, lol....yaani anaongea vibaya kweli...Mama Terry pia nilikuwa namashaka naye na nJU yeye alikuwa anautaka ubunge ndo akaamua kutumia hizo rishe zake...Ukweli mimi si mtaalam wa afya ila nakumbuka mama Terry alikuwa anawaambia watu watengeneze juice ya mchunga (Kwetu hiki ni chakula cha sungura ila sehemu zingine ni mboga)..Yaani wanauchukua mchunga na kuuosha kisha kusanga kwa blenda na kuchanganya na maji kisha unakunywa...Lol...Yaani mchunga ulivyo mchungu! hata wanaoupika huwa wanamwaga sana maji mpaka uchungu unatoweka...Nway, mimi nitakuwa nakusumbua sana na haya maswali ya kuhusu afya...

  Mimi nilizaliwa bila kuwa na pumu...Ukoo wetu nillifuatilia kwa kuwauliza wazazi wangu wote kabla hawajafariki ikiwa kulikuwa na mtu ana pumu na wakanihakikishia kuwa hakuna...Mwaka 1998 mwezi wa nane sikumbuki tarehe ndo kwa mara ya kwanza nilibanwa na pumu...Mwanzoni sikujua ni nini kwani sikuwahi kutumia dawa wala kwenda hospital...Niliangaaika hivyo kwa mda mrefu...mwaka 2004 ndo nikaenda hospital na nikagundulika nia allergy ya vumbi laini ambayo imedevelop kuwa pumu..Hivi sasa nimekuwa natumia dawa kama salbutom spray au vidonge na nikiwa na hali mbaya sana huwa nachomwa sindano...Hata hivyo nikitoka nje ya Dar huwa sibanwi mara kwa mara..Sasa swali, Je watoto wangu wanaweza kurithi ugonjwa huu hatari....??????Mmoja kazaliwa 2005 na mwingine 2007, ukweli nawaonea huruma sana hebu nisaidie, na je pumu inaponyeka I mean inatibika na kwisha kabisa?
   
Loading...