unywaji ulanzi Iringa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
"KARIBU mchumba, karibu unywe ulanzi, unataka mtogwa (uliogemwa leo) au mkangafu (wa siku nyingi) na mdindifu ulio fukiwa kwenye mchanga wiki 1 pia kuna baruti huo ni ulanzi uliokaa kama wiki 2 hv? Njoo ukae nami hapa usiogope! Mama Anita, lete lita moja fanya haraka mrembo asije akaondoka," hivyo ndivyo nilivyopokewa katika klabu cha pombe cha Ndiuka, Iringa.
Nilikwenda kufanyia kazi utafiti wa wataalamu unaosema kuwa moja ya sababu zinazochangia kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa wa Iringa ni ulevi hasa wa pombe za kienyeji.
Mmoja wa wauzaji wa pombe hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe anasema wakati wa msimu wa pombe ya ulanzi, wanywaji wengi hushindwa kuzuia tamaa zao za ngono na kujikuta wakijiingiza katika vitendo hivyo bila kinga.
"Ulanzi ukiwa mwingi ngono pia huwa nje nje! Ndiyo maana msimu wa ulanzi ukiisha tu wanawake wengi huwa na mimba zisizotarajiwa. Ulanzi ni hatari, unasababisha watu washindwe kujizuia na hatuwezi kuuacha kwani ni asili yetu," anasema.
Pombe hiyo iligunduliwa wakati wa utawala wa machifu wa kabila la Wabena katika Wilaya ya Njombe baada ya mti mchanga wa mwanzi kukatika na kuanza kutoa maji matamu.
Tangu wakati huo, pombe hiyo imekuwa ikithaminiwa na wakazi wa Mkoa wa Iringa na tayari imeshambaa na kufika katika maeneo mengine mengi hasa kusini mwa Tanzania.
Wanywaji wengi wa ulanzi wanasema bila shaka kwamba pombe hiyo inachangia kasi ya Ukimwi.
"Msimu wa ulanzi huwa unauzwa bei rahisi ambayo hakuna inayemshinda ndo maana watu wengi hulewa hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ngono bila kujiandaa kwani wanawake wengi wakishanunuliwa kinywaji hicho huwa wepesi kukubali," anasema Richard Mwenda.
Mtaalamu wa magonjwa ya ngono mkoani Iringa, Dk Paul Luvanda anasema pombe hiyo ndiyo kichocheo kikubwa cha ngono zembe hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi.
"Ulevi hasa wa pombe ya ulanzi unachangia kuongeza hamu ya kufanya ngono zembe, wengi wamejikuta wakipata maambukizi kutoka na pombe hii ambayo inaheshimiwa na wenyeji," anasema Dk Luvanda.
Ulanzi siyo kichocheo pekee, Luvanda anataja mila na desturi potofu ambazo jamii nyingi mkoani humo bado inaziendeleza. Miongoni mwazo ni kurithi wajane, kukosekana kwa usawa kijinsia, kutakasa wajane na wasichana, kuoa wake wengi, imani za kishirikina na kutotahiri.
Nyingine ni umaskini wa kipato. Maisha ya wananchi wengi ni duni.
Anasema kutobadili tabia licha ya elimu ya ukimwi kuwafikia wananchi na wengine kuathiriwa kwa njia moja au nyingine na Ukimwi ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ugonjwa huo.
Anataja sababu nyingine kuwa ni muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli nyingi za biashara na ongezeko la taasisi mbalimbali mkoani humo.
Hali ya maambukizi ikoje?
Dk Luvanda anasema watu 17,555 kati ya 71,628 waliojitokeza kupima kwa hiari kati ya Julai 2008 hadi Juni 2009, walikutwa na maambukizi ya VVU. Hali inayoonyesha kwamba maambukizi yameongezeka na kufikia asilimia 24.5 hali ambayo ni hatari.
Anasema kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa hali ya ukimwi kitaifa mwaka 2003/2004, maambukizi yalikuwa asilimia 13.4 na mwaka 2007/2008 yakapanda na kufikia asilimia 15.7.
"Utafiti unaonyesha Iringa tupo asilimia 24.5, hii siyo hali ya kawaida hata kidogo." Anasema Wilaya ya Makete inaongoza kwa kuwa na asilimia 35.9, Njombe 31.9, Iringa 30.5, Mufindi 24.0, Manispaa 23.5, Ludewa 18.6, Njombe mjini 21.1 na Kilolo 12.2.
Hadi Juni 2009, wananchi walioandikishwa kweny mpango wa dawa za kupunguza makali ni 51,137 na walioanza kutumia dawa hizo ni 25,703.
Wakati maambukizi ya Ukimwi mkoani Iringa yakiongezeka kwa kasi, takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa yamepungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi asilimia 5.8 mwaka 2007.
Hiyo ina maana kwamba Mkoa wa Iringa ndiyo wa kwanza nchini kwa kuwa na kiwango cha juu kabisa cha maambukizi, ukifuatiwa na Dar es Salaam yenye asilimia 8.9 na wa tatu ni Mbeya yenye asilimia 7.9.
Kutokana na kiwango hicho cha maambukizi mkoa unakisiwa kuwa na watu 246,935 wanaoishi na VVU/Ukimwi kati ya wakazi wake wote zaidi ya milioni 1.5 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.
Idadi ya watoto yatima nayo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na wazazi wengi kupoteza maisha. Watoto 67,915 wameshatambuliwa na 30,303 wanapatiwa misaada ya chakula, mavazi, malazi na elimu.
Mkoa unafanya nini?
Kupaa kwa takwimu za maambukizi ya Ukimwi kunaonyesha kuwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na mkoa huo kupambana na janga hilo zimegonga mwamba.
Hata hivyo, Dk Luvanda anasema umeandaa mkakati wa kupambana na kasi hiyo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2008 utakaomilika Septemba 2012 ukilenga kupunguza kasi hiyo kwa asilimia 50.
Anasema tayari Sh1.8 bilioni zimeshatumika kuanzia Juni 2008 hadi June 2009. Kati ya fedha zilizotumika, Sh953.9milioni ni kutoka serikali kuu wakati Sh870.1milioni ni michango wa wadau mbalimbali wanaoshiriki katika mapambano ya Ukimwi Iringa.
Dk Luvanda anasema Wilaya ya Makete ilitumia Sh 942.5milioni, Ludewa 150.7milioni, Manispaa 22.2 milioni, Iringa Vijijini 116.2 milioni, Kilolo 54.6 milioni, Mufindi 442.6 milioni na Wilaya ya Njombe ilitumia Sh114.8 milioni.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Ezekiel Mpuya anasema mkakati huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mapambano dhidi ya Ukimwi katika halmashauri za wilaya na kuwa umeandaliwa kwa kuzingatia vipengele vilivyomo katika Mkakati wa Pili wa Taifa wa Mapambano ya Ukimwi (NMSF) wa mwaka 2008 hadi 2012.
Mpuya anasema mpango huo umezingatia pia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali walio katika mapambano ya Ukimwi mkoani Iringa, pamoja na maelekezo ya wataalamu wa ndani ya mkoa na taifa.
Anasema mipango iliyoibuliwa inatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja na kutathminiwa kila mwaka kisha kuendelezwa na mipya kuibuliwa kulingana na matokeo ya tathmini.
Anasema huduma za tiba zinatolewa katika hospitali 16 zilizopo mkoani Iringa na vituo vya afya 14 kati ya 26. Lengo ni kufikia vituo vya vyote.
Ili kufikia lengo hilo, mkoa unatekeleza mikakati minne ambayo ni pamoja na kutoa huduma za majumbani kwa wagonjwa wa Ukimwi, tiba na huduma muhimu kwa wagonjwa wa Ukimwi na watu wanaoishi na VVU, kuanzisha mapambano dhidi ya Ukimwi sehemu za kazi katika sekta ya afya na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz anatilia shaka takwimu hizo. Anawataka wataalamu kukaa upya na kuzitafiti ili kujua kama kweli ni hali halisi.
“Pamoja na mikakati yetu, wataalamu kaeni mfanye utafiti upya tujue kama kweli hizi ndizo takwimu au siyo na kama ni kweli, kuna kila sababu ya kutangaza hali ya hatari kwa mkoa huu,†anasema
Wananchi wanasemaje?
Wakazi wengi wa Mkoa wa Iringa wanataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutoa elimu ya ukimwi na kuhakikisha kuwa misaada na fedha zinazotolewa kwa ajili ya janga hilo zinawafikia walengwa.
Lakini wanashangazwa na kitu kimoja. Ikiwa wengi wanalalamikiwa kwa kufanya ngono zembe baadhi ya maeneo hayana kondom na mengine watalaamu hawajawaeleza kinagaubaga juu ya matumuzi na umuhimu wake
 
Bee usimkumbushe Geoff mambo haya bee!
Ameshatoka huko, ameshaachana na hii maneno!..Unataka aombe likizo ya ghafla aisee babaake...hapana aisee!
 
hahaha MKuu Kilimasera unanikumbusha miaka ya tisini nasoma kule Iringa. Ulanzi kwa lugha ya Vijana tukiuita KITETE. Nyie mlienda Indiuka (Ndiuka) mlifika Ipogoro pale? kuna kilabu kikubwa sana cha Mzee Mwagongo? pale ni Noma. Kwa ufupi Vijana kwa watoto wa Iringa kuanzia miaka nane wote anakunywa ulanzi. Kwa kipindi hiki cha mvua ndo balaa kila Kaya atleast shambani kwao kuna VITINDI (mianzi inayogemwa Ulanzi). so mkitoka shambani kiburudisho cha kwanza ni ulanzi, hapo utakuta si watoto, akina mama, akina baba wote wanajiburudisha na hii kitu. Mimi nilikuwa na rafiki zangu wana mashamba ya ulanzi, tukiwa kijiweni tumejipumzisha tunapiga story hatukosi lita tano pembeni za MTOGWA, tunashusha taratiibu hapo tunasubiri saa kumi kwenda mazoezini pale Ipogoroo shule ya msingi kwenye chama letu enzi hizo ligi daraja la tatu. nilibahatika sikuwa sana nimejikita kwenye mambo ya ngono hata wale rafiki zangu karibu wote wapo Arusha sasa hivi ILA takriban jirani zetu wote(Akina BABA au MAMA au kaka au dada) kila unayeuliza unaambiwa ameshakufa kwa NGOMA. kweli inasikitisha kuna jamaa mmoja alikuwa na Gereji pale Ipogoro karibu na stendi mpya, ikiitwa km sikosei Masasi Garage (alikuwa Jirani yangu) na yeye Ngoma ilimuondoa ukienda maeneo yale ukiiulizia utalia kila family imeondokewa na kipenzi chao sababu ya huyu NGOMA -Kweli tubadili tabia ama laa TUTAKWISHA.
 
kuna ulanzi wa BANDABICHI PALE IFUNDA.........we acha.......Afu kuna wale wanaosafirisha toka Ifunda/Ihemi..yaaki wanakuwa na kile kidumu cha lita 5 pale juu yalita ishirini katika baiskeli zao.............uwakute mteremko wa ihemi huku wakinyonya mrija toka kwenye lita 5.....UTACHOKA.........anafika nao mjini akiwa bwiiiiiiiiiiiiiiiii.........
 
Takwimu kutoka Manispaa ya Iringa wanaelezea kuna zaidi ya vilabu 100 za pombe ya kienyeji ziinazotambuliwa na Manispaa hiyo na kila klabu ya pombe huuza debe 10 mpaka 20 za ulanzi kwa siku huuzwa lita 30000 mpaka 40000 za ulanzi kwa siku lita moja kipindi cha masika huuzwa 100 mpaka 150 turnover ya ulanzi manispaa iringa hufikia mpaka 4,5000.000/- kwa siku kwa mwezi shs 135.500.000/-kwa mwezi.msimu wa ulanzi huanza Dec-May kwa miezi sita 6*135.5000.000 =810.000.000/=
Asilimia kubwa ya wanyawaji wa ulanzi ni watu wa hali chini!Hapo ni manispaa tu !!!sijui mkoa mzima itakuwa wanakunywa lita ngapi za ulanzi kwa siku!!!!
 
Inanukia biashara nzuri hapa, I think bottling the juice will earn me money,thanks for your analysis.
 
Bee usimkumbushe Geoff mambo haya bee!
Ameshatoka huko, ameshaachana na hii maneno!..Unataka aombe likizo ya ghafla aisee babaake...hapana aisee!
hahahahahaha!naomba umkataze huyo...!(BTW:hali ya hewa leo dar INAFAVOUR SANA NDOA CHANGA:D:D)
 
Mi nataka kunywea kwenye kitindi bee!!
sio kitindi ile inaitwa mbeta ambayo hutundikwa kwenye kitindi kukinga ulanzi!wanasema ukinywea mle ni sawa na kunywa maji ya dafu kwenye dafu lake yaani unapata kitu natural!
 
kuna ulanzi wa BANDABICHI PALE IFUNDA.........we acha.......Afu kuna wale wanaosafirisha toka Ifunda/Ihemi..yaaki wanakuwa na kile kidumu cha lita 5 pale juu yalita ishirini katika baiskeli zao.............uwakute mteremko wa ihemi huku wakinyonya mrija toka kwenye lita 5.....UTACHOKA.........anafika nao mjini akiwa bwiiiiiiiiiiiiiiiii.........

kaka ifunda nakupata kwa sana tu, ila tanangozi napo balaa pale, wakati ule tanangozi ilisifika mpaka watu wakasema kuna jamaa kajenga kabisa pipeline yake toka shambani kwake mpaka home kwake halafu ana reserve system yake eti katandaza mabomba km dawasco anawauzia watu ulanzi. pale njia panda ya tosa lita ishirini buku tu mwana dah kweli maisha yalikuwa matamu.
 
Tuacheni kasumba mbaya za kushabikia vya wazungu na kuponda vya asili,hv mtu akinywa ulanzi akafanya ngono zembe kuna tofauti gan na mtu akinywa bia na akafanya ngono zembe?,basi kwa taarifa yenu ulanzi na bia vyote ni vilevi na nna imani kubwa wote hapa waliotupia madongo kwenye ulanzi ni wanywaj wazuri wa bia na wakilewa ngono zembe kama kawa,tuacheni utumwa wa kifikra me nadhan mada ingekuwa ni kupinga unywaj wa pombe kwa ujumla na sio ulanzi pekee tubadirike bila hvyo vyetu daima vitakuwa vibaya vya wazungu vizuri!,iringa oyeeee!
 
Sore ofutopik,kumbe wewe ni she.Hongera.

Mhh labda ame-Cut and paste from somewhere without editing, otherwise hata mimi nasema hongera yake!!

Mhh Labda Iringa hata He wanakuwa reffered as mrembo, mmh hongera tena!!
 
Nimegema ulanzi kuanzia miaka 7 hadi namaliza shule ya msingi.najua kugema na pia najua ulanzi mzuri.jaman ulanzi ni zao kama pamba au kahawa ina maana zao la biashara.wengi tuliosoma iringa vijijini ulanzi umetusomesha.nakumbuka enzi za mwalimu lita 20 uliuzwa sh.20.ambayo ada ilikuwa sh.20!pili ulanzi ukinywa huwa unavunja viungo vyote,unakuwa ni mvivu hiyo ngono utafanya?pia ulanzi unaleta njaa sana swali ngono na njaa zinaendana?
 
"KARIBU mchumba, karibu unywe ulanzi, unataka mtogwa (uliogemwa leo) au mkangafu (wa siku nyingi) na mdindifu ulio fukiwa kwenye mchanga wiki 1 pia kuna baruti huo ni ulanzi uliokaa kama wiki 2 hv? Njoo ukae nami hapa usiogope! Mama Anita, lete lita moja fanya haraka mrembo asije akaondoka," hivyo ndivyo nilivyopokewa katika klabu cha pombe cha Ndiuka, Iringa.
Nilikwenda kufanyia kazi utafiti wa wataalamu unaosema kuwa moja ya sababu zinazochangia kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa wa Iringa ni ulevi hasa wa pombe za kienyeji.
Mmoja wa wauzaji wa pombe hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe anasema wakati wa msimu wa pombe ya ulanzi, wanywaji wengi hushindwa kuzuia tamaa zao za ngono na kujikuta wakijiingiza katika vitendo hivyo bila kinga.
"Ulanzi ukiwa mwingi ngono pia huwa nje nje! Ndiyo maana msimu wa ulanzi ukiisha tu wanawake wengi huwa na mimba zisizotarajiwa. Ulanzi ni hatari, unasababisha watu washindwe kujizuia na hatuwezi kuuacha kwani ni asili yetu," anasema.
Pombe hiyo iligunduliwa wakati wa utawala wa machifu wa kabila la Wabena katika Wilaya ya Njombe baada ya mti mchanga wa mwanzi kukatika na kuanza kutoa maji matamu.
Tangu wakati huo, pombe hiyo imekuwa ikithaminiwa na wakazi wa Mkoa wa Iringa na tayari imeshambaa na kufika katika maeneo mengine mengi hasa kusini mwa Tanzania.
Wanywaji wengi wa ulanzi wanasema bila shaka kwamba pombe hiyo inachangia kasi ya Ukimwi.
"Msimu wa ulanzi huwa unauzwa bei rahisi ambayo hakuna inayemshinda ndo maana watu wengi hulewa hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ngono bila kujiandaa kwani wanawake wengi wakishanunuliwa kinywaji hicho huwa wepesi kukubali," anasema Richard Mwenda.
Mtaalamu wa magonjwa ya ngono mkoani Iringa, Dk Paul Luvanda anasema pombe hiyo ndiyo kichocheo kikubwa cha ngono zembe hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi.
"Ulevi hasa wa pombe ya ulanzi unachangia kuongeza hamu ya kufanya ngono zembe, wengi wamejikuta wakipata maambukizi kutoka na pombe hii ambayo inaheshimiwa na wenyeji," anasema Dk Luvanda.
Ulanzi siyo kichocheo pekee, Luvanda anataja mila na desturi potofu ambazo jamii nyingi mkoani humo bado inaziendeleza. Miongoni mwazo ni kurithi wajane, kukosekana kwa usawa kijinsia, kutakasa wajane na wasichana, kuoa wake wengi, imani za kishirikina na kutotahiri.
Nyingine ni umaskini wa kipato. Maisha ya wananchi wengi ni duni.
Anasema kutobadili tabia licha ya elimu ya ukimwi kuwafikia wananchi na wengine kuathiriwa kwa njia moja au nyingine na Ukimwi ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ugonjwa huo.
Anataja sababu nyingine kuwa ni muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli nyingi za biashara na ongezeko la taasisi mbalimbali mkoani humo.
Hali ya maambukizi ikoje?
Dk Luvanda anasema watu 17,555 kati ya 71,628 waliojitokeza kupima kwa hiari kati ya Julai 2008 hadi Juni 2009, walikutwa na maambukizi ya VVU. Hali inayoonyesha kwamba maambukizi yameongezeka na kufikia asilimia 24.5 hali ambayo ni hatari.
Anasema kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa hali ya ukimwi kitaifa mwaka 2003/2004, maambukizi yalikuwa asilimia 13.4 na mwaka 2007/2008 yakapanda na kufikia asilimia 15.7.
"Utafiti unaonyesha Iringa tupo asilimia 24.5, hii siyo hali ya kawaida hata kidogo." Anasema Wilaya ya Makete inaongoza kwa kuwa na asilimia 35.9, Njombe 31.9, Iringa 30.5, Mufindi 24.0, Manispaa 23.5, Ludewa 18.6, Njombe mjini 21.1 na Kilolo 12.2.
Hadi Juni 2009, wananchi walioandikishwa kweny mpango wa dawa za kupunguza makali ni 51,137 na walioanza kutumia dawa hizo ni 25,703.
Wakati maambukizi ya Ukimwi mkoani Iringa yakiongezeka kwa kasi, takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa yamepungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi asilimia 5.8 mwaka 2007.
Hiyo ina maana kwamba Mkoa wa Iringa ndiyo wa kwanza nchini kwa kuwa na kiwango cha juu kabisa cha maambukizi, ukifuatiwa na Dar es Salaam yenye asilimia 8.9 na wa tatu ni Mbeya yenye asilimia 7.9.
Kutokana na kiwango hicho cha maambukizi mkoa unakisiwa kuwa na watu 246,935 wanaoishi na VVU/Ukimwi kati ya wakazi wake wote zaidi ya milioni 1.5 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.
Idadi ya watoto yatima nayo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na wazazi wengi kupoteza maisha. Watoto 67,915 wameshatambuliwa na 30,303 wanapatiwa misaada ya chakula, mavazi, malazi na elimu.
Mkoa unafanya nini?
Kupaa kwa takwimu za maambukizi ya Ukimwi kunaonyesha kuwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na mkoa huo kupambana na janga hilo zimegonga mwamba.
Hata hivyo, Dk Luvanda anasema umeandaa mkakati wa kupambana na kasi hiyo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2008 utakaomilika Septemba 2012 ukilenga kupunguza kasi hiyo kwa asilimia 50.
Anasema tayari Sh1.8 bilioni zimeshatumika kuanzia Juni 2008 hadi June 2009. Kati ya fedha zilizotumika, Sh953.9milioni ni kutoka serikali kuu wakati Sh870.1milioni ni michango wa wadau mbalimbali wanaoshiriki katika mapambano ya Ukimwi Iringa.
Dk Luvanda anasema Wilaya ya Makete ilitumia Sh 942.5milioni, Ludewa 150.7milioni, Manispaa 22.2 milioni, Iringa Vijijini 116.2 milioni, Kilolo 54.6 milioni, Mufindi 442.6 milioni na Wilaya ya Njombe ilitumia Sh114.8 milioni.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Ezekiel Mpuya anasema mkakati huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mapambano dhidi ya Ukimwi katika halmashauri za wilaya na kuwa umeandaliwa kwa kuzingatia vipengele vilivyomo katika Mkakati wa Pili wa Taifa wa Mapambano ya Ukimwi (NMSF) wa mwaka 2008 hadi 2012.
Mpuya anasema mpango huo umezingatia pia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali walio katika mapambano ya Ukimwi mkoani Iringa, pamoja na maelekezo ya wataalamu wa ndani ya mkoa na taifa.
Anasema mipango iliyoibuliwa inatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja na kutathminiwa kila mwaka kisha kuendelezwa na mipya kuibuliwa kulingana na matokeo ya tathmini.
Anasema huduma za tiba zinatolewa katika hospitali 16 zilizopo mkoani Iringa na vituo vya afya 14 kati ya 26. Lengo ni kufikia vituo vya vyote.
Ili kufikia lengo hilo, mkoa unatekeleza mikakati minne ambayo ni pamoja na kutoa huduma za majumbani kwa wagonjwa wa Ukimwi, tiba na huduma muhimu kwa wagonjwa wa Ukimwi na watu wanaoishi na VVU, kuanzisha mapambano dhidi ya Ukimwi sehemu za kazi katika sekta ya afya na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz anatilia shaka takwimu hizo. Anawataka wataalamu kukaa upya na kuzitafiti ili kujua kama kweli ni hali halisi.
“Pamoja na mikakati yetu, wataalamu kaeni mfanye utafiti upya tujue kama kweli hizi ndizo takwimu au siyo na kama ni kweli, kuna kila sababu ya kutangaza hali ya hatari kwa mkoa huu,†anasema
Wananchi wanasemaje?
Wakazi wengi wa Mkoa wa Iringa wanataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutoa elimu ya ukimwi na kuhakikisha kuwa misaada na fedha zinazotolewa kwa ajili ya janga hilo zinawafikia walengwa.
Lakini wanashangazwa na kitu kimoja. Ikiwa wengi wanalalamikiwa kwa kufanya ngono zembe baadhi ya maeneo hayana kondom na mengine watalaamu hawajawaeleza kinagaubaga juu ya matumuzi na umuhimu wake
Ndugu yangu,hapo kwenye RED umedanganya be.Wanyalukolo tunarithi wake lakini hatutakasi wajane na wasichan ahamna hiyo kitu.Nimezaliwa kijijini na kukulia huko nami ni wa kike hamna hiyo kitu.Dini de!
 
Vanyalukolo sitwaitakasa vamama na vadala bee, ipo udetite bee. Wahehe hatutakasi mtu wangu, ila mila ya kurithi ipo. Pia ulanzi hauleti hamasa ya ngono coz huwa inavunja joints zote za mwili na kuleta njaa. Kwa kifupi huwezi kupata nguvu za kuzini. Kinachopelekea uzinzi Iringa nadhani ni baridi kali iliyopo kule. Makete baridi yake unaweza ganda bt ndio kwenye maambukizi makubwa zaidi, mbeya pia kuna baridi kali, pia kuna maambukizi makubwa. I thnk there is direct relatnship btn cold weather and ngono holela, fanyeni utafiti wadau, fanyen correlation analysis ya hiyo ki2 barid na sex
 
ye uvanzile amatata be
Ndugu yangu,hapo kwenye RED umedanganya be.Wanyalukolo tunarithi wake lakini hatutakasi wajane na wasichan ahamna hiyo kitu.Nimezaliwa kijijini na kukulia huko nami ni wa kike hamna hiyo kitu.Dini de!
 
Daah umenikumbusha njia panda tosa kwa akina maembe.ulanzi ugali na mboga ya figiri chukuchuku.debe linaisha hv hv mtu 2.we acha tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom