Unywaji pombe, uvutaji sigara na kuongezeka uzito huchangia kutopata hedhi kwa wanawake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
KUTOPATA HEDHI KWA WANAWAKE




alcohol%20drinking.jpg

Vichangizi vya mwenedo mbaya wa maisha (lifestyle factors) ya kila siku kwa wanawake, huchangia wanawake kuacha kupata hedhi, hii ni kutokana na utafiti uliofanya na kituo cha utafiti wa saratani nchini Uingereza (Institute of Cancer Research in UK).

Uvutaji sigara ndio huathiri zaidi wanawake na kuwafanya wanawake wavutaji sigara kuingia katika hatua hii ya kuacha kupata hedhi miaka miwili mapema zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawavuti sigara.

Hata hivyo kuongezeka uzito kumeonekana kuwa na matokeo ghasi kwani, kuongezeka uzito kunasababisha mwanamke kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa. Hii inahusishwa na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene/walio na uzito ulopitiliza) na homoni za kujamiana (sex homones).

Wanawake huingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa zaidi kwa mwaka mmoja kama watakuwa wanakunywa chupa mbili za pombe kwa siku kwa wale walio na umri kati ya miaka 25 na 49, au wale wanaofanya mazoezi mazito mara kwa mara kati ya umri wa miaka 39 na 49 au wale ambao hawali nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian).

Matokeo ya utafiti huu ni muhimu sana kwani kuchelewa kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi ni moja ya vihatarishi vya kupata saratani ya matiti kama ilivyoelezwa katika jarida laMyHealthDailysNews.

“Utafiti huu umeonesha jinsi mwenendo wa maisha wa kila siku wa mwanamke unavyoathiri kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi au menopause kama inavyojulikana kitaalamu na tafiti zaidi zinahitajika ili kuweza kujua kama kupunguza kiwango cha unywaji pombe na ufanyaji mazoezi hubadilisha umri wa mwanamke wa kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi” alisemaDr Danielle Morris ambaye ndiye aliyekuwa mtafiti mkuu katika utafiti huu.
Utafiti huu uliochapishwa katika jarida la American Journal of Epidemiology na uliotumia takwimu za wanawake 50,000 ambao wanahusika katika utafiti wa Breakthrough Generations Study nchini Uingereza.
obese%20woman.jpg


Watafiti hao walitumia takwimu kutoka kwa wanawake walio na umri wa miaka 40 na 90 ambao kwenye dodosa ya maswali walijaza umri, uzito, ufanyaji mazoezi wao na kama wameshaingia katika menopause au la.

Menopause ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana
na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiana (hivyo kusababisha kupungua

kwa hamu ya kujamiana kwa mwanamke), tupu ya mwanamke kuwa kavu(vaginal dryness), mood swings, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala (sleep disturbances),matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
http://www.tanzmed.com/component/k2/item/263-unywaji-pombeuvutaji-sigarakuongezeka-uzito-huchangia-kutopata-hedhi-kwa-wanawake.html

 
Back
Top Bottom