Unywaji pombe, uvutaji sigara na kuongezeka uzito huchangia kutopata hedhi kwa wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unywaji pombe, uvutaji sigara na kuongezeka uzito huchangia kutopata hedhi kwa wanawake

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  I


  [​IMG]
  Vichangizi vya mwenedo mbaya wa maisha (lifestyle factors) ya kila siku kwa wanawake, huchangia wanawake kuacha kupata hedhi, hii ni kutokana na utafiti uliofanya na kituo cha utafiti wa saratani nchini Uingereza (Institute of Cancer Research in UK).

  Uvutaji sigara ndio huathiri zaidi wanawake na kuwafanya wanawake wavutaji sigara kuingia katika hatua hii ya kuacha kupata hedhi miaka miwili mapema zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawavuti sigara.

  Hata hivyo kuongezeka uzito kumeonekana kuwa na matokeo ghasi kwani, kuongezeka uzito kunasababisha mwanamke kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa. Hii inahusishwa na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene/walio na uzito ulopitiliza) na homoni za kujamiana (sex homones).

  Wanawake huingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa zaidi kwa mwaka mmoja kama watakuwa wanakunywa chupa mbili za pombe kwa siku kwa wale walio na umri kati ya miaka 25 na 49, au wale wanaofanya mazoezi mazito mara kwa mara kati ya umri wa miaka 39 na 49 au wale ambao hawali nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian).

  Matokeo ya utafiti huu ni muhimu sana kwani kuchelewa kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi ni moja ya vihatarishi vya kupata saratani ya matiti kama ilivyoelezwa katika jarida la MyHealthDailysNews.

  “Utafiti huu umeonesha jinsi mwenendo wa maisha wa kila siku wa mwanamke unavyoathiri kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi au menopause kama inavyojulikana kitaalamu na tafiti zaidi zinahitajika ili kuweza kujua kama kupunguza kiwango cha unywaji pombe na ufanyaji mazoezi hubadilisha umri wa mwanamke wa kuingia katika hatua ya kuacha kupata hedhi” alisema Dr Danielle Morris ambaye ndiye aliyekuwa mtafiti mkuu katika utafiti huu.
  Utafiti huu uliochapishwa katika jarida la American Journal of Epidemiology na uliotumia takwimu za wanawake 50,000 ambao wanahusika katika utafiti wa Breakthrough Generations Study nchini Uingereza.
  [​IMG]

  Watafiti hao walitumia takwimu kutoka kwa wanawake walio na umri wa miaka 40 na 90 ambao kwenye dodosa ya maswali walijaza umri, uzito, ufanyaji mazoezi wao na kama wameshaingia katika menopause au la.

  Menopause ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiana (hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiana kwa mwanamke), tupu ya mwanamke kuwa kavu (vaginal dryness), mood swings, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala (sleep disturbances),matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
  Unywaji Pombe, Uvutaji Sigara na Kuongezeka Uzito Huchangia Kutopata Hedhi kwa Wanawake

   
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuongezeka uzito somehow kunachelewesha kupata hedhi kweli, kipindi flan nilipokuwa home wakati wa skuli holiday niliongezeka kgs kutoka 49 mpaka 52,baada ya hapo nilikaa siku 39 bila kupata hedhi nikaingia net nikasoma makala mbalimbali kutafuta chanzo cha hali hiyo kwani sikuwa nimefanya ngono kwa wakati huo,so mbali na mimba nikapata knowledge kuwa uzito huchangia hali hyo and after 39 days nikapata hedhi.
   
Loading...