Unyonyaji wa Madalali wa mazao sasa imetosha

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,277
Ni kikundi cha watanzania ambao wamemua kutengeneza mtandao wa masoko kwa bidhaa za kilimo ambao utapunguza kwa kiwango cha juu utapeli wa madalali ambao Leo hii wanachukua asilimia 40 Ya mzigo wote uliouza bila kujali mtaji wa mkulima. Tunayo mifano ya watu ambao walikumbana na hili na hivyo tumeona ni hitaji la msingi.

Mtandao huo wa masoko tulioamua kuuanzisha unahitaji watu maana tutakuwa tunatafuta taarifa zote za masoko kwa jiji la Dar es salaam, mikoani na hata nje ya nchi... na hivyo tutawapatia wakulima taarifa hizo na wao badala ya kulipa asilimia 40 ya mzigo waliouza wanaweza kulipa asilimia 15 tu ya faida waliyopata kwenye process nzima (hii hela itatumika kwenye shughuli za mitandao huo ikiwemo kutafuta taarifa na mawasiliano mbali mbali).

Huu mtandao utasajiliwa kama company by guarantee na aina hii Ya company haina share ni kampuni inayooperate kama NGO na viongozi wake wana patikana kwa kuchaguliwa na ina fanya kazi yá jamii Kama Kusaidia jamii kwenye mambo mbali mbali unaweza kutoa huduma yeyote ilimradi iwepo kwenye memorandum na utaweza kuichukulia compliancy ya NGOs.

Tafadhali hatuhitaji madalali.

--------------------------------
Clarifications kulingana na muitikio wenu:
15% ni mfano umewekwa kumaanisha kwamba gharama itakuwa ndogo kuliko ilivyo sasa hivyo basi makubaliano yatafikiwa na kupunguza hadi kiasi ambacho hakitamuumiza mkulima. Bado tuko kwenye mchakato wa kuangalia hili swala liwe na sura gani. Hivyo basi maoni yenu yanakaribishwa sana ili kuboresha mtandao huu.
Kwa hali ilivyo sasa ni kweli kwamba huwezi kupenya soko bila mkono wa Dalali. Hawa madalali wanatoza fedha kubwa kiasi kwamba unatamani kulia wala hawajali kama una faida au hasara. Huu ni ukombozi kwa maana unapunguza mzigo wa gharama. Kwakuwa bado swala la udalali limegoma kwisha ni vyema kuandaa scheme mbadala ambazo zinapunguza mzigo. Uzuri wa mtandao wetu hautagusa gharama zauzalishaji. Tutapimaje hili? Kwakuwa ni mtandao basi tutakuwa na taarifa zote za gharama ya uzalishaji au manunuzi. Mnaopinga tumekubali hoja zenu ila tunaamini kwamba angalau kwa kiasi kikubwa mkulima amepunguziwa gharama.
 
Mrs Bishanga,
With all due respect kama nimekuelewa vizuri kwenye thread yako na wewe utakuwa ni Dalali (Broker). Kama unaijua biashara ya mazao vizuri utakubaliana na mimi kwamba katika biashara ya mazao huwezi kukwepa Madalali.....na hii ni kwa ulimwengu mzima.

Kwa mujibu wa thread yako wewe ni Dalali Ila unatumia teknolojia kuunganisha Wakulima na Wanunuzi. Otherwise usingekuwa una charge hiyo 15%. Huduma yenu ingekuwa bure ili kuwasaidia wakulima kuondokana na unyonyaji.
All the best.
 
Mrs Bishanga iyo ni good idea. Unabase wapi wewe, maana huwezi dalalia mwenyewe, utahitaji subordinates.
 
Utawaona wapi wakati wanapinaa kila hatua ya maendeleo chini ya JPM, wako busy na kutafuta definition za dikteta ili wamchafue rais wetu
Matapeli tu nyinyi twendeni shambani mimi nilime wewe uchukue aslimia 15?.acheni usanii Serikali haina msaada wowote kwa mkulima acheni porojo
 
Elimu kwanza, wakulima wengi elimu yao ni ya kawaida. Hili ni jambo jema na ni hatua muhimu kupunguza unyonyaji kwa wavuja jasho. Ninachoshauri ni elimu ya kutosha kubadili mind set za wakulima wetu ambao walishazoea mfumo huo wa unyonyaji.
 
15% ni mfano umewekwa lakini makubaliano yatafikiwa na kupunguza hadi kiasi ambacho hakitamuumiza mkulima.
Kwa hali ilivyo sasa ni kweli kwamba huwezi kupenya soko bila mkono wa Dalali. Hawa madalali wanatoza fedha kubwa kiasi kwamba unatamani kulia wala hawajali kama una faida au hasara. Huu ni ukombozi kwa maana unapunguza mzigo wa gharama. Kwakuwa bado swala la udalali limegoma kwisha ni vyema kuandaa scheme mbadala ambazo zinapunguza mzigo. mpango wa namna yoyote unahitaji fedha kwa hivyo ili tuwasaidie wakulima na wanaouza mazao ya kilimo hawana budi kuchangia gharama kidogo. Uzuri wa mtandao wetu hautagusa gharama za uzalishaji. Tutapimaje hili? Kwakuwa ni mtandao basi tutakuwa na taarifa zote za gharama ya uzalishaji au manunuzi. Mnaopinga tumekubali hoja zenu ila tunaamini kwamba angalau kwa kiasi kikubwa mkulima amepunguziwa gharama
 
Udalali hauwezi isha kamwe, the only ways kuwa by pass madalali ni kupitia Contract Farming, Bila kuwa na contract farming madalali hawaepkiki, Ila mtu akilima nuku anjua anenda kumuuzia nani na kwa sh ngapi huwezi waona madalali, togfati na hapo ni hakuna
 
Mrs Bishanga. Kama dalali unatarajia vipi kupata kipato kupitia utaratibu wako ?
 
Mleta mada mnaweza kumGARANTEE mkulima kwamba atauza mzigo wake isijekuwa nyie mkishapata Taarifa za soko mnakuwa Ofisini...then mizigo inapofika mnawafuata hao madalalo wauze....Kuuvunja mtandao wa Udall I kwenye Biashara ya Mazao sio issue ya kitoto..
 
Back
Top Bottom