Unyonyaji unaofanywa na mwekezaji Estate Highland Ltd kwa wananchi Mbarali, Rais ingilia kati sisi tumechoka mbunge wetu anatutesa kwa fedha zake

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
2,991
2,000
HIGHLAND ESTATE LTD kampuni ya kibepali iliyopo kwa mgongo wa uwekezaji katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inayomilikiwa na Mbunge wa CCM Mh Haroon Mulla wa jimbo la Mbarali imekuwa mwiba kwa sisi wananchi wa wilaya hii.

Kampuni hii imepora Ardhi kwa wana nchi wa wilaya hii kinyume cha utaratibu wa sheria za nchi kutokana na fedha za mwekezaji kuwa chambo kwa baadhi ya watendaji wa Serikali wasio waaminifu, wako tayari kupokea rushwa ili kumlinda mwekezaji na kuwaumiza wananchi.
SERA YA TAIFA YA ARDHI YA MWAKA 1995 INASEMA.

Ili kutatua matatizo yaliyotokana na sheria y ardhi ya mwaka 1923 (no.113) iliyoridhiwa kutoka kwa wakoloni, serikali iliandaa sera ya Taifa ya ardhi iliyokamilika na kutolewa mnamo mwaka wa 1995 amabayo ni pamoja na mambo mengine nipamoja na
 • Jinsi ya kuongoza ugawaji na umilikaji matumizi bora ya ardhi na kueleza namna ya kutatua migogoro ya ardhi.
 • Kutambua kuwa ardhi yote ni mali ya Umma na imekabidhiwa kwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya Raia wote.
 • Kuhakikisha kwamba haki zote zilizopo katika ardhi na umilikaji wa ardhi kwa mda mrefu unatambulika na kufafanuliwa na kulindwa kisheria.
 • Kuweka mfumo madhubuti rahisi na wazi wa kusimamia kwa ufanisi masuala ya ardhi.

 • MAANA YA SHERIA YA ARDHI YA KIJIJI KWA MJIBU WA SHERIA. ARDHI YA KIJIJI NI
 • 1.Ardhi iliyondani ya mipaka ya vijiji vilivyo sjiliwa chini ya sheria ya serikali ya mitaa (mamlaka za wilaya ya mwaka 1982) Sura ya 287. Kama zilivyorekebishwa mwaka 2002 na kujumuisha pia vijiji vilivyohusishwa chini ya sheria ya makazi ya mwaka 1965.
 • 2.Ardhi ambayo imemilikiwa na wanakijiji kwa miaka 12 na zaidi kabla au baada ya kaunza kutumika kwa sheria hii.
 • 3.Halmashauri ya kijiji, kusimamia ardhi ya kijiji kwa niaba ya wanakijiji wote.

 • KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 TOLEO LA 2005 UK.34, IBARA 24 KIFUNGU 1 INASEMA ( “Kilamtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mjibu wa sheria.” Kifungu kidogo chapili cha katiba hii ibara hii 24 kinasema (Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote Yule kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kutaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.

 • Kwa mjibu wa baadhi ya sheri hapo juu kwetu watu wa Mbarali tumeonewa sana na huyu mwekezaji, tunaushahidi usio na shaka kuwa anawatumia baadhi ya watendaji wa serikali ngazi ya wilaya, Mkoa na baadhi ya viongozi wa juu pia na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi wapo kwenye payment yake.
 • Huyu mwekezaji amepola mashamba ya wanakijiji aidi ya ekali 3500 mashamba ya mpunga na kujimilikisha yeye mwenyewe ,sisi tumejitahidi kutoa malala miko yetu kwa Mkuu wetu wa wilaya, hakuna utekelezaji tukatoa kwa mkuu wa Mkoa pia hakuna utekelezaji tulienda mbele hadi kwa waziri wa Ardhi . Ameagiza hili swala lipatiwe ufumbuzi lakini hakuna lolote.
 • Hivyo basi tunaomba Mh Rais Dr Joseph Pombe Magufuli ingilia kati swala hili lipatiwe ufumbuzi mapema.
 • Wananchi tumechoka kunyimwa haki tumetuma barua nyingi sana huko ngazi za juu hakunautekelezaji hatujui wanaogopa nini kutatua hili swala, Kampuni hii inafanya maovu sana huku yanayofahamika wananchi tumechoshwa lakini hakuna hatua madhubuti zinazo chukuliwa kumdhibiti huyu mhusika.
 • ITAENDELEA................
 

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,370
2,000
Huyo si mbunge ambaye JPM alimpa misifa mingi hadi akasema angekuwa ana mamlaka angemuhamishia jimbo la Chato kwa vile ana mwitikio la maendeleo kwa sana
 

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
2,991
2,000
Huyo si mbunge ambaye JPM alimpa misifa mingi hadi akasema angekuwa ana mamlaka angemuhamishia jimbo la Chato kwa vile ana mwitikio la maendeleo kwa sana
JPM alisema vile kulinda chama jamaa anamadudu sana sijui kwanini hawayaoni
 

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
5,675
2,000
Mkajiandikiahe kupiga kura ... Mnalalamika nini na mna mbunge wa ccm .... Maendeleo yataenda kwenye viongozi wa ccm tu ... Ndio maendeleo hayo mtulie dawa iingie vizuri
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,078
2,000
Mtaweza kutunza mifumo ya umwagiliaji ulioasisiwa na wenyeji wenzenu kabila la Wabulushi? Maana kutunza mifumo hiyo inatakiwa uwe na uchungu nao kuanzia vizazi na vizazi siyo siasa siasa tu.
Source kwa hisani kubwa sana ya :
MbeyaYetuOnlineTV
 

Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,445
2,000
acheni fitina nyie si ndio mlienda kufukia bunduki shambani kwake ili aonekane jangili? ardhi mmemuuzia wenyewe, baada ya pesa kunywea ulanzi na kuisha ndio mnalalamika
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,078
2,000
Ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji maji bonde la Usangu
Source kwa hisani kubwa ya : MbeyaYetuOnlineTV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom