Unyenyekevu na umuhimu wake katika ndoa na mahusiano

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Kuna fadhila nyingi sana katika ulimwengu huu lakini hakuna fadhila iliyo kuu kama fadhila ya unyenyenyekevu. Unyenyekevu sio udhaifu bali unyenyekevu ni hali ya moyo na akili inayomfanya mtu ajikubali alivyo na awakubali wengine walivyo. Ni hali ya mtu kutambua analopaswa kutenda na analitenda na pia asilopaswa kulitenda halitendi. Ni hali ya mtu kujishusha na kujiona kuwa si kitu. Ni hali ya kuwajali zaidi watu kuliko kujijali na kujipendelea sisi wenyewe. Ni hali ya kuonyesha upendo wetu zaidi kuliko kutaka kupendwa. Ni hali ya kuwaheshimu zaidi wenzetu kuliko kutaka kuheshimiwa.

Kwa njia ya unyenyekevu, tunaweza kufundishwa, kuelekezwa, kuongozwa, kuonywa, kulindwa, kutetewa na kukuzwa kwa ujumla. Ni fadhila ya msingi sana katika maisha ya mahusiano ya kila siku katika familia na katika jumuiya yoyote ile ya watu. Hata marafiki wa kawaida tu au wachumba wakikosa unyenyekevu basi mahusiano yao daima hayatakosa malumbano, matusi, dharau, ukandamizaji na kila aina ya mateso.

Wakati mwingine watu hushindwa kuishi na sisi kwa sababu tunakosa unyenyekevu, na ndio maana, hatuonyeki, haturekebishiki hatupendeki, hatuelekezeki, hatufundishiki, daima tunajiona kuwa ndio wenye haki sana mbele za watu na mbele za Mungu.

Ndoa ama uhusiano wowote wa kimapenzi usiokuwa na unyenyekevu, daima huwa ni uwanja wa vita. Vita za maneno na za mikono hazitakwisha.

Watu katika mahusiano, wakinyenyekeana wao kwa wao wanakuza zaidi upendo wao. Kiburi, maringo, dharau na majivuno, hufukuza upendo lakini unyenyekevu hukuza na kudumisha upendo. Inapotokea kwa sababu zozote watu katika mahusiano wanaoneshana umwamba, hakuna anayetaka kujishusha hata pale linapotokea kosa, hapo upendo na furaha ya maisha ya ndoa na mahusiano huingia katika dosari kubwa.

Ndoa na mahusiano mengi yameingia katika migogoro ya kudumu sio kwa sababu ya matatizo makubwa, hapana! Pengine migogoro hiyo inasababishwa na makosa madogomadogo ya kawaida kabisa ya kibinadamu. Lakini kwa vile hakuna ile hali ya unyenyekevu, yaani kuwa tayari kujishusha, kila mtu anataka kujionesha yeye ni zaidi, na yupo sahihi zaidi ya mwenzake; hapo ndipo mgogoro hukuzwa zaidi.

Enyi vijana wenzangu mliopo kwenye ndoa na hata wale ambao wanatarajia kuingia kwenye ndoa; mkitaka amani, utulivu na maelewano ndani ya ndoa na mahusiano yenu, muwe wanyenyekevu. Komesheni vilema vya kiburi, dharau, kujiona na maringo. Unyenyekevu ni daraja ya kufikiana na kuafikiana. Ukiwa mnyenyekevu, hata pale unapopatwa na tatizo, mwenzi wako ni rahisi kukuelewa, kukupokea na kukuinua. Lakini ukikosa unyenyekevu, utamfanya mwenzio ashangilie ukipatwa na mabaya.

Unyenyekevu, ni kitu cha kutuweka katika mazungumzo yenye mwafaka daima. Bila unyenyekevu, kila neno ama jambo utakalotenda litakuwa na chanzo cha fujo.

Kwa wale wanandoa ambao ni wazazi nawaasa muwe mfano kwa watoto wenu. Mkiwa wanyenyekevu, watoto wenu wataiga mwenendo wenu wa unyenyekevu nao pia watawafundisha watoto wao unyenyekevu.

Cc: ladyfurahia
 
Unyenyekevu, ni kiti cha kutuweka katika mazungumzo yenye mwafaka daima. Bila unyenyekevu, kila neno ama jambo utakalotenda litakuwa na chanzo cha fujo.

Kwa wale wanandoa ambao ni wazazi nawaasa muwe mfano kwa watoto wenu. Mkiwa wanyenyekevu, watoto wenu wataiga mwenendo wenu wa unyenyekevu nao pia watawafundisha watoto wao unyenyekevu.

Cc: ladyfurahia
Asante kwa somo zur
 
Back
Top Bottom