Unyanyasaji wa polisi (FFU) wanaolinda Ikulu dhidi ya raia - 20/09/2011

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,068
183
Jamani hii imetokea jioni hii pale Magogoni, nia inayopita Ikulu kutokea Ferry kuelekea Upanga! Mtangajika mmoja amepita akiendesha gari muda mfupi baada ya saa 12 Jioni, cha ajabu FFU waliokuwa zamu wakamkimbiza kwa kuwa hairuhusiwi kupita pale muda huo, kijana wa watu akasimama na kujieleza kuwa hakuona kibao na ni mgeni, Cha kushangaza aliamuriwa yafuatayo:-
1. Alipe faini ya shilingi 80,000/= (ambayo baaday eilipunguzwa hadi kufikia 50,000/= baada ya kjana yule kulalamika kuhusu hilo). Na hat ahiyo elfu 50, masikini yule kijana hakuwa nayo, alikuwa na 5000/= tu mfukoni!!! ALipoeleza hayo wale askari wakamnyang’anya hele hizo na kasha wakamwambia kwa kuwa amekosa faini basi watamuadhibu hapo hapo!!
2. ADHABU: Kijana wa watu alichangiwa kwa kupigwa sana mateke na virungu na askari hao, pamoja na kumnyang’anya hela yake aliyokuwa nayo (5000/=)!! Baadaye akatakiwa kuondoka mara moja eneo la tukio na kuelezwa kwamba endapo akikutana na askari wengine mbele ya safari wakimuona anatokea njia ile basi awaeleze kuwa “TAYARI AMEMALIZANA NA KIKUNDI HICHO CHA MWANZO”
Hii ni kweli imetokea, jioni ya leo (majira ya saa moja na nusu jioni) nanimejikuta nina maswali meeengi sana….
Hivi utaratibu uliopaswa kufuatwa ni upi?? Kama amekosa si angepelekwa moja kwa moja Central Police??
Inakuwaje Polisi wetu wanamvamia na kumshambulia raia amabaye hana silaha na amejisalimisha kwao?? Naelewa kupiga virungu ni pale tu endapo mtuhumiwa anakataa kukamatwa kisheria au anatiumia nguvu katika kuping akukamatwa kwake…hapo pia polisi hawa wlaipaswa kutumia “REASONABLE FORCE”!! Anaposhambuliwa raia mwema kama huyu, ambaya hajakaidi hat akidogo agizo la askari ni haki??
Wana JF naomba msaada wa mawazo, kama kuna mwenye anuaniya barua pepe ya Mh. Nahodha naomba msaada ili tuelimishane!! Hili halikubaliki na ni aibu kubwa kwa nchoi inayojisifia kuwa inaongoza kwa amani!
KAMA MH NAHODHA NA WATENDAJI WAKE WANASIKIA HILI HEBU FANYENI KAZI …..
 
macho yao yote barabarani badala ya ikulu.angekubali fine akalipe kituoni wampe na risiti(GRR)<br />
Hawana tofauti na wanaolinda MAJENGO ya benki wakiona umepita no entry wanaacha lindo.ndo maana watu wanaiba pesa na kuwapita mlangoni na smg zao..poor intelligence
 
Nchi hii haina utawala wa kisheria. Ndivyo walivyoagizwa na wakuu wao.
 
Jamaa akivaa zile suti za hongo analindwa na culprits, lol
 
Hao jamaa ma frustration kibao. Kazi zingine noma. Cha msingi jihadharini kupita hapo, watawatengua viuno.
 
Nadhani wanapenda sana madereva wakatize hapo ili wapate posho KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI! Rushwa hoyeeee
 
hukufanikiwa hata kupiga picha kwa simu yako? ungekuwa na evidence tungewabana wanatolewa gazetini na pia mkuu wao angepewa taarifa na ushahidi huo na vyombo vya hanari vingefuatilia hatma yao na yule kijana pia,
 
kuna mazigira ya kupigasimu mkuu vinginevyo kibao kingeweza kumgeukia yeye na hata kupoteza hiyo cmu yake.inf aliyotoa ni habari tosha unless kuna namna inakuhusu and you need more evidence unaweza ku-mpm mtoa habari kama yupo willing ku-coperate
 
This is not new. It happened to me more than 15 years ago when I was driving and showing my kids the animals in the state house compound from the side of magogoni road. Askari alipanda katika gari langu and ikanibidi nitoe hela. Sikumbuki ngapi lakini alikuwa na bunduki na mimi nilikuwa na watoto kwa hiyo sikutaka malumbano.
 
Fiction.

Faini ambayo unatakiwa kulipa hapo hapo, na halafu ni negotiable, ni rushwa. Walikuwa wanataka kupozwa.

Sasa polisi mkishindwana kwenye viwango vya rushwa hawezi kuanza kukupa kipondo, ataingia garini na kukuamuru uelekee to the nearest mazabe, all the while, negotiation zinaendelea.

Na kama ukipigwa hawezi tena ku strike a deal na wewe eti ukienda mbele ukimaindiwa na polisi wengine waambie tumeshamalizana na wengine huko nyuma, hiyo ni kama mlielewana ki-rushwa rushwa, sio kama ulipewa kipondo.
Ndivyo wanavyo operate. Unless kuna mengine yalitokea/yalijibizana hapo katikati.

Story hii imetiwa garlic salt, black pepper, curry powder, na all-purpose seasoning!
 
Na wewe kwa nini usipige picha ukaleta hapa? yasije kuwa majungu tu

Ndugu, niamaini, sian sababu ya kuleta majungu hapa! Ni kweli imetokea na imeniumiza sana! Sidhani kama jamaa angeweza kupiga picha katika mazingira hayo...si ndiyo wangemuua kabisa?
 
Fiction.

Faini ambayo unatakiwa kulipa hapo hapo, na halafu ni negotiable, ni rushwa. Walikuwa wanataka kupozwa.

Sasa polisi mkishindwana kwenye viwango vya rushwa hawezi kuanza kukupa kipondo, ataingia garini na kukuamuru uelekee to the nearest mazabe, all the while, negotiation zinaendelea.

Na kama ukipigwa hawezi tena ku strike a deal na wewe eti ukienda mbele ukimaindiwa na polisi wengine waambie tumeshamalizana na wengine huko nyuma, hiyo ni kama mlielewana ki-rushwa rushwa, sio kama ulipewa kipondo.
Ndivyo wanavyo operate. Unless kuna mengine yalitokea/yalijibizana hapo katikati.

Story hii imetiwa garlic salt, black pepper, curry powder, na all-purpose seasoning!

Are you one of them?? AU wewe ni mwakilishi wa Ikulu? Hakuna fiction hapo, believe me or believe them...
 
huwa wanaangalia kwanza ni mtu wa aina gani na una uwezo gani katika kujieleza........mi nilipita hapo saa 2 jioni nilisimamishwa na nikajieleza wakaniachia bila bughudha yeyote ila nisipite tena muda huo.......Acheni kulialia, jieleze..............
 
Acha kujishebedua,,,,unahisi hao polisi waliokushika ndio waliomshika jamaaa,,,????au kabla yako walishapita wangapi??????inawezekana walishakamata weng na wakahisi wanaweza kukuachia,kwan maeneo mangap huwa watu wanajieleza na hawasikilizwi???,je polisi watu ambao imewaua hawajui kujieleza,,,,,,,SHUKURU MUNGU IT WAZ UR LUCKY
huwa wanaangalia kwanza ni mtu wa aina gani na una uwezo gani katika kujieleza........mi nilipita hapo saa 2 jioni nilisimamishwa na nikajieleza wakaniachia bila bughudha yeyote ila nisipite tena muda huo.......Acheni kulialia, jieleze..............
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom