Unyanyasaji wa hali ya juu Arusha Sunrise Radio...

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU WANAHABARI SISI BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO ARUSHA KUANZIA LEO TAREHE 22/8/2012 TUMEAMUA KUGOMA KUENDELEA KUFANYA KAZI NA ASPIRE MEDIA COMPANY LIMITED AMBAO NDIO WAMILIKI WA SUNRISE RADIO 94.8 FM ARUSHA BAADA YA KUSHINDWA KUTIMIZIWA MAMBO KADHA WA KADHA TULIYOKUWA TUNAYAHITAJI.
MGOMO HUU ULIANZA KAMA MGOMO BARIDI MNAMO TAREHE 10/8/2012 BAADA YA SHEREHE ZA WAKULIMA NANE NANE NA HII NI BAADA YA KUTOKEA TOFAUTI KATI YA MKURUGENZI WA UFUNDI WA SUNRISE RADIO NDUGU DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO NA KAMATI YA SHEREHE ZA WAKULIMA NANE NANE MWAKA 2012 AMBAO NDIYO WALIOKUWA NA JUKUMU YA KURUSHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YAANI LIVE KUTOKA KATIKA VIWANJA VYA TASO NANE NANE NJIRO.
NDUGU WANAHABARI MGOMO HUU UMESABABISHWA PIA NA KUTOFANYIWA KAZI KWA MADAI YA WAFANYAKAZI, WAFANYAKAZI TUMEKUA TUKIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWANI:-
a) TUNALIPWA MISHAHARA MIDOGO ISIYOKIDHI MAHITAJI (MSHAHARA WA 100,000 NA WENGINE 170,000)
b) KUFANYISHWA KAZI BILA KUWA NA MIKATABA, TUKIDAI MIKATABA TUNAPIGWA TAREHE
c) KUTOKATWA MAKATO KWENYE MISHAHARA KWAAJILI YA PENSHENI
d) BAADHI YA WAFANYAKAZI KUFANYISHWA KAZI BILA KULIPWA
e) HAKUNA OVERTIME PAYMENT
f) WAFANYAKAZI KUTISHIWA KUFUKUZWA MARA KWA MARA PALE WANAPODAI HAKI ZAO
g) HAKUNA LIKIZO
h) WAANDISHI WA HABARI WALIORIPOTI LIVE YA UCHAGUZI WA ARUMERU MASHARIKI TAREHE 1/4/2012 KUTOLIPWA POSHO ZAO HADI LEO NA WENGINE WALIDAI NA HATIMAYE WAKAFUKUZWA KAZI
i) MISHAHARA WA WAFANYAKAZI KUCHELEWESHWA KULIPWA KWANI UTAKUTA MSHAHARA WA MWEZI HUU TUNAWEZA KULIPWA MWEZI UJAO KATIKATI AU MWISHONI
j) MKURUGENZI WA UFUNDI KUTISHIA KUMFUKUZA KAZI MHASIBU KWA MASLAHI YAKE BINAFSI
k) WAFANYAKAZI WANAOFANYA VIPINDI VYA USIKU KUTOPEWA USAFIRI WAKATI WA KWENDA NA KURUDI KITU AMBACHO KINAMLAZIMISHA MTANGAZAJI KULALA STUDIO KWA LAZIMA
l) GARI LA OFISI KUTOTUMIKA KWA MAHITAJI YA OFISI BALI KWA MASLAHI YA MKURUGENZI WA UFUNDI
m) MISHAHARA YA MWEZI JULY YA BAADHI YA WAFANYAKAZI KUZUILIWA KUANZIA TAREHE 1/8/2012 HADI LEO HII TAREHE 22/8/2012 KWA SABABU ZISIZO ZA MSINGI
NDUGU WANAHABARI, KWA MADAI HAYO HAPO JUU SISI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO HATUPO TAYARI KURUDI KAZINI MPAKA PALE MKURUGENZI WA UFUNDI NDUGU DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO ATAKAPOJIUZULU NAFASI YAKE NA MADAI YA WAFANYAKAZI YATAKAPOKUA YAMETATULIWA.
TUNAIPENDA SANA SUNRISE RADIO BILA KUWASAHAU WASIKILIZAJI WETU PIA TUNAWAPENDA SANA ILA TUMEONA NI VYEMA KUYAWEKA BAYANA HAYA YOTE ILI MTUELEWE NA PIA NI MAJIBU YA BAADHI YA MASWALI MLIYOKUWA MNATUULIZA WASIKILIZAJI WETU WAPENDWA.
NDUGU WANAHABARI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO WALIOGOMA KFANYA KAZI IDADI YAO NI KUMI NA WAWILI (12) WAKIWEMO
a) WATANGAZAJI 4
b) MARIPOTA 2
c) WATU WA MASOKO 3
d) WAZALISHAJI WA VIPINDI 2 NA
e) MHASIBU 1
WAFANYAKAZI HAO WAMEGOMA KUTOKANA NA MADAI YAO HAPO JUU PAMOJA NA MADAI MENGINE MENGI AMBAYO HAYAJAORODHESHWA
MAJINA YA WAFANYAKAZI WALIOGOMA NI HAYA YAFUATAYO
1. SEVERINUS MWIJAGE Jr – MTANGAZAJI
2. BEATRICE GERALD NANGAWE – MTANGAZAJI
3. EMMANUE MWAKALUKWA – MTANGAZAJI
4. JALACK ALLY – MTANGAZAJI
5. HAMIS ABTWAY (DJ HAAZU) – MTANGAZAJI, MZALISHA VIPINDI NA DJ
6. BERTHA ISMAIL – RIPOTA
7. ONESMO LOY – RIPOTA
8. JOSEPH AMANI – MZALISHAJI WA VIPINDI
9. ALLY CHARO – MENEJA WA MASOKO
10. RODGERS I. NELSON – MHASIBU
11. WITNESS RAYMOND – MASOKO
12. HAPPYNESS ALPHONCE – MASOKO

ASANTENI SANA KWA KUTUSIKILIZA

NAKALA
1. MCT
2. TCRA
3. OFISI YA MKUU WA MKOA
 
Kwa lugha nyingine biashara ya utumwa bado ipo. Lakini biashara hii inachochewa na uhaba wa ajira nchini. "Wawekezaji" wanatumia uhaba wa ajira kama ngao ya kuwanyanyasia watumishi wao.
Mtu atakayewasaidia hawa kufungua kesi mahakamani atafanya jambo la maana sana, kwa sababu kugoma tu haitoshi...
 
Si mchape mwendo, kwani kazi ni kutangaza tu. Au fungueni ya kwenu na mwiite sun shine. Au mmeforge vyeti? Kwani lazima mfanye hapo. Halafu ni mjinga mmeandika majina yenu, ina maana hakuna ajira kwingine tena, labda mfungue ya kewnu. A blessing in disguise!
 
Si mchape mwendo, kwani kazi ni kutangaza tu. Au fungueni ya kwenu na mwiite sun shine. Au mmeforge vyeti? Kwani lazima mfanye hapo. Halafu ni mjinga mmeandika majina yenu, ina maana hakuna ajira kwingine tena, labda mfungue ya kewnu. A blessing in disguise!

Wakiondoka kimya kimya wengiine pia watanasa kwenye mtego kama walionsa wao. Wakifunguka namna hii inawasaidia hata perspective job seekers kujua mwajiri huyo yukoje.
Hata hivyo kumbuka vijana wakikaa mtaani bila kazi wanakuwa desperate na waajiri kama hawa wanatumia vulnerability yao kwa kujinufaisha. Vijana hawa wanapaswa kulindwa na jamii kwa kukemea na kuchukulia hatua waajiri wa namna hii...
 
TUNALIPWA MISHAHARA MIDOGO ISIYOKIDHI MAHITAJI (MSHAHARA WA 100,000 NA WENGINE 170,000)
Ninyi ombeni kuongezewa mshahara kama mlivyosema, na ndio mdai huo mshahara mpya ambao utakua angalau na nafuu ndio mkatwe pension, ila kwa kipato hicho mlicho kiandika hapo juu kisha kikatwe dah, sasa mtabaki na sh. ngapi??
 
Mi ningewashauri hawa vijana warudi shuleni, au wafanye maandamano mazito ya kufa mtu. Hapo kitaelweka tu either wao au jamaaa.
 
Back
Top Bottom