Unyanyapaa wa baadhi ya watu wa magharibi kuhusu China haubadilishi ukweli wa mambo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,030
微信图片_20220413102047.png


b1a4c276637146268c9297c4b8e80b34.jpeg


Fadhili Mpunji

Hivi karibuni mwanamtandao mmoja wa youtube katika mji wa Shenzhen kusini mwa China, alionekana akizingumzia hali ya usalama katika miji mbalimbali ya China. Bwana Oli kutoka Uingereza alikuwa akielekeza hali halisi ya usalama wa mtu binafsi aliyojionea katika miji mbalimbali ya China, baada ya kuishi na kusafiri katika miji hiyo katika kipindi cha miaka miwili ya kuwepo kwake nchini China.

Katika hali ya kushangaza Bwana huyo amekosolewa vikali na baadhi ya watu kutoka nchi za magharibi, kwa kuonekana kama ni mtu aliyenunuliwa na kulipwa na kueneza propaganda za China, na kwamba anachosema hakiendani na kinachofahamika kwa wengi. Kwa watu wanaofahamu vizuri historia ya uhusiano kati ya China na nchi za magharibi, wanatambua kuwa msingi wa ukosoaji dhidi ya Bw. Oli unatokana na fikra za vita baridi zilizoganda vichwani kwa baadhi ya watu, ambao hadi leo wanaiangalia China kwa jicho hasi, na bado wanatilia shaka na kutoamini lolote zuri linalotajwa kuhusu China.

Lakini jambo la kufurahisha kuhusu video hiyo kwenye youtube, ni kwamba kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake, na wengi waliotoa maoni na hasa wachina wanaoishi kwenye nchi za magharibi na wageni wanaoishi na walioishi China, wanakubaliana na maoni ya Bw. Oli, na mimi mwandishi wa makala hii nikiwa na uzoefu wa kutembelea miji mingi ya China, pia nakubaliana na maoni ya Bw. Oli, kwamba uwe ni mwanaume au mwanamke, uwe ni kijana au mzee, hali ya usalama katika miji yote mikubwa ya China, ni bora kuliko hali ya miji mingi mikubwa ya nchi za magharibi. Wasichana na wanawake katika miji ya China wanaweza kutembelea kwa uhuru na kujisikia salama kuliko ilivyo katika miji mingi ya nchi za magharibi

Swali ambalo Bw. Oli aliuliza kwenye video yake kuwa ni kweli China kuna usalama kiasi hicho? Jibu la swali hilo ni kweli. Lakini swali la kwanini usalama katika miji ya China ni imara, jibu lake ni la kina zaidi.

Kwanza wachina wanatambua kuwa usalama ni moja kati ya haki muhimu kabisa ya kila binadamu, kwa hiyo hili ni jambo la kipaumbele katika jamii na mamlaka zinafanya kila linalowezekana kuhakikisha watu wanakuwa salama.

Pili ni kuwa usalama ni msingi wa haki nyingine muhimu kwa kila mtu, yaani haki ya kufanya kazi na kujiendeleza. Kama hakuna usalama, watu wanaweza kuishi kwa mazingira ya hofu na kushindwa kufanya kazi zao. Kwa hiyo kimsingi, usalama ni msingi wa karibu kila jambo katika jamii.

Tukiangalia picha kubwa, tunaweza kuona hali hii haipo kwenye suala la usalama peke yake, ipo kwenye mambo kadhaa yanayoihusu China. Nakumbuka mwanzoni wakati wataalam walipokuwa wakitaja ongezeko la uchumi wa China, kuna watu waliokuwa wanasita kukubali ukweli huo, wakiamini kuwa ni takwimu za kupikwa zisizo na ukweli wowote, hadi watalaam wa benki ya dunia na Shirika la fedha duniani walipokuja kuthibitisha takwimu hizo. Suala hili pia limeonekana kwenye mapambano dhidi ya janga la COVID-19, baadhi ya watu wakitilia shaka takwimu zinazotolewa na mamlaka.

Ni wazi kuwa kwenye ukweli uongo hujitenga, katika dunia ya sasa sio rahisi kudanganya watu kwa habari za uongo na takwimu za uongo, hasa ikizingatiwa kuwa watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaweza kuishi sehemu yoyote ile na kuwafahamisha wengine wanachokiona. Mitandao ya kijamii inaweza kuonyesha mawazo na hisia halisi za watu kuhusu mambo wanayoyaona. Hali ya usalama nchini China ni jambo ambalo ni rahisi kwa kila mtu anayetembelea China kuliona na kulifanyia tathmini, na kupitia jambo hilo unaweza kuona mtazamo wa wachina kuhusu umuhimu wa usalama katika maisha.
 
Wazungu pumbavu sana na wana wivu wa kishoga. Shoga anamuonea wivu mwanamke, yaani ndivyo wazungu walivyo, hawataki nchi nyingine ziwe na vitu vizuri isipokiwa zao tu
 
Back
Top Bottom