Unyang'anyi wawaponza, mwingine adaiwa kutapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyang'anyi wawaponza, mwingine adaiwa kutapeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 18, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na shitaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

  Washitakiwa hao ni Seif Jumanne (20), mkazi wa Mburahati Barafu na Khalfan Hemed (21) mkazi wa Mburahati Mianzini.

  Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Frednand Kiwonde, Mwendesha Mashitaka Boniface Edwin alidai kuwa washitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 25 mwaka huu, saa 3 usiku katika eneo la Kigogo.

  Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika muda na siku ambayo haikufahamika washitakiwa hao kwa pamoja walipanga njama ya kuiba mali za Issa Idd.

  Alidai kuwa katika shitaka la pili washitakiwa waliiba fedha taslimu Sh 330,000 na simu aina ya Nokia yenye thamani ya Sh 80,000, mali zote kwa ujumla zikiwa na thamani ya Sh 410,000. Zote ni mali za Idd.

  Kwa mujibu wa Edwin, kabla ya kuiba mali hiyo washitakiwa walitumia panga na kipande cha nondo kumtishia Idd ili awape mali hizo.

  Washitakiwa walikana mashitaka na wamerudishwa rumande kwa kuwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha haina dhamana.

  Wakati huo huo , mkazi Msaki, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Wilson Mbaruku (33) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kujipatia Sh milioni 11.3 kwa njia ya udanganyifu.

  Mwendesha Mashitaka Magina Magoma alidai mbele ya Hakimu Flora Mtarani kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Mei na Novemba mwaka huu.

  Alidai kuwa, mshitakiwa alijipatia fedha hizo kutoka kwa Ahmad Vans kwa madai ya kununua kiwanja kilichopo katika eneo la Madale na kuanza ujenzi wa nyumba badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini.

  Katika hatua nyingine, mkazi wa Sinza Msafiri Ramadhani (27) amefikishwa katika Mahakama hiyo kwa tuhuma za kujipatia Sh milioni 3.7 kwa njia ya udanganyifu.

  Mwendesha Mashitaka Mohamed Kilongo alidai mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kuwa Oktoba 3 mwaka huu katika eneo la Mwenge, mshitakiwa alijipatia fedha hizo kutoka kwa Mansoor Mohammed kwa madai kuwa atamuuzia nyumba.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na kurudishwa rumande hadi Desemba 27 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
   
Loading...