Unyang'anyi wa VODACOM utaisha lini?

Mu7

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
1,549
1,804
Hivi ni lini wateja tutapata mtetezi dhidi ya unyang'anyi huu tunaofanyiwa na mitandao ya simu hasa Vodacom? Tuliambiwa sheria inawataka Vodacom na mitandao ya simu kwa ujumla kutoa taarifa kwa umma kabla ya kubadilisha gharama za vifurushi vyao lakini kila wakati Vodacom hupandisha bei kwa njia ya kupunguza MBs bila kutoa taarifa kwa umma. Mara zote sijawahi kusikia mamlaka zikisema lolote kuhusu mwenendo huu. Ni kusema mamlaka hazijui hiki kinachoendelea au utaratibu huo wa kutoa taarifa kwanza umeshabadilishwa?

Sasa bundle la Tshs. 35,000 si GB 20 tena na la 50,000 si GB 28 tena.

Ni lini walaji tutapata mtetezi? Au mtetezi ameamua kuwa sehemu ya hiki kinachoendelea!

Inaboa, inaumiza na inakera sana!!!

Screenshot_20221027-133842_1.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom