Unyama wa Walimu, Serikali imulike ukatili wa walimu dhidi ya wanafunzi mashuleni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831

Walimu hawana utu wala huruma, sasa wameamua liwalo na liwe. Piga, uwa, garagaza.

Hawajali tena namna ya upigaji, mtoto wa kike apigwe mkononi, wa kiume matakoni. Walimu wanapiga ngumi wanafunzi utadhani wako kwenye tamasha la Karate.

Wanawazaba watoto vibao vya uso, ukatili mbalimbali wanaufanyia.

Sasa tunasikia habari za ulawiti, walimu wakiwafanyia watoto wa kiume, huku wale wa kike wakimiminiwa mimbegu iletayo mimba.

Hii kada ni kada adhimu kwa future ya taifa letu na vizazi vijavyo. Iheshimiwe na watu wote, walimu ndio wanatakìwa wawe wa kwanza kuiheshimu.

Na pia wakumbuke kwamba hata Yesu, alikuwa ni nabii. Hivyo elimu ndiye mkombozi pekee wa fikra za taifa letu na kizazi kijacho

 
Ila tukubaliane tu, kuna mitoto wabishi na wababe sana. Siafiki kitendo hicho, ila wazazi tuwajibike katika malezi ya watoto wetu.

Mfano, Mwanafunzi kujitutumua kutaka kupigana na mwalimu ni kiwango cha mwisho cha ukosefu wa nidhamu.
Ila mpka mtoto atake kupigana na mwalimu pande zote mbili zina shida.

Mimi kipindi tunasoma kulikua na watu wanapiga chuma hasa A level lakini mpaka namaliza shule sijawahi sikia mwalimu kukunjana na mwanafunzi kuanzia form 1 mpka 6
 
Siasa zinaharibu kabisa taaluma na maadili. Hawa wasainishaji lazima ni wanasiasa ambao hata hawajawahi kushika chaki
Uko sahihi 100% mbaya zaidi wamewasainisha walimu wanyonge wao wanaokesha na kuchangia moto hawajawagusa maprofesori ...soon watawasainisha mikataba madakitari na wauguzi asife mtu wagonjwa wote wapone
 
Daa kweli teknolojia inawasadia sana new age, sijui wkt wetu haya mambo yalivyokuwa, maana nakumbuka kisa kilichonitokea mimi mwenyewe kwa walimu hao wa mazoezi kutokana na kisa ambacho hakikuwepo ila kikatengenezwa ili kiwepo.

Haya maisha na matendo wayafanyayo watu wa aina hii huwa hayapiti bure huko mbeleni, ni vile huwezi kukutana naye hapo baadaye ila huwa wanapata pigo fulani.
 
Back
Top Bottom