Unyama wa polisi wakithiri, manyara wapiga na kujeruhi mtoto. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyama wa polisi wakithiri, manyara wapiga na kujeruhi mtoto.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngofilo, Aug 29, 2012.

 1. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Posted by Pamela Mollel on August 29, 2012 [​IMG]Mtoto aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu,Kadogoo Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian akiwa anahudumiwa na manesi hospitalini hapo juzi jijini Arusha


  • [h=2]WAMSHAMBULIA KWA MARUNGU NA KUMBANA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HADI KUTOKWA NA HAJA NDOGO.[/h]
  • [h=2]APOTEZA FAHAMU NA KULAZWA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI.[/h]
  [h=2]JESHI la Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada ya Askari wake wa tatu kutuhumiwa kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16 wa jamii ya kifugaji anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu.[/h] [h=2]Tukio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012 majira ya saa tano na nusu katika eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa jina moja tu la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu kuiba mbuzi wa jirani yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa eneo hilo la Orkesmet.[/h] [​IMG]Mmoja wa ndugu wa kijana huyo akiwa anawaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani nguo(kaptula) ya kijana aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu namna ilivyokuwa imechanika chanika baada kushushiwa kipigo

  [h=2]Mashuhuda wanadai kuwa polisi hao baada ya kumkamata mtoto huyo, walianza kumuadhibu bila huruma hali iliyopelekea mtoto huyo kulazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Selian iliyopo jijini Arusha.[/h] [h=2]Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa kutokana na kisa hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa walitaka kufungua mashtaka dhidi ya askari waliofanya unyama huo lakini walikataliwa.[/h] [​IMG]MAMA MZAZI WA KIJANA KADOGOO KALANGA AMBAYE ALIPIGWA NA MAASKARI WA KITUO CHA OLKESIMETI AKIWA ANAONYESHA SEHEMU AMBAZO MTOTO WAKE ANAMAUMIVU MAKALI BAADA YA KUPIGWA

  [h=2]Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ndani ya Hospitali ya Selian mama mzazi wa kijana huyo, Bi. Paulina Kalanga alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshumbulia kwa kumpiga bila kumpa nafasi ya kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na haja ndogo mfululizo na kisha kupoteza fahamu.[/h] [h=2]“Yaani walimkamata kijana wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke ….. wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako cha silaha ya moto ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza fahamu”alisema huku machozi yakimtiririka[/h] [​IMG]WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SELIANI WAKIWA WANAMUAMISHA HOSPITALI MTOTO HUYO BAADA YAKUKOSA KIFAA CHA KUMPIMIA KATIKA HOSPITALI HIYO NA KUMPELEKA HOSPITALI YA AGAKAN

  [h=2]Taarifa zinasema kuwa polisi hao baada ya kuona hali ya mtoto huyo imekuwa mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa ajili ya matibabu kabla ya wanandugu kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance) kumkimbiza katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.[/h] [h=2]Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo alikiri kupata taarifa zake huku akisema kwa kifupi kwamba tayari ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.[/h] [​IMG]
  [h=2]“Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo”alisema[/h] [h=2]Hatahivyo,aliongeza kwa kusema kwamba endapo kuna askari atabainika kuhusika na tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.[/h] [h=2]“Ikibainika askari amehusika basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa na hapa tayari uchuinguzi unaendelea”alisema[/h]
  [​IMG]

  source blog ya JAMII
   
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Sio endapo itabainika, kama wao hawakuchunguza na kubaini ila waliamua tu kupga, kwani wao ingojwd wabainike?!

  Na jina la mmoja lishatajwa? Wawekwe tu parade wananchi walokuwa tukioni waje kuwatambua.
   
 3. Ngofilo

  Ngofilo JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tatizo la nchi hii taharuma ilikufa zamani imebaki siasa tu
   
 4. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  The Day are numbered!
   
Loading...