Unyama na ukatili tunaofanyiwa na madalali

JAMANI KWELI KUNA MADALALI NI WAAJABU KWA TAMAA ZISIZONA MSINGI!
NDUGU ZANGU NIWAPE MKASA WA DALALI NILINUNUA NYUMBA MIAKA 8 ILIYOPITA KWA MAELEKEZO YA DALALI MMOJA HIVI KISA CHA KUNUNUA NYUMBA HIYO MUUZAJI ALIKUA ANASHIDA SASA LEO DALALI KAPATWA NA SHIDA YA PESA ETI WAMEKULA NJAMA NA MUUZAJI KUWA ANANIDAI BATI BANDARI 1IKIWA NI MAKUBALIANO BAADA YA KUUZIANA HIYO NYUMBA.KIMSINGI KUNA MADALALI MATAPELI
 
Ulitakiwa kutafuta nyumba wakati wa Mfungo wa ramadhani.!!

Ukitaka nyumba/chumba cha kupanga, tuma tu akaangalie nyumba kama tano hivi.Baadaye mtumie huyo mtu akupitishe kwenye zile nyumba.Basi kazi yako ni moja tu ya kulipa mwenye nyumba.
 
Tena kuwa makini, hukawii kuingiliwa na majambazi waliochongwa na Dalali! Nimewahi kuishuhudia
Ndugu zangu wana JF poleni na majukuumu,
Juzi nikiwa kwenye harakati zangu za kutafuta makazi katika mojawapo ya mikoa ya Kanda ya ziwa, nilibahatika kukutana na bwana mmoja kwa jina "Abdalla"ambaye ni dalali.

Nilimueleza aina ya nyumba niliyokuwa nahitaji na bila kusita tukaanza safari,

Baada ya kuzunguka takribani saa 4 hivi tulibahatika kupata nyumba moja iliyokuwa inahitaji mpangaji. Nilpata fursa ya kuongea na mwenye nyumba tukakubaliana ingawa nilimuomba anipe muda nikashauriane na mwenzangu (mke wangu) kwa kuwa yeye alipendelea "self".

Baada ya hapo nilichukua namba za mwenye nyumba, nikamlipa dalali elfu kumi (10,000) yake, ingawa alisisitiza kulipwa malipo sawia na kodi ya Mwezi mmoja kiasi cha Tshs laki moja na ishirini (120,000) jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wangu.

Kutokana na usumbufu uliokuwepo na kiasi kikubwa alichokuwa anadai dalali niliamua kupotezea kwa kumwambia nimeairisha na wala siwezi kuhamia kwenye nyumba hiyo.

Nilipofika nyumbani niliamua kusubiri kama siku 6 hivi ili kuepusha ugomvi na yule dalali. Siku ya saba nilitinga kwa mwenye nyumba tukamalizana kishikaji bila dalali kujua, nikashukuru Mungu.

Sasa juzi nikiwa nimetoka zangu job nimefika home nakutana na jamaa 3 wananisubiri, mmoja wao ni yule dalali eti ananidai (120,000) malipo yake ya udalali. Nimejitahidi kukanusha hanielewi anasema atawatumia "Sungusungu"endapo sitalipa ndani ya wiki hii.

Jamani huu ni ungwana? Nisaidieni
Asanteni.


Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Kama makubaliano yalikua hivyo kabla ya kuanza kutafuta hicho chumba kwanini usimpe chake? Ungemwambia toka mwanzo kuwa huna sidhani kama angekutafuta. Hapo mwenye nyumba pia lazima kakuchoma, lakini ni kwa kulinda biashara yake inamaana huyo dalali kamletea mteja sasa akimzunguka wewe ukihama atarudije kwa dalali?
 
Back
Top Bottom