Unyama na ukatili tunaofanyiwa na madalali

Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,000
2,000
Ndugu zangu wana JF poleni na majukuumu,
Juzi nikiwa kwenye harakati zangu za kutafuta makazi katika mojawapo ya mikoa ya Kanda ya ziwa, nilibahatika kukutana na bwana mmoja kwa jina "Abdalla"ambaye ni dalali.

Nilimueleza aina ya nyumba niliyokuwa nahitaji na bila kusita tukaanza safari,

Baada ya kuzunguka takribani saa 4 hivi tulibahatika kupata nyumba moja iliyokuwa inahitaji mpangaji. Nilpata fursa ya kuongea na mwenye nyumba tukakubaliana ingawa nilimuomba anipe muda nikashauriane na mwenzangu (mke wangu) kwa kuwa yeye alipendelea "self".

Baada ya hapo nilichukua namba za mwenye nyumba, nikamlipa dalali elfu kumi (10,000) yake, ingawa alisisitiza kulipwa malipo sawia na kodi ya Mwezi mmoja kiasi cha Tshs laki moja na ishirini (120,000) jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wangu.

Kutokana na usumbufu uliokuwepo na kiasi kikubwa alichokuwa anadai dalali niliamua kupotezea kwa kumwambia nimeairisha na wala siwezi kuhamia kwenye nyumba hiyo.

Nilipofika nyumbani niliamua kusubiri kama siku 6 hivi ili kuepusha ugomvi na yule dalali. Siku ya saba nilitinga kwa mwenye nyumba tukamalizana kishikaji bila dalali kujua, nikashukuru Mungu.

Sasa juzi nikiwa nimetoka zangu job nimefika home nakutana na jamaa 3 wananisubiri, mmoja wao ni yule dalali eti ananidai (120,000) malipo yake ya udalali. Nimejitahidi kukanusha hanielewi anasema atawatumia "Sungusungu"endapo sitalipa ndani ya wiki hii.

Jamani huu ni ungwana? Nisaidieni
Asanteni.


Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 

Maserati

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
11,614
2,000
Kiukweli madalali wanafanya kazi ngumu sikatai,lakini je, hii habari ya kulipana ela sawa na kodi ya nyumba huu utaratibu vepe!?? Mi siuelewagi aisee. Na usawa huu, we mpe hata 30 au 40 basi.
Akapambane na hali yake.
 

Imwase

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
501
1,000
Kiukweli madalali wanafanya kazi ngumu sikatai,lakini je, hii habari ya kulipana ela sawa na kodi ya nyumba huu utaratibu vepe!?? Mi siuelewagi aisee. Na usawa huu, we mpe hata 30 au 40 basi.
Akapambane na hali yake.
Hivi kwani kuna kazi ambayo ni rahisi ? Mimi nadhani kazi zote zinazomuingizia mtu kipato ni ngumu,hata kuuza ngada nayo ni ngumu

Najisikia fahari kuwa MTANZANIA
 

Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,000
2,000
Kiukweli madalali wanafanya kazi ngumu sikatai,lakini je, hii habari ya kulipana ela sawa na kodi ya nyumba huu utaratibu vepe!?? Mi siuelewagi aisee. Na usawa huu, we mpe hata 30 au 40 basi.
Akapambane na hali yake.
Nimejaribu kuwa mpole achukue hata 20,000 amegoma,,,!

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom