Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 672
Mjamzito ajifungulia ofisi ya Kata
2007-12-13 10:57:04
Na Anceth Nyahore, PST Shinyanga
Mjamzito aliyekuwa amewekwa chini ya ulinzi katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ilola, Wilaya ya Shinyanga kwa kutolipa mchango wa sekondari ya kata, amelazimika kujifungulia ndani ya ofisi hiyo.
Mjamzito huyo, Bi. Pili Kaya, mkazi wa kijiji cha Kasingili, wilayani humo, alikutwa na kadhia hiyo wakati akishikiliwa katika ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ilola, Bi. Noela Magesa kwa kushindwa kulipa mchango wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ilola.
Baada ya kukamatwa, alifikishwa katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ambako aliwekwa chini ya ulinzi.
Hata hivyo, akiwa chini ya ulinzi katika ofisi hiyo, Bi. Pili aliwaeleza viongozi wa Kata kuwa, anajisikia vibaya kutokana na hali yake ya ujauzito na kuomba aruhusiwe ili aende hospitali, lakini `walimtolea nje`.
Kufuatia hali hiyo, ndipo mwanamke huyo alipojikuta akijifungua katika ofisi hiyo tena mbele ya wanaume waliokuwepo.
Inasemekana kuwa, Bi. Pili alipatiwa huduma ya kwanza na baadaye kupelekwa hospitalini kwa huduma zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Kanali Edmund Mjengwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Kanali Mjengwa alisema ofisi yake hivi sasa kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, inafanya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
SOURCE: Nipashe