Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Tarehe 7 Mwezi August mwaka 2011, ITV walitangaza kuhusu unyama wa kutisha wanaofanyiwa wananchi wa Geita .Serikali imeshindwa kuchukua hatua madhubuti kumaliza tatizo la watu waliostahili kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kwenye makazi yao na Mgodi wa Geita Gold Mining.
Hadi sasa hali ni mbaya,wananchi wanaishi katika mazingira magumu vifo na udhalilishaji wa hali ya juu.Geita sasa haina tofauti na Niger Delta (iliyokuwa na utajiri mkubwa wa mafuta nchini Nigeria,huku wananchi wake wakiteseka kutokana na uwekezaji wa makampuni ya mafuta kutoka nje).
Ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa nchi yenye serikali iliyoridhia mkataba wa haki za binadamu wa mwaka 1948 na pia kwa serikali yenye uwakilishi katika idara na ngazi zote. Ingawa serikali mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu iliyoruhusu wananchi kubakia katika makzi yao hadi kesi ya msingi kuhusu fidia itakaposikilizwa,mkuu wa Wilaya ndugu Shelutete alisimamia zoezi la kuhakiksha wananchi wanaondoka maaeneo hayo pasipokujua wanaelekea wapi wengine wakiwa wajawazito,wagonjwa na wazee.Picha za mahema unazoona hapa chini ni msaada kutoka mashirika ya Dini.Wananchi hawa wako katika eneo hili tangu mwaka 2004 na hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
Hii ndiyo taswira halisi ya uwekezaji uliofanywa na serikali ya CCM kupitia sera zake za uwekezaji zilizoasisiwa na chini ya Uongozi wa Mh.Benjamini Mkapa (Wakati Rais wa Sasa Jakaya kikwete akiwa waziri wa mambo ya nje),wote kwa pamoja kwa kushirikiana na Wageni (kutoka Afrika Kusini) walisimamia zoezi hili lillilozaa wakimbizi ndani ya Ardhi ya Geita.
Jana ilikuwa tufanye mkutano wa hadhara uliohujumiwa katika mazingira ya kutatanisha,tulitembelea kwenye kambi ya wakimbizi hawa nikiwa na Kamanda Grayson Nyakarungu,Kamanda Otto-Mwenyekiti wa BAVICHA Geita,Diwani Machachari Vitimaalum kata ya Kagu Kamanda Marceline Simbasana na Viongozi wengine wa BAVICHA