unyama gani huu???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

unyama gani huu????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ms Judith, Jul 17, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  [h=2]Unyama gani huu?[/h]


  Na Moshi Lusonzo, 17th July 2011
  Baba ambaka na kumlawiti mtoto wake wa kumzaa

  Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukumbwa na matukio ya ukatili dhidi ya watoto ambapo hivi karibuni kumeibuka tukio la kutisha baada ya baba kumlawiti mtoto wake wa kike.
  Tukio hilo lemetokea eneo la Kimara Suka, ambapo mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamisi Elia Minga alidaiwa kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wake wa kumzaa (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 10 anayesoma darasa la tatu.
  Katika hali ya kusikitisha inadaiwa Mlinga alifanya unyama huo huku akimtishia kumchinja na kisu.
  Akisimulia mkasa huo, mtoto aliyefanyiwa unyama huo alisema baba yake alimbaka na kumlawiti mara mbili usiku huku akimtishia kumuua kwa kisu endapo atapiga kelele.
  Alisema siku zote mbili kwake ilikuwa siku za mateso kwani baba yake huyo ambaye anafanya kazi ya kuchuga ng’ombe alimuingilia kwa nguvu na kisha alimkanda kwa maji ya moto ili kumpunguzia maumivu.
  Alisema, matukio hayo yote alifanyiwa wakati mama yake aliposafiri kwenda kwao Dodoma kwa ajili ya kushiriki mazishi ya ndugu yao.
  “Baba siku ya kwanza alikuja kitandani kwangu na kuniambia nivue nguo yangu, nilikataa lakini alinitishia kuniua kwa kisu,” alisema binti huyo.
  Alisema baada ya kufanikiwa kumvua nguo zake za ndani alimuingilia huku akimziba mdomo ili asitioe sauti ya kulia.
  Kutokana na kuwa na maumivu makali, baba huyo alikuwa na kawaida ya kumkanda kwa maji ya moto kwa ajili ya kupunguza maimivu.
  “Baba wakati anapomaliza kuniingilia ananikanda kwa maji ya moto halafu anasema nisimwambie mtu kwa usalama wangu,” aliongeza kusema.
  Alisema kutokana na maumivu makali alishindwa kukaa vizuri hivyo siku ya tatu alishindwa kwenda kulala kwenye nyumba yao akihofia baba yake kumfanyia vitendo hivyo.
  SIRI YAFICHUKA.
  MAMA mdogo wa mtoto huyo, Rebecca Msigwa alisema kuvuja kwa habari hiyo kulitokana na hatua ya mtoto huyo kukataa kwenda kulala kwenye nyumba ya baba yake.
  Alisema, akiwa na dada yake nyakati ya usiku, baba yake alimuita kwa ajili ya kwenda kulala lakini mtoto huyo alikataa kwenda na kuanza kulia.
  Kutokana na hali hiyo, dada yake alimbana kwa nini hataki kwenda kulala, ndipo alipomwambia hataki kwenda kulala kwa sababu baba yake anambaka usiku.
  “Baada ya kuambiwa maneno hayo, dada yake alikuja kwangu na kuniambia jambo hilo hivyo haraka nikaamua kwenda kwa mjumbe na kumuarifu dada yangu nyumbani,” alisema Rebecca.
  Alisema siku ya pili yake waliamua kumpeleka kwenye kituo cha Afya cha Kimara, ambapo madaktari walithibitisha kuwa mtoto huyo aliingiliwa kinyume na maumbile.
  MTOTO ALITOKANA NA MAMA YAKE KUBAKWA.
  Katika hali inayoonekana ya kushangaza wengi ni kuwa mtoto aliyefanyiwa unyama huo alizaliwa baada ya mtuhumiwa huyo kumbaka mtoto wa dada wa mkewe ambaye alikuwa akiishi naye.
  Kwa mujibu wa maelezo ya familia ya mtoto huyo imefahamika, mama yake alikuwa akiishi hapo ndipo Mlingwa alianza kufanya naye mapenzi na hatimaye kuzaliwa kwa binti huyo.
  Akieleza kwa uchungu bibi wa mtoto huyo, Joyce Msigwa alisema anashangazwa na kitendo cha mwanaume huyo kufanya unyama huo hata kwa kiumbe chake.
  “Unajua huyu mtoto amezaliwa na binti yangu mwenyewe, mama yake mdogo ambaye ni mke wa mtuhumiwa alikuja kumchukua ili akaishi naye lakini mwishowe alijazwa mimba na baba yake huyu mdogo,” alisema.
  Alisema kutokana na tukio hilo, inaonekana wazi ameshazoea tabia hiyo kitu ambacho ukoo wao umeanza kuchanganyikiwa.
  “Hivi sasa hatujui la kufanya kwani huko nyuma tulidhani amepitiwa na tuliamua kumsamehe lakini hili la kumuingilia binti yake mwenyewe halivumiliki,” alisema.
  Pamoja na hayo, Mke wa mtuhumiwa Juliana Msigwa (33) anakiri mumewe kufanya tukio hilo la kinyama na kueleza kinachomsikitisha ni kwamba Jeshi la Polisi halichukui hatua yoyote licha ya kwenda kuripoti.
  Alisema, tukio la kubakwa kwa mtoto huyo ambaye alimlea mwenyewe akiwa na umri wa miaka miwili limemsononesha kiasi ambacho sasa anashindwa kuishi kwa furaha.
  “Huyu bwana sijui ana kitu gani mpaka anakuwa hivi, kwanza alimbaka mtoto wa dada yangu na kisha kupatikana kwa mtoto huyu, kwa nini jamani ananifanyia hivi,” Juliana alisema huku akiangua kilio.
  POLISI YASHUTUMIWA KUMLINDA MTUHUMIWA.
  Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamewashutumu Askari Polisi wa Kituo cha Kimara kutokana na kutochukua hatua zozote licha ya kuripotiwa kwa tukio hilo.
  Akizungumza na gazeti hili Mjumbe wa eneo hilo Kesi Tunda alisema mara alipopatiwa taarifa juu ya tukio hilo, walitoa taarifa polisi ili wafanye juhudi za kumkamata mtuhumiwa lakini toka siku hiyo hakuna kilichofanyika.
  Alisema mara zote wanapokwenda kituoni hapo wanaambiwa warudi nyumbani na wao watakwenda kumkamata, kitu ambacho hakijafanyika mpaka leo.
  “Tunapatwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hawa polisi kwa nini hawaji kumkamata huyu bwana, ukweli ni kwamba hatumtaki kwenye mtaa wetu,” alisema Tunda.
  Hata hivyo, Tunda alieleza kitu kibaya ni kitendo cha Mlingwa kutembea na kisu kila wakati akimtafuta shemeji yake Rebecca ili amuue kwa madai ndiye chanzo cha vitendo vyake kuwekwa hadharani.
  “Sasa kama mtu kaamua kutembea na kisu kwa ajili ya kumuua mtu huku tayari amefanya vitendo vya kinyama anaachiwa hivi hivi sisi raia tutaliangalia vipi jeshi la Polisi,” alihoji.
  Hata hivyo Tuhuma hizo zinakanushwa na Polisi ambapo imeeleza juhudi za kumtafuta mtuhumiwa huyo inafanyika lakini bado hawajaweza kumkamata.
  Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kimara, Mratibu Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa alisema ni kweli wanazo taarifa hizo na wapo katika juhudi kubwa za kumtia mbaroni mtu huyo.
  “Unaju watu wanasema tu, sisi tunafanya kazi ya kumtafuta lakini kutokana na kujificha hatujaweza kumkamata, tunaomba kama wanajua mahali alipo watuambie na sisi tutakwenda kumkamata,’ alisema OSS Mambosasa.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu wamekuwa na tabia za kinyama sijui tunaelekea wapi!
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Imeniuzi sana.......kwa nini polisi wanadelay namna hiyo kumkamata......hii inasababisha wananchi kufikia hatua ya kuchukua sheria mkononi
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Hukumu yake huyo ni "bangubangu till death". Ukitaka kuijuwa hiyo hukumu pita kule kwenye jukwaa la udaku, ntaweka kisa chake.
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh! hata sijui tumuamini nani sasa kwenye dunia hii Baba ndio hali kama hiyo,Mungu atustiri na balaa kama hilo.
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bi Faiza Chechei! hujambo?
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Cheichei, AlhamduliLlahi sijambo. Na wewe hali yako Falcon?

  Naomba avatar yako iwe ya real Arabian Falcon, what a beautiful bird.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is disgusting, hivi hako kadudu kanasimamaje hivyo??

  aisee
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Huyo baba ni wakuuliwa tu tena unakata kiungo kimoja kimoja apate maumivu yake
   
 10. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hii habari nimeisikia leo radio maria iliniuma sana, huyu mtu angekuwa mwanza wananchi wangeshamuhukumu, polisi watz wanalaana sasa hapa wananchi wakichoma vituo vya polisi mtadai upinzani umewatuma, ni bora kusikia mtoto amekufa kwa kutumbukia chooni kuliko kusikia hii habari
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huu ni unyama kwa kweli, anafaa kunyongwa kabisa huyo baba...
   
Loading...