Unveiling the political horizon; m4c pushing harder in southern zone, pichazzzz!!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa (kulia), akizungumza baada ya kufungua moja ya matawi mjini Newala ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi wa chama hicho. Katikati ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiwa amembeba mtoto Muaza Mohamed na kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Zanzibar, Ali Issa Mohamed.


Akina mama wa kijiji cha Mbuyuni, katika jimbo la Lulindi mkoani Mtwara, wakiimba nyimbo za kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, mara baada ya mkutano wake wa hadhara katika kijiji hicho
Akina mama wa kijiji cha Mbuyuni katika jimbo la Lulindi mkoani Mtwara, wakiitikia kibwagizo cha Peoples Power kinachotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wa mkutano wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho wa kampeni ya Vua Gamba Vaa Gwanda, uliofanyika mjini Tandahima mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya Vua Gamba Vaa Gwanda, uliofanyika huko Chiungutwa, Lulindi mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akipandisha bendera ya chama hicho, wakati alipofungua Tawi jipya katika Mtaa wa Mkombozi mjini Newala juzi. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Zanzibar, Ali Issa Mohamed.

Kama imekuuma sana na Magamba yako 'GO & EAT A COKE'

 
haaaaa haaaa...
hamjaniconvice bado..... wakoloni mmekuja kueneza nini?? wenyeji wanawashangaaa mmetokea wapi?? nashuluru TINDU LISSU nimekuona kijijini kwangu pale MILANGO MINNE, MTWARA VIJIJINI......
 
Wanawake wenzangu msirudi nyuma sukumeni gurudumu la ukombozi nawaona mulivyohamasika hadi Raha ahsante kwa picha mleta uzi
 
haaaaa haaaa...
hamjaniconvice bado..... wakoloni mmekuja kueneza nini?? wenyeji wanawashangaaa mmetokea wapi?? nashuluru TINDU LISSU nimekuona kijijini kwangu pale MILANGO MINNE, MTWARA VIJIJINI......

safiii
 
Kipindi kile cha staili ya jmaandamano ccm walilalamika na baada ya kushindwa wakaiga na wao wakafanya ya kwao kule mbeya! Sasa hivi cdm wanamkimbiza mwizi kimya kimya mpaka atakapozidiwa atapiga kelele yeye mwenyewe! Kwa staili hii CDM wako juu!
 
haaaaa haaaa...
hamjaniconvice bado..... wakoloni mmekuja kueneza nini?? wenyeji wanawashangaaa mmetokea wapi?? nashuluru TINDU LISSU nimekuona kijijini kwangu pale MILANGO MINNE, MTWARA VIJIJINI......


Pasco hata JK anakuzidi akili ,yeye kesha waonyesha M4C ofisi yao pale magogoni kama huamini kaongee na Laurence Masha atakwambia hata yeye hakuamini mpaka siku alipomuona Wenje bungeni? gamba lako ni zaidi ya la kobe na utakufa nalo
 
body guards je?
133957683_313de52d3a_o.jpg
 
Back
Top Bottom