Ununuzi wa Ndege nyingi ni janga kwa Wananchi

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Wakuuu Mimi Sitaki upishi usio waushahid, ninataka kufafanua na kutetea hoja Yangu Kama ifuatavyo:

1. Ununuzi wa Ndege ni mojawapo Ya miradi mikubwa Sana tulioambiwa kuwa inasababisa mishahara Ya watumishi isipande na vijana wasiajiriwe tukiambiwa kuwa baada Ya muda miradi hiyo itawezesha faida kubwa na kupelekea watu kunufaika nayo.

Kwa mujibu wa mkaguzi wa hesabu za serikali ni kuwa Ndege hizi zinaendeshwa Kwa hasara, maaana yake nikwamba baada Ya miaka kumi Ndege hizo moja itakuwa imegarimu kiasi cha fedha sawa na garama za kununua Ndege nne.

Wananchi wamekamuliwa Sana kodi toka kila pande Ya nchi Toka Vijijini had mjini, wamejikuta wakiwa mafukara wakubwa kutokana na kodi kuwa nyiiiiingi na matokeo yake hiyo hela inaenda kununua kitu kinachokuja kuendeshwa Kwa hasara, unawaacha wananchi wakiwa hawana nadawa kwenye hospital, zahanati na shule zikiwa hazina walimu, watu hawana Huduma muhimu Kama Maji, vijana hawaajiriwi na mishahara haipandishi.

Katika akili ya kawaida huwezi Chukua hela ndani ukanunua Gari ukawaacha watoto hawana ada za shule kisa unarahisisha usafiri, pia tunafaham fika kuwa hizi Ndege asilimia tisini wanaonufaika nazo ni matajiri na vigogo wa Juu, mwananchi wa kawaida karibu asilimia tisini hata Kuiona hiyo Ndege watazeeka pasipo kuiona na Kwa kuwa inaendeshwa Kwa hasara hela Ya huyo mwananchi itakuwa imepotea.

Lakini Jambo lingne Ndege hizi zilinunuliwa pasipo kufuata taratibu za kisheria, Hakuna mahali palipoidhinishwa na wananchi kupitia waawakilishi wao kununua hizi Ndege, Jambo lingne Ndege hizi zimekuwa zikiharibika Mara Kwa Mara, najua kuwa ukinunua Gari Mpya inapaswa kuchukua muda mrefu Sana kuja kuharibika.

Ninachokiona nikuwa ikitokea Magufuli anashinda Uchaguzi huu, Mwaka 2025 hizi Ndege Nina Uhakika kuwa hazitakuwa agenda ya CCM tena ninamaanisha kuwa zitakuwa zimekufa na tumeingia hasara watakuja na karata nyingne, hiii nikutokana na sasa hivi magufuli kuacha agenda ya viwanda gafla kitu ambacho ilikuwa ni Wimbo wa taifa Kwa Magufuli.

Ilikuwa kumtenganisha Magufuli na Wimbo wa viwanda nikama kumtenganisha samaki kambale na Maji, watanzania ni wepesi wa kusahau mambo, hivi viwanda vya magufuli mnakumbuka huo Wimbo? Viko wapi? Hizo ajira za viwanda ziko wapi?

Wakuu, Kama wewe sio mfia chama shutuka ungana na lisu kuhoji hizi Ndege, nasema kuwa Kama sio mfia chama nikimaanisha kuwa wapo watu wachache ambao wanakula CCM, wanalala CCM, wanaamka CCM, Hawa hata nchi ikafilisika Kabisa wao watakufa na chama maana pasipo CCM watakufa Siku ya kesho yake.
 
Ila rami zinakusaidiaga??
Flyover inakusaidiaga??

Kuna vitu hua vinafanywa kwa maslahi ya nchi...!!sio ya wananchi...!!
Kama unafanya vitu kwako maslahi Ya nchi na sio wananchi Halafu ukaenda kuomba kura Kwa hao wananchi basi wewe utakuwa ni zaid ya taira, Kwan hiyo Mimi nikupe kura Yangu ili uende kufanya vitu Kwa maslahi ya nchi? Nenda ukapigiwe kura na nchi
 
Ndo hapo anapokosea mkuu...kuna muda uzalendo ukizidi katk nchi yenye watanzania ni ishu

Ila nnavoamin kufikia maendeleo lazima tupitie msoto...!!japo n kweli hali iko vbaya..
Kama unafanya vitu kwako maslahi Ya nchi na sio wananchi Halafu ukaenda kuomba kura Kwa hao wananchi basi wewe utakuwa ni zaid ya taira, Kwan hiyo Mimi nikupe kura Yangu ili uende kufanya vitu Kwa maslahi ya nchi? Nenda ukapigiwe kura na nchi
 
Chukua hatua ikianza na we we!!!! Mtu anaitwa jiwe afu unaleta ushaur kwa jiwe
Ununuzi wa ndege nyingi kwa cash,wakati hazizalishi ni majanga kwa uchumi.
Wangeacha kwanza kuongeza zingine,hadi zilizopo ziweze kuingiza faida.
 
Taifa linalojielewa lazima liwe na shirika lake linalofanya kazi,Watu wengine tumieni akili walau kidogo tu,katika miaka mitano na budget zake zote ndege zimetumia %ngap ya budget iyo?Mlitegemea Tuendelee kutumia ndege Za mataifa mengine ili dawa zipatikane kila wakat unajua hata dawa zisipotumika zianaharibika na ni hasara pia, BTW kwann unasema dawa hazipatikani unatakwimu hazipatikan kwa %ngap na kwa muda gani?

Sio kwa ubaya watz hatuna jema basi unapojenga hoja yako hakikisha inamashiko
 
Taifa linalojielewa lazima liwe na shirika lake linalofanya kazi,Watu wengine tumieni akili walau kidogo tu,katika miaka mitano na budget zake zote ndege zimetumia %ngap ya budget iyo?Mlitegemea Tuendelee kutumia ndege Za mataifa mengine ili dawa zipatikane kila wakat unajua hata dawa zisipotumika zianaharibika na ni hasara pia, BTW kwann unasema dawa hazipatikani unatakwimu hazipatikan kwa %ngap na kwa muda gani?

Sio kwa ubaya watz hatuna jema basi unapojenga hoja yako hakikisha inamashiko
Nyie ndio wazee wa ndio, unanjaa ndiooooo, umeshiba ndiooooo, mwenzio tumeeleza na kufafanua kiundani zaid na kiutaalam zaid wewe unakuja na kauli Ya kupinga hoja unauliza asilimia, ulitakiwa uje na asilimia hizo Kwa ajiri Ya kujenga hoja na kutetea sio tena uje kuuliza na kupinga jenga hoja yako, angalia kule Juu ufafanuz na hoja ilivyojengwa
 
Nanga lazima ipae, kwa nature ya tume ya uchaguzi, uchaguzi umeisha kitambo. Hii miaka5 ijayo itafanana na miaka50.
 
Mpaka sasa sisi tulioko huku Likuyufusi hizo ndege hazijatusaidia lolote!
Sisi wakulima wa parachichi na mbogamboga tumeshaanza kufaidika nazo kwa kusafirisha na kuuza nje ya nchi. Tunaiomba serikali iharakishe ununuzi wa ndege ya mizigo ili mazao yetu ya mbogamboga na parachichi yawe yanasafirishwa kwa wingi moja kwa moja kwenda Ulaya.
 
Ukisikia JPM anasema kwani kiwanja ni Chato tu mbona hamuongelei vingine; ujue chumvi iliyosuguliwa kwenye kidonda inauma!
 
Back
Top Bottom