Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Nilikuwa nje kidogo ya kijiji kwa hiyo kwa muda sikuwa na taarifa za nini kinaendelea. Baada ya majaribio ya karibu siku tatu hatimaye kura zimetosha kwa CCM. Regia aliweka wakala kwenye kila kituo na matokeo yote waliyonayo kutoka vituoni (kwa mawakala) yalionesha Regia anaongoza kwa kura nilizodokeza awali. Hata hivyo baada ya kuhesabu na kuhesabu tena kiasi cha kura kikazidi in favor ya CCM.
Hivyo, Mkoa wa Morogoro wote umeenda CCM. Kwa hivi sasa matokeo rasmi ndiyo hayo ya CCM kushiinda Kilombero. Kwa vile tunajua kuwa baada ya kukata rufaa mahakama zimepewa jukumu la kushughulikia kesi za uchaguzi mapema (mabadiliko ya karibuni ya sheria) tungojee ushahidi katika mahakama wa kuchakachuliwa kura au la.