Unless the Lord build the house, the builders labor in vain

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Historia ni mwalimu mzuri sana, hutufundisha mambo mengi sana ambayo tunapaswa kujifunza kutokana nayo, Kwahakika hatupaswi kupuuza historia. Kama ilivyowahi kunenwa kama hujui ulikotoka, kamwe hautofahamu unapokwenda.

Tunapaswa kujifunza kutokana na historia lakini agharabu mara chache mno hujifunza. Tunafahamu kuwa baadhi ya matendo yetu hutupelekea kuwa katika mwisho mbaya, lakini tunayarudia yale yale kama kizazi kimoja kiliyowahi kuyafanya na tunadhani kwamba mwisho wetu utakuwa tofauti na wao.

Binadamu anapaswa kuangalia kwa ukaribu sana matendo yake, yumkini dira yake hutegemea yale anayotenda. Kuna matokeo katika kila matendo yetu. Ni ukweli usiopingika kwamba tukibadili jinsi tunavyofikiri na kutenda maisha yetu yatabadilika. Ni kweli pia ya kwamba tutavuna kile tunachopanda na hakuna bahati mbaya katika hili. ''We are products of our thoughts and actions'' Nasema tena tunatakiwa kuwa makini jinsi tunavyofikiri na kutenda. Tusije kusema tumerogwa baadae''

Kunapotokea vita au machafuko katika nchi hayatokei kwa bahati mbaya bali ni mtiririko wa mawazo na matendo ambayo huleta matokeo mabaya. Mawazo mabaya kila wakati hutoa mazao mabaya. Chuki , ulafi , uongo, wizi , tamaa, choyo, kujifikiria mwenyewe bila kuangalia wengine ambao ni ubinafsi haviwezi kuleta matokeo chanya katika nchi wala utulivu na utaratibu.

Kama mawazo yetu mabaya na ya uovu tunawezaje kujenga taifa la watu wema? Tuna taifa ambalo leo watu wamejawa na tamaa ya mali kuliko utaifa, wako tayari kuvuruga nchi kwa tamaa ya mali na madaraka. Na wengine wanataka kujikweza na kujiweka juu ya wengine. Tunataifa ambalo umalaya unaabudiwa na watu hao sasa wanakuwa maarufu na wenye ushawishi katika tabia za vijana tutawezaje kuendelea? Na tunaamini kabisa tunaweza kuendelea bila mkono wa Mungu kuwepo na sisi? Katika mazingira haya tunawezaje kujenga umoja wa nchi na kulifanya taifa hili kuwa moja? Nani awezaye kunipinga kwamba chimbuko la mambo yote yanayotokea sasa yanatokana na tabia zetu?

Kwa hakika tusitegemee kupata viongozi wazuri kama sisi wenyewe sio wema. Kwasababu viongozi wanatoka miongoni mwetu. Watu wema kamwe hawawezi kuchagua viongozi waovu wawatawale, kama tunawachagua na tunajua kabisa ni waovu na wasiopenda haki na usawa tumlaumu nani? Sio kwamba tabia zao ni taswira ya tabia zilizomo katika jamii ambazo tumezilea wenyewe na kuzikuza ndani ya familia na katika jamii? Jukumu letu ni lipi katika makuzi na malezi ili kutengeneza raia wema na waadilifu? Wengi wetu tumefeli katika wajibu huu na tunajua kabisa baadae ya taifa hili inategemea jinsi gani tumetayarisha kizazi kimoja kwenda kingine kuchukua majukumu ya kitaifa. Kama hakuna maadili tusitegemea amani na maendeleo katika taifa hili. Inawezekanaje taifa la watu wasio na maadili likawa moja na lenye dira?

Hatua moja na ya muhimu ili taifa hili liendeleee ni kubadili tabia za watu na jinsi wanavyofikiri. Ni lazima tutengeneze raia ambao wanatenda matendo mema. Na hili sio kwamba haliwezekani linawezekana. Tunauwezo wa kujenga raia waaminifu na wawajibikaji. Mambo yanaweza kubadilika. Naamini kama tukibadilika kifikra tunaweza kuwa kitu chochote kile tunachotaka. Lakini kama watu sio wamoja na wenye mawazo ya kibinafsi hakuna cha maana watakachofanikiwa na hata kidogo walichokifanya hakitathaminiwa.

Na kuna watu wanafikiri wana haki ya kutawala wengine na kuwa juu yao. Binadamu wote ni sawa. Hawa walioko kwenye utawala lazima watumie mamlaka yao kwa busara sio katika kukandamiza watu na kutumia madaraka yao kwa uonevu. Kila binadamu ni huru na anastahili uhuru. Pale uhuru wa mtu unapoingiliwa na hofu kumuingia hapo serikali imekiuka misingi ya uwepo wake ambao ni kusimamia haki na usawa na sio kuwafanya raia kuwa watumwa. Binadamu hapaswi kuwa na hofu ya kutoa maoni yake haswa kuhusu jinsi anavyoona anavyotawaliwa. Kutumia madaraka kuua au kufunga watu wenye mawazo tofauti na wewe si sahihi.

Maisha ya binadamu yana thamani kubwa mno. Na nguvu pekee haiwezi kukufanya kutawala watu. Hakuna mtu anayependa kukosa uhuru wake na kuwa mtumwa. Ukiwanyima watu uhuru watatafuta uhuru huo katika njia ambazo si sahihi. Ninachotaka kusema watu lazima wawajibike na kile wanachosema na kutenda kwa kuangalia taifa kwanza kabla ya jambo jingine lolote. Viongozi na wanasiasa wa taifa hili lazima watambue hilo na kubadilika. Nchi hii ni muhimu kuliko maslahi yetu binafsi. Mamlaka bila busara ni hatari mno. Kama viongozi wetu wanasema na kutenda bila hekima na busara baadae yetu itakuwa na shida na hata amani yetu.

Tunaongea kila siku kulinda amani yetu amani yetu tunailindaje? Kwa nguvu za polisi na jeshi? No ! Amani hailindwi kwa nguvu za jeshi na polisi. Tukiamini hivyo tutakuwa tunajidanganya. Na hilo jeshi la polisi litakuwa linalinda upepo. Amani ni kitu ambacho kiko ndani ya mtu na ni zao la matendo ya uadilifu na haki. Kama hakuna uadilifu na haki katika jamii sahau kuhusu amani hata kama una majeshi kiasi gani huwezi kuilinda kwasababu ni kitu kinachotoka ndani ya mtu kwanza sio cha nje. Utawatishia watu kwa bunduki huku ndani ya mioyo yao wanaendelea kunung'unika na kuhuzunika kwa kutokuwepo kwa usawa na haki katika jamii. Amani ya namna hii ya kulindwa kwa bunduki na ya kutia watu hofu haidumu ni ya kipindi kifupi. Kiongozi yeyote mwenye akili hawezi kufikiri amani inalindwa kwa bunduki bila kuwepo na haki na usawa katika jamii na hata uadilifu. haya mambo yanaanza ndani kwanza kwenye nafsi ya mtu. kama nafsi ya mtu haina amani amani ya nje ni kiini macho. Kwahiyo tunapoongelea amani sisi kama viongozi ni lazima matendo yetu ya reflect hiyo amani tunayotaka. Amani ni product of our deeds. Tunapodai tutailinda amani na matendo yetu hayafanani na hiyo amani ni unafiki wa hali ya juu. Na iko siku hiyo nguvu unayoitumia dhidi ya watu wengine inaweza kukurudia. Kama biblia inavyotuambia ukweli huu muhimu;

''Unless the Lord build the house, the builders labor in vain. Unless the Lord watches over the city, The guard stand watch in vain'' psalm 121:1. All things starts from within.

Ni ukweli usiopingika kama utawala hautendi haki , amani ni kiini macho. Kama utawala hautendi yale yaliyo sahihi, hata usalama wao uko hatarini. Mambo yanapoanza kubadilika yanaanza pole pole kwa mabadiliko ya fikra na mioyo ya watu. Hofu huwa haidumu mara nyingi hugeuka na kuwa ushupavu kwa wale watu ambao huonewa. Ili utawala wowote udumu ni lazima utende haki. Kama nilivyosema mwanzo tutavuna tulichopanda iwe kwetu sisi wananchi au kwa watawala wetu. Nawaambia watawala wa dunia wasipandishe mabega yao juu kwasababu wana majeshi wakafikiri wanaweza kutenda wanachotaka watende yaliyo sahihi.


Any power must be directed by wisdom otherwise it will be harmful to a man with power and to the country. As the bible says in the book of proverbs Desire without knowledge is not good.
 
Back
Top Bottom