Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Wakati mjadala juu ya ubora wa elimu hapa nchini ukishika kasi kila kukicha, swala la sheria/kanuni za mitihani katika vyuo vikuu vyetu hapa nchini linaonekana kusahaulika kabisa au kutopewa uzito wakati hizi regulations ndio msingi wa kupatikana kwa kitu kinachoitwa Grades Point Average(GPA).
Yaani iko hivi,wakati GPA za wahitimu wa vyuo katika kujiendeleza kielimu na katika soko la ajira zikiangaliwa bila kujali mhitimu ametoka chuo gani,msingi wa upatikanaji wa GPA hizo ni tofauti kabisa baina ya vyuo kutokana na kila chuo kuwa na sheria/kanuni zake za mitihani ambazo ndio uamua ufaulu wa mwanafunzi husika.
Kwa mfano,kuna vyuo ambavyo coursework ni asilimia 50 na UE (University Examanination) ni asilimia 50 wakati vyuo vingine coursework ni asilimia 40 wakati UE ni asilimia 60.
Kuna vyuo vingine mwanafunzi akifeli kozi 3 tu katika semister moja haruhusiwi kuendelea na semister inayofuata bali hatukiwa kurudia semister hiyo hata kama ana GPA ya above 1.8(iwe 2.5,3.5 n.k haisaidii) au kurudi kabisa nyumbani kama GPA iko chini sana.Yaani matokeo ya semister moja tu ya mwaka wa masomo inaweza kumfanya mwanafunzi arudie semister au hata arudi nyumba (adi-sco)
Wakati hali ikiwa hivyo,vyuo vikuu vingine hali ni tofauti kabisa ambapo mwanafunzi hupimwa kwa average GPA ya semister zote 2 za mwaka wa masomo na sio GPA ya semister moja au idadi ya kozi mtu alizofeli katika semister moja.Hii maana yake ni kwamba,mwanafunzi akifeli hata kozi 5 katika semister moja, anaruhusiwa kuendelea na semister ya pili ya mwaka wa masomi inayofuata na average ya GPA ya semister ya pili na ile ya kwanza ndio inaamua mwanafunzi aendelee na mwaka wa masomo unaofuata,arudie mwaka au arudi nyumbani(discontinuation).
Kuna vyuo vingine vina kitu kinachoitwa Departmental GPA ambayo hutumika kupima ufaulu wa mwanafunzi wakati vyuo vingine havina utaratibu huu wa Departmental GPA.
Vile vile kuna masomo kama Communication skills na Development studies ambayo katika vyuo vingine huchukuliwa kama masomo ya ziada na vyuo vingine hupewa uzito sawa na masomo mengine kiasi kwamba ukifeli masomo hayo yanaweza ku-coast.
Mbali na hayo,hata swala la grades za ufaulu ambazo ni A,B, B+,C,D na E kwa masomo baina ya vyuo sidhani kama ziko uniform.Unaweza kuta chuo X grade ya A inaanzia 70 wakati chuo Y inaanzia 75.
Hata units kwa masomo sijui kama ziko uniform. Mfano units zinazotolewa kwa Research katika chuo A unaweza kuta ni tofauti kabisa na units zinazotolewa kwa Research katika chuo B wakati mwisho wa siku units hizi ndio hu-determine GPA ya mhitimu wa chuo fulani.
Vile vile hata utaratibu wa ku-calculate GPA nao sijui kama kweli ni uniform baina ya vyuo au kila chuo kina utaratibu wake.
Cha ajabu na kushangaza,licha ya mazingira haya tofauti ambayo hutumika kupima uwezo na ufaulu wa mwanafunzi katika vyuo vikuu vyetu,GPA hizi ambazo hupatikana kwa vigezo visivyofanana huchukuliwa kwa usawa bila kujali mhitimu kasoma chuo gani iwe ni katika soko la ajira,katika kujiendeleza kielimu, n.k.
Tukumbuke examination regulations za kila chuo na grades za ufaulu kwa kila somo katika kila chuo, ndio hu-determine GPA ya mhitimu kwahiyo kama kanuni/sheria hizi hazifanani baina ya vyuo kamwe GPA hizi haziwezi kuwa sawa hata kidogo na hazistahili kabisa kuwekwa katika mzani mmoja.
Naamini yako mengi zaidi ya haya ambayo nanyi wadau wengine hapa JF mnaweza kuyaongezea
TCU na wadau wengine wa elimu ya juu litazameni upya jambo hili hasa huu uhuru wa kila chuo kujiwekea regulations zake hata kama zitakuwa zinaridhiwa na TCU.
Nafahamu haiwezekani vyuo vyote vikafana kwa kila kitu lakini kuna mambo kadhaa ya msingi ambayo yanayopaswa kuwa uniform baina ya vyuo vyote nchini kwenye swala zima la academic standards.