jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 25,958
- 24,541
`Muafaka baada ya uchaguzi haufai`
2008-07-20 13:02:52
Na Mwandishi Wetu
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro amesema utaratibu wa kutafuta muafaka baada ya uchaguzi mkuu, sio utamaduni unaopaswa kuendelezwa.
Badala yake amezitaka nchi za Afrika kujenga misingi imara ya demokrasia na kufanya chaguzi zilizo huru na haki ili kuepusha kupinga matokeo ya uchaguzi kunakosababisha kutumia muda mwingi na gharama kwenye mazungumzo ya usuluhishi wa migogoro inayotokea baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
Dk. Asha-Rose ambaye yupo nchini kwa mapumziko, alitoa ushauri huo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alikuwa akijibu swali la mwanahabari aliyetaka kupata maoni ya UN iwapo inaunga mkono utamaduni unaoibuka sasa barani Afrika wa kukimbilia kutafuta muafaka baina ya wanasiasa wanaodaiwa kushindwa kwenye uchaguzi mkuu kwa njia ya hila na wapinzani wao.
``Huo sio utamaduni wa kuendelezwa, kinachotakiwa ni kujenga utaratibu wa kuwa na demokrasia na kuelimishana kijamii,`` alisema na kuongeza kuwa, ``dawa ni kujenga misingi imara ya demokrasia na baada ya uchaguzi, isiwe tena tunatumia muda mrefu kushughulikia matatizo yatokanayo na uchachguzi mkuu.``
Mwishoni mwa mwaka jana vyama vya ODM na PNU vya Kenya viliingia kwenye mgogoro wa uchaguzi mkuu ambao mgombea wa ODM Bw. Raila Odinga, alidai ameshinda na kuibiwa ushindi na mgombea wa PNU Rais Mwai Kibaki.
Hali hili ilisababisha mamia ya wananchi kupoteza maisha, wengine kujeruhiwa vibaya na kupoteza mali, kuwa wakimbizi nchini Uganda yote hayo yalitokana na kuzuka kwa vurugu na mapigano baada ya jamii mbalimbali zilizokuwa zinapinga ama kukubaliana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na kumpa ushindi Rais Mwai Kibaki ambaye alidaiwa na wapinzani kuwa hakushinda kihalali.
Baada ya vurugu hizo, wasuluhishi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa zamani wa UN Dk. Kofi Annan, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) aliyemaliza muda wake Rais Ghana John Kufuor, mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Bi. Graca Machel ni miongoni mwa walishiriki katika kutafuta muafaka kati ya Rais Kibaki na mpinzani wake mkuu Bw. Raila Odinga.
Matokeo yao muafaka huo yalipelekea kuundwa kwa serikali ya mseto ambapo Bw. Odinga aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
Hali kadhalika, uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe hivi karibuni, umeibua hoja za kuanza mjadala wa usuluhishi baina ya Rais Robert Mugabe na mpinzani wake wa chama cha MDC Bw. Morgan Tsvangirai.
Kadhalika hali si shwari visiwani Zanzibar baina ya CUF na CCM ambapo CUF inadai ilipokonywa ushindi na CCM katika chaguzi zote za vyama na kumekuwa na milolongo ya mazungumzo ya mwafaka ambayo hayajawahi kukamilika.
Akizungumzia changamoto za UN, Dk. Asha-Rose alisema umoja huo unakabiliwa na tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta na chakula duniani hali ambayo ilimlazimu Katibu Mkuu Bw. Ban Ki Moon kuziomba nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani kuongeza uzalishaji huo.
Kuhusu chakula alisema Benki ya Dunia (WB) na Marekani zimekubali kutoa fedha kwa ajili ya kununua chakula kitakachopelekwa sehemu mbalimbali.
Alisema tayari Bw. Moon ameunda kikosi kazi ambacho kitaangalia mahitaji ya sasa ya chakula duniani na kwamba katika awamu ya pili umoja huo utaangalia namna ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupata mbolea na mbegu.
Alisema katika awamu ya tatu, suala litakalopewa kipaumbele ni kuboresha miundombinu ili kuwezesha kilimo na chakula kupatikana kwa wingi.
Alitaja changamoto zingine kuwa ni tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa, mazingira, ukimwi, malaria na tatizo la kusukuma maendeleo ambapo alisema ipo dira ya pamoja ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
Katika hatua nyingine, Dk. Asha-Rose amewataka Watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kupeperusha bendara ya Tanzania nje ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii, kujenga demokrasia, amani na kusaidia nchi zingine.
Alisema haitaridhisha iwapo ataambiwa aiangalie Tanzania katika suala la amani iwapo kutakuwa na machafuko.
Pia aliwataka Watanzania kuchangamkia kujifunza lugha zaidi ya mbili iwapo wanataka kupata kwa urahisi nafasi za kazi katika ofisi ya UN.
``Tuendelee kujitahidi katika lugha, Watanzania na baadhi ya nchi zingine wasiotumia lugha ya Kifaransa hawana nafasi kubwa sana wanapoomba kazi wakishindana na wengine wanaojua lugha mbili ya Kifaransa na Kiingereza.
Aidha alisema baadhi ya watu hawana utamaduni wa kubahatisha katika kutafuta, kwa kuwa kazi za UN ni za mkataba na wengi wanahofia kuacha kazi zao na kwenda kwenye kazi za mkabata.
Naibu Katibu Mkuu huyo leo anatarajiwa kwenda Zanzibar kumsalimia Rais Aman Karume.

- SOURCE: Nipashe