UNICEF: Zaidi ya watoto 6,000 wa Kiyemen wameuawa au kujeruhiwa katika vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
752
3,092
4bmy14037e89b8rq8e_800C450.jpg

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto 6,700 wa Kiyemen wameuawa au kujeruhiwa tangu Saudi Arabia ilipoanzisha hujuma yake ya kijeshi dhidi ya nchi masikini ya Yemen.

Taarifa ya Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) imeeleza kuwa, watoto 385,000 wa Yemen pia wanakabiliwa na hali mbaya ya lishe duni na kwamba, wanahitajia msaada wa haraka wa chakula.

Kadhalika UNICEF imesisitiza katika taarifa yake hiyo kwamba, kuna udharura wa kukomeshwa mashambulio dhidi ya watoto huko nchini Yemen.

Katika ripoti yake kuhusiana na kuzidi kuwa mbaya hali ya watoto katika maeneo yaliyokumbwa na vita kama Syria, Iraq na kwingineko duniani, Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ulisema hivi karibuni kwamba, unahitaji msaada wa dola bilioni 3.9 ili kuwasaidia watoto milioni 41 walio katika maeneo ya majanga kote duniani.

Saudi Arabia imeendelea kuishambulia kijeshi Yemen na kupuuza miito ya walimwengu ya kutaka kukomesha vita vyake hivyo
Tangu mwezi Machi 2015, Saudi Arabia kwa kushirikiana na Marekani, Imarati, utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi ilianzisha mashambulizi ya kinyama ya kila upande dhidi ya wananchi wa Yemen na kuwazingira kutokea angani, ardhini na baharini sambamba na kuendesha mashambulizi mtawalia ya kikatili dhidi ya wananchi hao Waislamu.

Watawala wa Saudi Arabia walidhani kuwa watamaliza vita hivyo muda mfupi tu, lakini karibu miaka minne sasa inapita na bado utawala wa Aal Saud na washirika wake wamekwama kwenye kinamasi nchini humo.
 
Hii ni hatari sana, kuna ripoti ilitoka last year mwishoni kwamba watoto sita wanakufa kila baada ya saa moja.
 
Back
Top Bottom