UNICEF: Athari za COVID19 kuongeza ndoa za Watoto zaidi ya Milioni 10 ndani ya muongo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Athari kubwa za janga la Covid-19 kwa wanawake katika baadhi ya mataifa huenda zikasababisha ndoa milioni 10 zaidi za watoto katika muongo huu, kwa mujibu wa tathmini iliyotolewa na UNICEF Jumatatu.

"Kufungwa kwa shule, msongo wa kiuchumi, kuvurugwa kwa huduma na vifo vya wazazi kutokana na janga la Covid-19 vinawaweka wasichana walio katika mazingira hatarishi zaidi, kwenye hatari inayoongezeka ya kuozeshwa wakiwa watoto," ulisema utafiti uliopewa jina la "Covid-19: Kitisho kwa mafanikio dhidi ya ndoa za watoto."

Mwelekeo huo, ikiwa utathibishwa, utasababisha kurejea nyuma zaidi mafanikio ya miaka kadhaa dhidi ya ndoa za watoto. Katika miaka 10 iliyopita, kulingana na utafiti huo, kiwango cha wanawake wadogo walioolewa wakiwa watoto kilipungua kwa asilimia 15, kutoka karibu moja katika wanne hadi moja katika watano.

Mafanikio hayo, "hivi sasa yanakabiliwa na kitisho," ilisema ripoti ya utafiti huo, iliyotolewa kwenye siku ya Wanawake Duniani. "Covid-19 imeifanya hali ambayo tayari ni ngumu kwa mamilioni ya wasichana kuwa mbaya zaidi," alisema mkurugenzi mtendaji wa Unicef Henrietta Fore.

"Shule zilizofungwa, kutengwa na marafiki na mitandao ya msaada, na umaskini unaoongezeka vimeongeza mafuta kwenye moto ambao dunia ilikuwa inapambana kuuzima."
 
Back
Top Bottom