Unguja: RC apiga Marufuku ngoma za vigodoro na Khanga moko. Asema ni kinyume na Maadili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga marufuku ya upigwaji wa ngoma za vigodoro pamoja ngoma ya kanga moja maarufu kama Kanga Moko katika Mkoa huo.

Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.

“Sio ruhusa kwa Wakazi wa Mkoa wa Kaskazini na Wananchi wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kuja kupiga ngoma na kucheza vigodoro na kanga moja “kanga moko”

Ameyasema haya wakati akitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu muelekeo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye miaka mitano ijayo Ofisini kwake Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

MillardAyo
 
Aaaah...aache hayo mambo... sasa sisi wengine hiyo ndio starehe yetu...sasa twende wapi?? Basi awakataze na wale wanaokunywa Pombe, wasinywe pia, ili twende sawa.
 
Tunasubiri mkoa wa Dar,,,, mtoto akisikia kigodoro yupo radhi akumwagie maji ya moto usoni ili umpishe aende.
 
Maadili ya wapi ?

Hao jamaa wajiongeze tu wafungue night clubs ili kuhakikisha wanaoingia na wanaotoa hizi huduma wote wanapenda na wala hawajashurutishwa...

Kama wasemavyo one person's meat is another one's poison na vice versa is true
 
Aliyeletaga huu msemo Mungu amuadhibu🙌🙌 Sasahivi elfu1 tuu inaheshimika kama anavyoheshimika babamkwe
kwako au kwa wale wanasiasa wanaozigawa kila wakienda huku na kule ?

Kodi zetu zimebanwa sehemu / mitaani ila kwa wachache hali ni tofauti (ingawa hakuna mzunguko ila kule inakotakiwa zitoke na zizunguke zimejaa)
 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga marufuku ya upigwaji wa ngoma za vigodoro pamoja ngoma ya kanga moja maarufu kama Kanga Moko katika Mkoa huo.

Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.

“Sio ruhusa kwa Wakazi wa Mkoa wa Kaskazini na Wananchi wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali kuja kupiga ngoma na kucheza vigodoro na kanga moja “kanga moko”

Ameyasema haya wakati akitoa taarifa kwa Waandishi kuhusu muelekeo wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye miaka mitano ijayo Ofisini kwake Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

MillardAyo
Huyu ana akili siyo yule alikwenda na mikasi kuwakamata vijana mtaani ati wamenyoa denge
 
Ayoub amesema kumekuwa na kawaida kwa Wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kuja katika Mkoa wa Kaskazini na kuja kucheza ngoma na starehe.
Hiyo ni nchi ya kiislamu, kwa nini wasitumie sheria za dini kudhibiti hayo mambo kwama wanavyofanya wakati wa mwezi wa Ramadhani?
 
Back
Top Bottom