Unguja: Bakari Mussa akamatwa na kete 32 za dawa za kulevya mbele ya kituo cha Polisi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Bakari Mussa Ame mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Tindini Unguja Ukuu amekamatwa kwa tuhuma za kujuhusisha na kete 32 zinazosadikiwa kuwa na Dawa za Kulevya huko Unguja Ukuu .

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa mnamo Octoba 2 mwaka huu majira ya saa tatu na nusu asubuhi akiwa na kete hizo 32 mbele ya Kituo cha Polisi cha Unguja Ukuu .

Nae sheha wa shehia hiyo Tindini Unguja Ukuu Simai Haji Makame amekiri kukamatwa kwa tuhuma huyo na kuwataka vijana hao wanaotumia madawa ya kulevya kuacha mara moja kwani wanapoteza nguvu kazi ya taifa.

Aidha Kamanda Suleiman amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano na jeshi hilo kwa kutoa taarifa zinazowahusu wahalifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Credit: Rauhiya Mussa Shaaban
 
Back
Top Bottom