Ungepewa nafasi leo kumshauri Jakaya Kikwete ungemwambia nini....?

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Hallo wana JF!! Ningependa kujua mawazo yenu kama great thinkers,Je,ukipata nafasi ya moja kwa moja kuongea na Jakaya Kikwete kuhusu mstakabali wa taifa hili kwasasa na baadae,UNGEMWAMBIA NINI?
 
Hallo wana JF!! Ningependa kujua mawazo yenu kama great thinkers,Je,ukipata nafasi ya moja kwa moja kuongea na Jakaya Kikwete kuhusu mstakabali wa taifa hili kwasasa na baadae,UNGEMWAMBIA NINI?


Atafute njia muafaka ya kuachi ngazi, kwani mambo yamemshinda, na hii ni kwa faida yake mwenyewe, familia yake na wapambe wake wa karibu yasije yakamkuta yaliyo wakuta wenzake.
 
baric watuachie mgodi wetu yani kibuku imelipa kodi zaidi yao wakati baric mapato yao ni US$$$ bilioni kazaa na hao kibuku wanatumia hii shilingi yetu nzembe ya madafu
 
Ningempongeza kwa safari zake nyingi nje ya nchi, ingawa hazina manufaa kwa nchi
 
Aachie ngazi kwa maana hata slogan yake anaikengeuka.Kwani alitamka kuwa atawapatia MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.Badala yake toka aingie madarakani anazidi kutupatia BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA.
 
Kwa sababu sio yeye anaye ongoza nchi, ( Magamba ndiyo yanaongoza). Aachie wenye uwezo wa kuyaondoa sasa na si 2015.
 
(a)Akajenge ikulu marekani na aongoze nchi kutokea huko ili kupunguza gharama za kusafiri kila cku kwenda marekani.. (b) aachie kuchochea udini
 
Hallo wana JF!! Ningependa kujua mawazo yenu kama great thinkers,Je,ukipata nafasi ya moja kwa moja kuongea na Jakaya Kikwete kuhusu mstakabali wa taifa hili kwasasa na baadae,UNGEMWAMBIA NINI?
Ningemwambia "im proud of my president because he is handsome" so aendelee kufanya make up mixxer Karolite azidi kuwa handsome.
 
Ningemwabia uongozi ni kipaji sio kukurupuka,ngemuukiza Ben aliacha dola bei gan na leo vp na kwann iko ivyo
 
Atende haki kwa wanyonge maskini wa nchi hii,,akumbuke yeye ni binadamu,,kuna kufa,atajaulizwa juu ya vile alivyovichunga
 
Hmhmhm......sijui niseme nini maana yako mengi sana........labda Awe kama Zuma....aoe wake wengi..................
 
Uzuri na yeye yumo humu jamvini.
Naomba asome yafuatayo
1.Ni rais aliyetegemewa na watanzania kuwa atatukomboa toka matatizo ya uchumi,siasa na kijamii suala ambalo limemshinda kwa 200% kwa sababu ameprove failure atuambie kwa nn asijiuzuru kabla ya 15
2.Atubu dhambi ya uongo anaowafanyia watanzania kwa ahadi hewa e.g maisha bora kwa kila mtanzania n.k
3.Anachokifanya kuchochea kwa umma kwamba chadema ni chama cha kikristo aache mara moja kwa sababu msajili wa vyama vya siasa hasajili vyama vya kidn basi kama ni hvyo sijawahi kusikia akitamka kwamba cdm ifutwe kwa kuwa ni chama cha dini
4.Aache kuwatumia waislam kama chambo i.e kuwadanganya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi wakati katiba hairusu serikali kuwa na dn
5.Aache kuhongwa anatuabisha sisi wanaume,kwa nn si tunamvalisha na kumlisha sisi wa2 wake bana.Hatujakosa hela za kumhudimia m2 mmoja
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom