Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,580
- 4,262
Natamani kuona mawazo chanya ya watanzania wakipendekeza nini kingefanyika ili kikidhi matarajio ya ndoto zao na za Taifa.
Hapa tuongelee maendeleo/Uchumi, mambo ya kampeni za siasa tuweke pembeni.
Kama hoja inahusu mkoa/eneo fulani litaje.
Binafsi napendekeza;
1. Vijana wetu wanao maliza Kozi za juu za Kilimo; kwa wale wenye ari ya kilimo wajiunge makundi ya vijana 20 hivi wa fani tofauti tofauti wapewe mtaji wa Tractor na pembejeo waka anzishe kilimo bora kwa mazao waliyo yachagua; kiwango cha chini cha shamba lao liwe angalau heka 100. Naamini hapo wata ajiri watu wengi wa kawaida. Tofauti na hapo ni kuhakikisha mikoa yenye Mvua nyingi inapata trector moja walau kwa kila kijiji na lifuatiliwe..lilete faida
2. Ajira za wataalamu (Diploma/Degree); kwa kuwa watu wapo wengi nafikiri viwepo vigezo vya ubora vilivyo wazi ili ziwafikie na wale wasio onekana.
3. Biashara mpya kabisa zingepewa angalau mwaka mmoja wa kutolipa kodi kwani kipindi hicho ni cha kujitangaza na pengine kusoma soko. Nafikiri utakuwa muda muafaka wa kulea biashara
4. Baada ya kuwa na sekondari, sasa tujenge Vyuo vya Veta na kuimarishwa vile vilivyopo; kwa kuanzia kuwe na mkakati wa kuwa na chuo kimoja kizuri kwa kila wilaya Kinachotoa elimu tofauti tofauti ya kujitegemea
6. Kila wilaya iweze kujenga ajira kwa vijana wake mf: kila mwaka wilaya iweze kuwawezesha vijana wake idadi flani kuweza kujitegemea (biashara, Kilimo, Ufugaji nk) na wafuatiliwe na kusaidiwa kiutaalam (mf vijana 100)
7. Mazao yanayo tumika ndani ya Nchi yawekewe utaratibu kwa soko la ndani kuyanunua kulingana na mahitaji
1: Korosho kwa wakulima imekosa soko ila soko la ndani halina korosho na wafanya biashara hawaruhusiwi kununua
ii: Miwa; wakulima wa nje wa kilombero wanakosa soko kwa kiwanda kuzidiwa na uzalishaji; serikali iingilie kati iwasaidie wakulima /kiwanda kupata mtambo mwingine
8......