Ungependa nani awe rais wako kati ya hawa?

W.Slaa anafaa sana kati ya hao watatu. sijaona ubaya wake zaidi ya jitihada anazoonyesha kupigania wanyonge. H.Mwinyi naogopa asijeiua nchi kama alivyofanya dingi yake enzi za utawala wake. mzee wa independent lowasa hafai hata kuonekana kwenye huu ukurasa. sifa zake mbaya, mtu mwenye tamaa tamaa ya mali, mwizi mwizi, richmond yeye, ametuibia ametosha hatumuhitaji tena.
 
Bwana John Pombe Magufuli anafaa zaidi kwa sababu;anamsimamo,mchapakazi na mpaka sasa bado hatujapata taarifa za uchafu kumhusu yeye.
 
John Pombe Magufuli,Anna Tibaijuka,Zito Zubdri Kabwe,Andrew Chenge,Bernad Membe,Edward Ngoyai Lowasa,Mizengo Kayanza Peter Pinda,Dr Wilbrod Peter Slaa,Fredirick Sumae,Freeman Aikaeli Mbowe,Anna Makinda,Asha Rose Mingiro,Getrude Mongella,Rostam Aziz,Agustine Mrema,Dk Ali Mohamed Shein,Seif Sharif Hamad,Prop Ibrahim Lipumba,Husein Mwinyi,Salim Ahmed Salim,Maik Mwandosya na Harison Mwakyembe?Je unapenda awe nani?

Kuna watu nimewamiss hapa. angekuwepo wassira au Lusinde ningechagua
 
magufuli mropokaji sana simfagilii mimi.

Sio mropokaji, mtendaji mzuri always hakosi wasiomkubali.
Kama humkubali yeye then unakubaliana na serikali ilio madarakani inayolea mafisadi kama mtu wa kawaida.
 
Dr Slaa anafaa japo hata awamu moja tutapata maendeleo kwa kutumia rasilimali zetu za nchi sisi Watanzania
 
Bwana John Pombe Magufuli anafaa zaidi kwa sababu;anamsimamo,mchapakazi na mpaka sasa bado hatujapata taarifa za uchafu kumhusu yeye.

Hana usafi wowote, uzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupa,na hata yeye alijiuzia nyumba adaestate kinondoni thamani ya soko wakati huo m400 yeye alijiuzia kwa m5 huo ulikuwa ni ufisadi akiwa waziri wa ujenzi kipindi cha mkapa.
 
mi nadhani raisi Dr Slaa,Makamu Dr Mohamed Shein speaker Zitto na waziri mkuu Freeman Mbowe
 
Rais - Dr. Slaa, makamo wake - Salim, waziri mkuu - Zito, speaker - Mbowe
 
naombea ccm wafanye kosa la kuweka mgombea wanayemtaka wao na akataliwe na wananchi.
 
Tumpe slaa angalau hata kwa kipindi kimoja tumcheki. Akifaa basi apige cah pili. Nina amini katiba haitakuwa ya kuchezea wakati huo -- hata kama akiwa mzuri kiasi gani.
 
Back
Top Bottom