Ungependa miaka 50 ijayo Tanzania ifanane na nchi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungependa miaka 50 ijayo Tanzania ifanane na nchi gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by J.K.Rayhope, Dec 9, 2011.

 1. J

  J.K.Rayhope JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo ni siku ya pekee sana nchini Tanzania ambapo ni kumbukumbu ya miaka 50. Miaka hamsini si mchezo. Ni rahisi sana kuitamka na kuandika, kiuhalisia ni jambo la kujivunia.

  Ni jambo la kawaida sana kwa mwanadamu kuiga kwa mwingine hasa mazuri na yale ya maendeleo.Tanzania ni watu kwa umoja wao, na dunia ni nchi kwa umoja wao.

  Zipo nchi nyingi sana duniani, na pengine nyingine zina maendeleo zaidi. Je,unadhani sisi tumeendelea? Kama jibu ndio, tunafanana na nchi gani? Kama jibu hapana tuna changamoto gani na tunataka tufanane na nchi gani yenye maendeleo kwa miaka 50 ijayo iliyoanza leo 2011 hadi 2061?
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,075
  Trophy Points: 280
  Ningependa ifanane na Jerusalemu Mpya.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  USA or Canada lakini ukweli ni kwamba tutakuwa Brazil. Brazil ilikuwa kama Tanzania ilivyo sasa miaka kama 15 iliyopita kila mtu mwenye pesa alikuwa na ukuta, rushwa ilikuwa kubwa sana Brazil na viongozi walikuwa kama wa Tanzania ambao wanajifanya wanajua kila kitu lakini hakuna cha kuongeza. Vilevile kama Tanzania kulikuwa na mafuta, madini, kilimo n.k lakini watu walikuwa masikini. Brazil leo inauchumi mkubwa kuliko India na Russia, watu hawaogopani teni hivyo hakuna ukuta kila nyumba. Brazili walipata kiongozi mzuri sijui kama sisi tutabahatika lakini kizazi chetu cha chini ya miaka 40 kitabadilisha nchi sana
   
 4. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Vanuatu!
   
 5. d

  dada jane JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natamani tuwe kama Rwanda. Wako serious na mambo karibu yote yaani ya kimwili na kiroho angalia uchumi unavyokuwa, pia nimewapenda hata kwaya yao ya ambasador wamenikumbusha enzi za upendo group
   
 6. William Mtitu

  William Mtitu Verified User

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mm ningependa ifanane na TANGANYIKA
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kama waTZ wataendelea kuwa mazuzu kwa kuichagua ccm, tanzania itakuwa inafanana na afghanistani kwa kujaa milima ambayo itasababishwa na vifusi vya wezi wa madini yetu. na kipindi hiko zao la bangi na unga itakuwa ni kawaida tu maana katika milima, 'kitu cha arusha hustawi vyema'
   
 8. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,172
  Trophy Points: 280
  Somalia nchi hii ina viongozi wasanii Haitoweza kuendelea.
   
 9. Amani Nyekele

  Amani Nyekele Senior Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  be a country of its identity where peace, order, human rights and freedom of expression are core values
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wala hatutafika 50 years tutakuwa kama China..
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono Mkuu!
  Inawezekana kabisa ujitoa katika hii skendo ya kuwa among top three wa kuombaomba.Unajua, kuomba kwa kweli ni fedheha.Kuna watu wachache sana wenye kuona afadhali wajifedheheshe waombe.Wengi huona ni bora kufa njaa kuliko kuombaomba.
  Ningependa kuona Tanzania yenye watu waliokataa kuombaomba na badala yake wakachukua hatua kubadili hali zao.Hii inatia ndani vongozi wetu.Yahitaji mapinduzi ya kifikra kuamini kuwa tunaweza kujitegemea kwa kutumia vizuri rasilimali zetu tulizojaaliwa na Mungu.
   
Loading...