Ungependa kuwa na Mamlaka na Ushawishi Duniani? Anzisha Secret Society yako

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Watu wengi wana hamu kubwa ya kuwa na sauti kwenye jamii zinazowazunguka. Wengine wana malengo makubwa zaidi ya kutawala nchi, kuitawala dunia, kuwa na ushawishi mkubwa katika biashara au fani fulani, nk.

Kuna njia ya kufanikisha hilo ambayo wengi wanadhani ni ngumu sana lakini labda ndiyo ya urahisi na uhakika zaidi. Na halihitaji pesa nyingi wala elimu kubwa kama wengi wanavyodhani.

Kinachohitajika ni uvumilivu wa hali ya juu kwa sababu itakuchukua muda mrefu kidogo kufikia malengo yako ila nakuhakikishia ukizingatia mambo muhimu utafikia malengo yako hayo 100% hata yakiwa makubwa kivipi.

Njia hiyo ni kuanzisha kikundi chako cha siri au yanayojulikana maarufu kama Secret Society.

Hili jambo unaweza kuanzisha mwenyewe 'from scratch' yaani kuanzia sifuri. Hapa siongelei kujiunga sijui na Illuminati, Skull and Bones, Knight Templer, nk. Hapa naongelea kuanzisha lako mwenyewe utakalolitungia mwenyewe malengo, sheria na kanuni zake zitakazoiendesha.

Binafsi naona kuna njia mbili ambazo unaweza kuanzisha Secret Society yako mwenyewe.

Moja ni kupitia kizazi chako mwenyewe na njia ya pili ni kwa kuweka watu pamoja walio katika fani mbalimbali muhimu.

Nitarudi kuzielezea hizi zote mbili baadae.
 
Watu wote wanaomiliki hizo system wana pesa nyingi. Kwa sababu kuna gharama kubwa sana ya kumpika mtu na kumfanya awe loyal kwako.
 
Watu wote wanaomiliki hizo system wana pesa nyingi. Kwa sababu kuna gharama kubwa sana ya kumpika mtu na kumfanya awe loyal kwako.

Hapana siyo lazima kuwa na pesa wala elimu kubwa. Mtaji mkubwa ni kuwa na malengo sahihi, mbinu sahihi, nidhamu ya kutoyumba na uvumilivu. Pesa inasaidia sana ila siyo muhimu.

Pesa peke yake hainunui loyalty.

Nitarudi kuelezea kwa mapana.
 
Back
Top Bottom