palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,455
Hiki ninachoandika hapa ni kisa cha kweli kilichotokea hivi karibuni. Umeoa na ndoa yako ina miaka miwili hivi na mnatarajia kupata mtoto (mkeo mjamzito) na kwa mila zetu za kiafrika mama wa mume huwa na majukumu ya kumlea mkeo baada ya kujifungua. Kama alivyo ada unamfahamisha mkeo kuwa mama atakuja toka kijijini ili kukupa support, mkeo anakujibu kuna ulazima gani mama yako kuja huku mbona mama yangu yupo (mama wa mkeo anaishi mjini ambako nanyi mnaishi).Lakini pamoja na mkeo kukomaa unaamua kumuita mama yako toka kijijini na mama anakuja ili ashuhudie akipata mjukuu ukichukulia wewe ndiye mtoto wa kwanza wa kiume kuoa na mama hajawahi pata mjukuu. Mama anafika lakini hali inakuwa tofauti mkeo hamthamini kabisi mama yako ikiwemo kuondoka kwenda kusiko julikana mchana wewe ukiwa kazini na muda mwingine anamucha mama yako bila chakula mpaka mama akupigie simu (wewe ukiwa kazini) kula anakufa njaa maana mkeo kaondoka kaenda kusikojulikana na hajamuuaga mama yako na bila kumuacha na msosi. Kama haitoshi mkeo ameenda kujifungua anaruhusiwa kurudi nyumbani anagoma anataka aende kwa wazazi wake (ili tu asihudumiwe na mama yako) . lakini wewe unagoma mnarudi kwenu. Mungu si athumani unapata safari ya kusoma kwa mwaka mmoja ngambo huku mama akiwa hajaondoka. zinapita wiki mbili mama anaondoka kwenda nyumbani lakini mkeo anashindwa kumpa mama yako hela ya kula njiani (wakati huohuo mkeo anachukua sehemu ya mshara wako). baada ya miezi kadhaa mkeo anakutana na mtu wa jirani yako na kumwambia vituko alivyokuwa anamfanyia mama yako na kwamba suala la hela unazopata wewe ni zake na wewe tu, mama yako na ndugu wengine waliyokuwa wanakutegemea wajue kwa kwenda. Mungu si athumani maneno yanafikia mama yako, mama analia sana maana anakumbuka alivyokulea mpaka ukafika hapo na sasa una kazi nzuri. Hata hivyo mkeo baada ya kujua mama yako amepata taarifa na huenda na wewe una taarifa anakupigia simu kumutuhumu mama yako mambo yeye aliyoongea kwa mtu wa jirani yako ni mama yako ndiyo aliongea . lakini baadaye hali inakuwa siyo maana ukweli unajulikana na yale yote yalioongelewa mama anakumbuka ni kweli yalikuwa yanatoke kipindi yupo kwako . Mama anaapa hata kuja kwako (kwa mkeo) na hataongea naye (mkeo) mpaka atakapo ingia kaburini.Wakati huohuo mume anawasaidia upande wa kike ikiwemo kulipa ada ya shemeji zake.UNGEKUWA WEWEYAMEKUTOKEA HAYA UNGEFANYA NINI (KWA SASA BADO UPO NGAPO NA HUJARUDI)