Ungekuwa wewe ungeweza?

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Jamaa yetu mmoja mnamo mwaka juzi alimfumania 'ugoni' mkewe.

Ilivyokuwa,

...kama ilivyojadi ya wanawake wengi huko vijijini hasa mida ya jioni huelekea palipo na kijipori kwa ajili ya kusenya/kukusanya kuni kwa ajili ya kupikia chakula.Na ndivyo ilivyokuwa kwa mke wa jamaa yetu.

Sasa basi,baada ya chakula cha mchana dada yule alielekea huko polini kwa ajili ya kusenya kuni.Pamoja na hilo pia alikuwa na miadi ya kukutana na mtu wake wa kando hukohuko polini ili wafanye na mambo yetu yale.Si unajua tena quest za vijijini huwa vichaka!

Msenya kuni alifika eneo la zilipo kuni na bahati iliyoje na mtu wa kando naye wakati uleule naye alifika.Wakakutana.Stori za hapa na pale za kimahaba zilianza mara moja na mara paaa, watu chini 'kuendeleza ibada.'

Kumbe mme alitonywa na msiri fulani.

Nyendo zote za mkewe alizifuatilia na hali ilipelekea kuwakamata ugoni wawili wale!Ajabu na haikutarajiwa na wagoni wale mme alimuomba mkewe asimamame waelekee nyumbani na kwa upande wa mgoni wake alimpa pole ya kazi na alimkanya asirudie jambo lile.Du!

Mke alilia njia nzima eti akiomba apewe adhabu na mme yule lakini jamaa alikataa katukatu kwamba hawezi mpiga ama kumfanya chochote kwa sababu anampenda sana!Hakika walifika nyumbani huku mke akigugumia kwa kilio cha kuweweseka asielewe yule mmewe atamfanya nini baadae-hakuelewa.

Mme alimsihi mke yule apike haraka ili wale na alifanya.Muda wa kuelekea chumbani kulala usiku iliwadia mme alitangulia lakini mke alibakia jikoni akilia na asijue la kufanya.Mme alimfuata mkewe jikoni na kumbembeleza waeleke chumbani watayazungumza na yataisha.Muda wote mke alikuwa akimwomba mme japo ampige ama ampe adhabu yeyote lakini jamaa aligoma katakata!

Ilipita wiki,miezi na miaka miwili baadae mme hakumfanya lolote mke yule.Na muda wote ule jamaa alimwonyesha upendo uleule wa siku zote mkewe kana kwamba lolote halikutukia.Jamaa alitisha!

Siku moja ya jioni mke aliitarifu familia kwamba wajiandae keshoye wataelekea ukweni kwake yaani kwa wazazi wa mke kwa minajili ya salamu.Kwa bashasha mke aliwaandaa wanawe na yeye pia.Kesho ilifika na walisafiri na kufika salama ukweni na waliwakuta wazee hawajambo na familia nzima.

Siku ya kwanza,pili na ya tatu zilitimu wakiwa na furaha pale ukweni.

Siku ya nne jioni kabla ya chakula mme wa mtu alimtaarifu mkwewe yaani baba yake na mzee kuwa anaomba aitishe kikao cha familia ili pamoja na kuwaaga pia alikuwa na mazungumzo nao.Mzee alifanya na kikao kikawa.

Pamoja na yote mme aliielezea familia mkasa wote wa namna alivyomshika ugoni mkewe na kwa muktadha huo yeye aliamua amrejeshe binti yao akiwa salama na mzima wa bukheri bila kumjeruhi na rasmi anawakabidhi na siyo mke wake tena.

Mali na vyote walivyochuma pamoja yupo tayari wagawane na hata mahali hakuwa na shida ya kurejeshewa.

Mke yule alizimia!

Jamaa hakutania na vyote alifanya na hivi juzi kaoa mke mwingine.

Je, ingekuwa wewe ungechukua hatua gani?
 
Nipo hapa kwa ajili ya kucheka 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
(Jitombashisho)

Dawa ya coruna ya nimri ipewe jina hili ...Aki Coronababy lazima akimbie.
 
Jamaa inaonekana alikua yuko mguu nje mguu ndani hakua stable kwenye maamuzi

Inaonekana msela alimpenda mno mke wake na kwa muda wote huo alikua akiishi kwa ku fake yaani usoni sura bashasha lakini moyoni ameikumbata huzuni.

Hapo hakuna tofauti sio upande wa.mwanamke ndio wenye depression hata msela atakua anapitia kipindi kigumu the same kama mwanamke
 
Back
Top Bottom