Ungekuwa wewe ungefanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by yus4tanzania, Sep 12, 2008.

 1. y

  yus4tanzania New Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Sep 12, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani
  waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda
  kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule
  uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula.
  Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule
  waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

  Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa
  wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.

  Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

  Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao
  umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa
  alivyokula.

  Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa
  kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe
  kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza
  akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike
  anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine
  watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

  Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nani nitubu Kwako.
  Huyu mtoto wa kiume mdogo si wakon nilizaa na Shamba boy wetu na huu
  ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

  Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.

  Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani
  na kukuta wakigombana. Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu
  ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule
  nnje?
  Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki
  wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

  Fikiria ni wewe ITAKUWAJE?
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  .....Tumeshasameana kila mtu ameanika uovu wake umejulikana maisha yanaendelea.....Ngoma draw!!!!!!!
   
Loading...