Ungekuwa wewe ungefanyaje au ungejibuje kwenye hili?

Macbook pro

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
661
896
Habarini za mchana huu wadau wa jamvi letu pendwabla MMU, natumaini mu wazima wa Afya na mnaendelea pilika pilika za kujitafutua ridhiki.

Asee kuandika udhibnahitaji mawazo na michangi yenu kwenye mkasa ufuatao. Mimi ni kijana wa Kiume (29) nina mpenzi wangu (She is 23). Eee bhana, huyu mpenzi anakitabia binafsi mimi sikipendi leo nimeamua kumwambia ili nisiendelee kuwa naumia au naudhika.

Mwenzangu huyu huwa anapokuwa anasifiwa na wanaume huko mtaani, atapiga simu ananiambia mara “leo babe nimesifiwa na mwanaume eti nina hips na shape nzuri”. “Mara leo hii nimeambiwa na mwanaume nimependeza sana “ Mara oooh l”eo nimeambiwa ni mzuri kweli na Mwanaume”

Sasa leo kaja kwenye normal text tukiwa tunachati vitu tofauti tofauti, sasa mara naambiwa Babe ninaubuyu, nikamwambia una ubuyu? Ngoja nikupigie nisikie huo Ubuyu. Kumpigia simu, anachokuja kuniambia, nikiwa natembea njiani kuna mwanaume kanisifia eti “dada umependeza kweli” Nikajibu sawa nikawa nimemaliza na mood yangu. Nikamuuliza mambo mengine? Ili niachane na hiyo habari. Na kwenye text ikawa hivi.
 
Mkuu shida haiko kwake tu inaelekea hata wewe humsifii huyo unayeita ni mpenzi wako, ndio maana akirudi anajaribu kukuonyesha vile wengine wameviona wewe huvioni.

Jaribu kumsifia Mara kwa mara uone Kama ataendelea na hako katabia, naamini utakuja kutoa mrejesho mkuu!
 
Umemaliza au bado unaendelea?

Kwa nini usimuambie hupendi hiyo tabia au unaogopa utaachwa?

Mpe mimba ataacha utoto (jokes)
 
Mkuu shida haiko kwake tu inaelekea hata wewe humsifii huyo unayeita ni mpenzi wako, ndio maana akirudi anajaribu kukuonyesha vile wengine wameviona wewe huvioni.

Jaribu kumsifia Mara kwa mara uone Kama ataendelea na hako katabia, naamini utakuja kutoa mrejesho mkuu!

Ahsantee mkuu kwa mrejesho, ila kama kumsifia namsifia sana tu mzee. Mpaka wakati mwingine huwa ananiambia namvimbisha kichwa misifa. Ila ushauri wako nimeuelewa
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom