Ndugu zangu,
Hebu kwa dakika moja turudi kwenye ubinadamu na tutafakari kwa kutumia akili zetu timamu. Hebu fikiria kwamba umepigwa risasi zaidi ya thelathini (30)!!!!, maana yake lengo lilikuwa kukutoa uhai. Bahati nzuri Mungu amekuwa upande wako umenusurika.
Licha ya kunusurika kifo bado ofisi yako (Bunge) haikupatii haki zako stahiki za matibabu wala kupewa pole kama taasisi. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aidha aliyekupa pole au angalau kulaani waovu waliofanya jaribio lile.
ItSi Rais, Si Makamu, Si Waziri Mkuu, Si Waziri anayeshukulika na usalama wa raia - angalau aliyeguswa kwa tukio lile la kinyama. Cha kushangaza hadi leo HAKUNA juhudi wala uchunguzi wowote uliofanyika kuwakama wahusika UNGEKUWA WEWE NI TUNDU LISSU UNGEFANYAJE!!??
Ni tukio lisilo la kibinadamu kuwahi kutokea nchini Tanzania na limetia DOA kubwa nchi yetu.
Tuweke ushabiki wa kisiasa pembeni, tuweke jazba pembeni, tuwe wakweli wa nafsi zetu, kama binadamu wenye moyo wa kibinadamu. Tutumie akili zetu timamu tulizopewa na Mungu. Hisia, ushabiki na jazba zitatuhamisha na tukashindwa kufikiri vizuri.
Tujifunze kujadili CHANZO na sio MATOKEO. Achana na siasa na anza kutafakari kwamba Tundu Lissu ni binadamu wa kawaida, labda kaka yako, baba yako, mume, au binadamu mwingine wa kawaida, mwenye haki ya kuishi kama wengine.
Tundu Lissu anapigania roho yake binadamu aliyenusurika kifo, na yanayoendelea sasa ni matokeo ya kilichomkuta, hivyo ni vema tujadili chanzo kuliko matokeo ya anachofanya leo.
Kitu gani kina thamani zaidi kulinganisha uhai wa binadamu?