Ungekuwa wewe: Part. 1

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,672
40,549
Tatizo:

Kufurika kwa maji katika mitaa ya Jiji la Dar-es-Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa magari, wapita njia na uharibifu wa barabara na majengo.

Kwa miaka nenda rudi maeneo ya Jangwani na maeneo mengine jijini hujikuta yakifurika maji kutokana na mfumo mbaya wa kuchukua maji machafu na kuyatupa baharini au kuyazungusha na kuyasafisha. Kwa jiji la watu zaidi ya milioni tatu ambalo kwanza meza ya maji (water table) iko karibu sana ni vigumu kuwa na mvua bila kusababisha mafuriko au madimbwi.

Ni kwa sababu hii utakutana katika baadhi ya mitaa tayari wamepanga matofali au matairi ya magari kwa ajili ya wakati wa mvua ili vitumike kama vivukio.

Hata hivyo, Watanzania wameweza kuaccommodate mafuriko ya maji kiasi kwamba wameyazoea kiasi cha kukubali kuwa hiyo ndiyo hali halisi.

Hata hivyo mafuriko haya yanaleta matatizo mengi, magonjwa ya kuambukiza, uharibifu wa mazingira, mmomonyoko wa udongo, uharibifu wa majengo na zaidi ya yote kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwa na maisha ya usumbufu usiowalazima. Maji haya machafu husambaza uchafu na mara baada ya mvua basi mazingira yanakuwa yamebadilika sana.

UNGEKUWA WEWE:


Sasa tatizo la mafuriko, madimbwi na kusimama maji katika jiji la Dar na bila ya shaka mikoa mingine ni tatizo sugu ambalo tangu uhuru halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Hata hivyo, kasi ya maendeleo inaongezeka kwa watu kujenga majengo makubwa, mazuri na yenye kuvutia ambayo hupendeza sana pasipokuwepo mvua.

a. Maji yanayotuwama kwenye mitaa iliyo nje ya Jiji yanaweza vipi kushughulikiwa?

b. Maji kwenye katikati ya jiji ambako kuna barabara za lami yanaweza vipi kuondoshwa au tukubali kuwa ndiyo hali halisi?

Je kama wewe ungetakiwa utolee maoni tatizo la mafuriko na maji kutuwama kwenye miji yetu ungependekeza nini kifanyike?

a: Ndani ya muda mfupi (kudhibiti hali ilivyo sasa)
b: Ndani ya muda mrefu (kuondokana kabisa na tatizo la maji kutuwama katikati ya jiji na uswahilini?
 
Ndani ya muda Mfupi

1.storm water drain zote zifanyiwe major maintenance

2.Vichimbwe visima only ktk problem araes 10inch or 12inch diameter 150ft or 200ft deep respectively


Ndani ya Muda mrefu

1.Ifanyike Topo survey ya Dar es salaam Nzima ili tuweze kujua terrain ilivyo pamoja na other developments

2.wataalamu wa Drainage (note this is a specialized field), waje na master plan
3.Capacity building in this specialised area.

Fundi Mchundo/Mtanzania/Morani and others wanaweza kuongezea zaidi nini kifanyike au kukosoa nilichopendekeza

nawakilisha
 
Pia tunapofikiria suluhisho la tatizo hili tufikiri kama kweli linawezekana na kama linahitaji msaaa wa "wafadhili"
 
MMKJJ,

kwa mapendekezo niliyoyatoa hapo juu.....yako within our (Governement) reach.......watu wangekuwa na planning na action plan nzuri wala kusingekuwepo na kurudisha zaidi ya 50% ya bajeti hazina kama ilivyoonekana kule Singida
 
Manispaa K`ndoni kukarabati mitaro yote ya maji machafu

2008-05-06 16:06:19 (Nipashe)
Na Valery Kiyungu, Kinondoni


Mwenyekiti wa Mipango Miji katika Manispaa ya Kinondoni, Bw. Rajabu Hassan, amesema ofisi yao iko katika mchakato wa kukarabati mitaro yote ya kupitisha maji machafu iliyoko katika Manispaa yao ili kuimarisha hali ya usafi na pia kurahisisha utunzaji wa barabara.

Na kwa kuanzia, Bw. Hassan amesema watafanya zoezi hilo kwenye kata saba ikiwemo ya Manzese ambayo karibu mitaro yake yote imeziba, kisha wataendelea katika kata nyinginezo.

Bw. Hassan amesema hayo katika mahojiano maalum kuhusiana na mikakati ya ofisi yake, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema katika bajeti ijayo ya mwaka huu, wamepanga kukarabati mitaro yote na hivyo kukamilisha zoezi hilo.

Amesema maazimio hayo yamefikiwa katika kikao cha hivi karibuni cha wajumbe wa kamati yao ya mipango miji, ambapo pamoja na mambo mengine, kwa kauli moja wamekubali kuwa baada ya kutengewa bajeti ya fedha, wafanye zoezi hilo la kusafisha mitaro ya maji machafu.

Amesema imebainika kuwa mitaro iliyoko katika hizo saba ipewe kipaumbele katika ukarabati huo kutokana na ukweli kuwa mifereji iliyoko kwenye kata hizo iko katika hali mbaya zaidi na hivyo kusababisha nyumba za wakazi kufurika maji pale panaponyesha mvua, hata kama mvua zenyewe si kubwa sana.

Ukiondoa Manzese, kata nyingine zitakazonufaika na zoezi hilo ni za Mwananyamala, Ndugumbi, Tandale, Hananasif, Magomeni na Mzimuni.

``Maandalizi kwa ajili ya zoezi hilo yameanza na tunaamini kuwa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa,`` akasema Bw. Hassan.

Bw. Hassan amesema hatua hiyo ya ofisi yake kuanza ukarabati kwenye kata hizo, inalenga katika kuwaondolea kero ya muda mrefu wakazi wa maeneo hayo ambao baadhi nyumba zao hujaa maji wakati wa mvua.

Wakati huo huo Bwana Rajabu amesema kuwa uongozi wake baada ya kukamilisha zoezi zima la kukarabati mitaro, umepanga kupambana na watu ambao wana tabia ya kutupa taka kwenye mitaro ya maji machafu.

Akasema hatua mojawapo ni kuwaburuza kortini watu wote watakaoendelea kutupa taka kwenye mitaro ya kupitishia maji machafu na yale ya mvua.
 
Ogah, BabaH, MKJJ, good observation but with those proposed short and long term plans na watu wetu kwenye hayo maeneo waelimishwe juu ya matumizi ya hii mifereji jamani usishangae kuona watu usiku wanatupa viroba na rambo zilizojaa takataka miferejini hivi kweli hata kama una mifereji iliyojengwa vizuri itasaidia kweli??? Siju tatizo ni nini kutokuwa - civilized au?? nisaidieni..
 
Mkuu Mwanakijiji hili ni swali zuri sana.

Naanza kwa kuwakumbusha hali iliyokuwepo Hannasif pale Kinondoni wengine wanapenda kuita TX. Wananchi wa eneo hilo wakishirikiana na Chuo cha Ardhi (UCLAS kipindi hicho) na wafadhili waliweza kuchimba mifereji ya maji ya mvua. mpaka sasa tatizo la mafuriko Hananasif limekuwa historia.

Hivyo panahitajika ushirikiano kati ya wananchi, NGOs, Civil socities na Serikali ili kuchimba mifereji ya maji ya mvua.

Katika maeneo yenye mifereji, izibuliwe. Lakini kwanini haizibuliwi mbona wananchi wanalipa kodi za majengo?

Nionavyo mimi, technologia ya kuvuna maji ya mvua inahitajika sana. Kwanza dar kuna uhaba wa maji, hivyo kuvuna maji ya mvua kungesaidia sana kutatua taizo la uhaba wa maji wakati huo huo tatizo la mafuriko.

Naungana na Ogah juu ya kufanya tathmini ya jiji zima ilikuona terrain ilivyo. Ninahisi mifereji iliyopo haitoshi kuondoa maji yote hasa eneo la mjini. Mifereji hiyo imejengwa miaka ya 47, makisio ya kipindi kile yamepitwa na wakati. Kumbuka kwamba majengo yanavyoongezeka na pavements zinavyozidi kujengwa zinaongeza run off.
 
Mimi nimekuwa nikifuatilia jambo moja ambalo limekuwa likinishangaza kidogo. Kwanini tunapotengeneza mifereji tunaweka ile ya alama ya V ambayo juu iko wazi, kama hii?

8.jpg


Matokeo yake mvua ikinyesha si ndio yanakuwa haya?

Image001.jpg


Kwanini tusitandaze drainage ya kama tubes?
 
Back
Top Bottom