Ungekuwa wewe Mmbongo tunavyokujua ungefanya kwako

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Ikawa baada ya mambo
hayo, mke wa bwana wake
akamtamani Yusufu,
akamwambia, Lala nami.
Lakini akakataa,
akamwambia mke wa bwana
wake, Tazama, bwana wangu
hajui kitu kilichowekwa kwangu
nyumbani, na vyote alivyo navyo
amevitia mkononi mwangu.
Hakuna mkuu katika
nyumba hii kuliko mimi, wala
hakunizuilia kitu cho chote ila
wewe, kwa kuwa wewe u mkewe.
Nifanyeje ubaya huu mkubwa
nikamkose Mungu?
Akawa akizidi kusema na
Yusufu siku baada ya siku, lakini
hakumsikia alale naye, wala
aongee naye.
Ikawa, siku moja, akaingia
nyumbani atende kazi yake, wala
hapakuwa na mtu katika watu wa
nyumbani humo ndani;
huyo mwanamke
akamshika nguo zake, akisema,
Lala nami. Yusufu akaiacha nguo
yake mkononi mwake, akakimbia,
akatoka nje.
Ikawa alipoona ya kwamba
amemwachilia nguo yake
mkononi mwake, naye amekimbia
nje,
akawaita watu wa
nyumbani mwake, akasema nao,
akinena, Angalieni, ametuletea
mtu Mwebrania atufanyie
dhihaka. Ameingia kwangu, ili
alale nami, nikalia kwa sauti kuu.
Ikawa, aliposikia ya kuwa
nimepaza sauti yangu na kulia,
aliiacha nguo yake kwangu,
akakimbia, akatoka nje.
Basi akaiweka ile nguo
kwake hata bwana wake aje
nyumbani.
Naye akamwambia kama
maneno hayo, akisema, Yule
mtumwa Mwebrania uliyemleta
kwetu, aliingia kwangu anidhihaki.
Ikawa nilipopaza sauti
yangu, nikalia, akaacha nguo
yake kwangu akakimbia nje.
Ikawa bwana wake
aliposikia maneno ya mkewe
aliyomwambia, akisema, Mtumwa
wako amenitendea mambo kama
haya, hasira yake ikawaka.
Bwana wake akamtwaa
Yusufu, akamtia gerezani, mahali
walipofungwa wafungwa wa
mfalme, naye akawamo humo
gerezani.
Lakini Bwana akawa
pamoja na Yusufu, akamfadhili,
akampa kibali machoni pa mkuu
wa gereza.
Mkuu wa gereza akawatia
mkononi mwa Yusufu watu wote
waliofungwa, waliomo gerezani;
na yote yaliyofanyika humo ndiye
aliyeyafanya.
Wala mkuu wa gereza
hakuangalia neno lililoko mkononi
mwa Yusufu; kwa kuwa Bwana
alikuwa pamoja naye. Bwana
akayafanikisha yote aliyoyafanya.40.1 Ikawa, baada ya mambo
hayo, mnyweshaji wa mfalme wa
Misri, na mwokaji wake,
wakamkosa bwana wao, mfalme
wa Misri.
40.2 Farao akawaghadhibikia
maakida wake wawili, mkuu wa
wanyweshaji na mkuu wa
waokaji.
40.3 Akawatia katika lindo
nyumbani mwa mkuu wa askari,
humo gerezani, mahali
alipofungwa Yusufu.
40.4 Mkuu wa askari akamwekea
Yusufu watu hao, naye
akawahudumu, nao wakakaa siku
kadha wa kadha katika kifungo.
40.5 Wakaota ndoto wote wawili,
kila mtu ndoto yake usiku mmoja,
kila mtu kwa tafsiri ya ndoto
yake, mnyweshaji na mwokaji wa
mfalme wa Misri waliofungwa
gerezani.
40.6 Yusufu akawajia asubuhi,
akawaona wamefadhaika.
40.7 Akawauliza hao maakida wa
Farao, waliokuwa pamoja naye
katika kifungo, nyumbani mwa
bwana wake, akisema, Mbona
nyuso zenu zimekunjamana leo?
40.8 Wakamwambia, Tumeota
ndoto wala hapana awezaye
kuifasiri. Yusufu akawaambia,
Kufasiri si kazi ya Mungu?
Tafadhalini mniambie.
40.9 Mnyweshaji mkuu
akamhadithia Yusufu ndoto yake;
akamwambia, Katika ndoto yangu
nimeota, uko mzabibu mbele
yangu.
40.10 Na katika mzabibu
mlikuwa na matawi matatu, nao
ulikuwa kana unamea, unachanua
maua, vishada vyake vikatoa
zabibu zilizoiva.
40.11 Na kikombe cha Farao
kilikuwa mkononi mwangu,
nikazitwaa zabibu, nikazikamua
katika kikombe cha Farao,
nikampa Farao kikombe mkononi
mwake.
40.12 Yusufu akamwambia,
Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi
matatu ni siku tatu.
40.13 Baada ya siku tatu Farao
atakiinua kichwa chako,
atakurudisha katika kazi yako;
nawe utampa Farao kikombe
mkononi mwake, kama desturi ya
kwanza, ulipokuwa mnyweshaji
wake.
40.14 Ila unikumbuke mimi,
utakapopata mema, ukanifanyie
fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa
Farao, na kunitoa katika nyumba
hii.
40.15 Kwa sababu hakika
naliibiwa kutoka nchi ya
Waebrania, wala hapa sikutenda
neno lo lote hata wanitie
gerezani.
40.16 Mkuu wa waokaji alipoona
ya kwamba hiyo tafsiri ni ya
mema, akamwambia Yusufu,
Mimi kadhalika nilikuwa katika
ndoto yangu, na tazama, ziko
nyungo tatu za mikate myeupe
juu ya kichwa changu.
40.17 Na katika ungo wa juu,
mlikuwa na kila namna ya
chakula kwa Farao, kazi za
mwokaji; ndege wakavila katika
ungo juu ya kichwa changu.
40.18 Yusufu akajibu, akasema,
Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu
ni siku tatu.
40.19 Baada ya siku tatu Farao
atakiinua na kukuondolea kichwa
chako, na kukutundika juu ya mti,
na ndege watakula nyama yako.
40.20 Ikawa siku ya tatu, siku ya
kuzaliwa kwake Farao,
akawafanyia karamu watumwa
wake wote; akakiinua kichwa cha
mkuu wa wanyweshaji, na cha
mkuu wa waokaji, miongoni mwa
watumwa wake.
40.21 Akamrudisha mkuu wa
wanyweshaji katika kazi yake ya
kunywesha, naye akampa Farao
kikombe mkononi mwake.
40.22 Bali akamtundika mkuu wa
waokaji, kama Yusufu
alivyowafasiria.
40.23 Lakini huyo mkuu wa
wanyweshaji hakumkumbuka
Yusufu, alimsahau.
 
Back
Top Bottom