Kobe
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 1,794
- 808
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameuomba Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia kuchangia katika ujenzi wa barabara ya Manyoni -Kigoma ambayo ni sehemu ya barabara muhimu ya Central Corridor.
Rais amesema kuwa barabara hiyo inayokadiriwa kuwa na kilomita 700 ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na kwa matumizi ya nchi za jirani na hasa Burundi.
Najua mnatusaidia katika miradi mingi, ikiwamo ile mitatu ya maji na tunashukuru sana. Lakini mahitaji ya maendeleo ya binadamu hayana mwisho ningefurahi sana kama Saudi Fund ingeshiriki katika kusaidia ujenzi wa barabara hii ya Central Corridor, amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ametoa ombi hilo leo, Jumatatu, Juni 22, 2009, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ufundi ya mfuko huo, Bwana Hassan M. Al-Attaas Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete ameusisitiza ujumbe huo kuwa maeneo ya kipaumbele ya Serikali yake yataendelea kuwa katika maeneo ya elimu, miundombinu, maji na afya.
Lakini ombi langu kwenu ni kushiriki katika miradi ya miundombinu. Najua kuna baadhi wameanza kutusaidia katika barabara hii ya Manyoni - Kigoma, lakini ningefurahi kama na nyie mngeshiriki katika kuchagua ujenzi huu kwa kuunga mkono, kwa mfano, ujenzi wa barabara hiyo kati ya Tabora na Kaliua, amesema Rais Kikwete.
Naye Bw. Attaas amemwambia Rais Kikwete kuwa ziara yake ni kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Rais Kikwete katika Saudi Arabia mwezi Aprili, mwaka huu.
Amesema kuwa Saudi Fund utahakikisha kuwa miradi yote ambayo imekubaliwa kutekelezwa katika Tanzania kwa kugharimiwa na Mfuko huo itatakelezwa kama ilivyokubaliwa. Tuko tayari hata kuanzia leo.
Serikali ya Rais Kikwete imo katika juhudi kubwa kutafuta fedha za ujenzi wa barabara zote kuu na kubwa kama mojawapo ya njia rahisi zaidi za kufungua zaidi uchumi wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Juni, 2009