Ungekuwa ni wewe mke, ungechukua hatua gani?

Dah! ni ngumu sana na inaumiza moyoni.... kwanza pole kwa yalikukuta.

Upande wangu sitomsemesha na nitamtafutia kibegi naenda kununua na pasi na sabuni pamoja na jik halafu nitamuuliza kwani hao wa dada huwa nafua nguo lini ni kila siku ama maramoja kwa wiki, akiuliza ni kwann nauliza hivyo namtolea nguo nilizozifungasha kwa ajili ya kufua ili awapatie wafue na wakimaliza wapige pasi mie kazi yangu ni kupanga kabatini.

Baada ya hapo hatosikia namuuliza uko wapi kwanini umechelewa kurudi nyumbani na akirudi anakuta chakula mezani akila asile wajibu wangu nimekamilisha ila kwa chakula kingine cha usiku ndio aandike maumivu kwani sitoweza kumpatia hadi pale atakapo jirekebisha na nikajihidhirisha kuwa amejirekebisha ndio nitampatia
 
Back
Top Bottom