Ungekuwa ni wewe mke, ungechukua hatua gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungekuwa ni wewe mke, ungechukua hatua gani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WALIMWEUSI, Jun 20, 2012.

 1. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Jana mumeo karudi toka kazini kalewa tilalila! Kwa upendo ukamhudumia hadi ukahakikisha amelala vizuri. Then ukasikia sim yake inaita, kwa vile hawezi kuongea ukataka kuipokea ila ikakata. Hujakaa sawa inaingia sms hii ' Baby niko didz nakusubiri, nimekumiss sana'. Ulipoiona ukawa mvumilivu hadi asubuhi ila ile namba ukaihifadhi somewhere.
  Asubuhi ukamwambia husband wako about simu yake na sms iloingia. Akaisoma with confidence na kusema kuwa huyo ni demu wa rafiki yake na kwamba aliitumia kuwasiliana nae coz sim yake ilikuwa off. Kwa vile hukutaka malumbano ukakubali lakini ukataka kufuatilia zaidi.

  Jioni ya siku hiyo mumeo akakwambia kuwa atachelewa kurudi coz ana kazi ofisini, na around saa 4 usiku ndo atarudi.Ilipofika mida ya saa 1 usiku ukampigia simu yake coz alikuja mtu kumtafta, ukakuta imezimwa. Ukawa anxious kujua why na ukaona utumie sim ya mtu mwingine kupiga ile namba ya jana ilomtext mumeo. Ukakuta haipatikani. Hadi mida ya saa 3 na nusu ndo simu zao zikapatikana tena kwa pamoja. Husband aliporudi home, alikuwa amevaa shati jipya ambalo hakulivaa asubuhi. Ukamuuliza why ana shati jipya akasema alovaa lilichafuka so kaliacha ofisini wadada wafanya usafi wamfulie.

  Wewe ukiwa mke hapa, utachukua hatua gani?
   
 2. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,230
  Likes Received: 13,687
  Trophy Points: 280
  Mbona Kila kitu hapo kinajieleza, Piga kibuti cha shingo asepe zake. Samahani,Mi sio mwanamke lakini.
   
 3. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Ha ha ha, men bwana! Eti 'my wife you dont trust me'! Khaaa!
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  unaendelea na maisha ya mume na mke...huna la kufanya..kesho yake unamkumbusha pia kuleta shati lililofuliwa ofsini pia kesho unampa nguo chafu zoote ndani maana wadada wa ofsini kwake wanapenda kufuafua waendelee kufua...
   
 5. G

  GALIMA JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ayaaaaaaa!!ngoja nimpigie kama anapatikana afu nakuja kukujibu
   
 6. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mi siwezi kuishi nae as if hakuna kilichotokea aisee! Yani from that day, sitoshika nguo yake kufua, looh! Kuna uzi aliuanzisha Mtambuzi kuhusu mambo haya haya, kwa nini wanawak ukiwakosea wananuna na kusitisha baadhi ya huduma, sa naomba wanaume mjue kuwa mambo kama haya ndo yanachangia mkose huduma humimu muhimu.
   
 7. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nakusubiri
   
 8. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hapo panataka moyo wa ujasiri sana mana moyo kama wangu nahisi unaweza kufa kabla ya wakati jamani mana unaona unaibiwa live ......kweli ndoa ndoana kha!
  kwamm ningemuomba aache hiyo tabia hiyo tabia na kama angeendelea tena ingeonesha kua upendo kwangu na mm na yy hauko tena ivo ingenilazimu kuondoka ...ila kuondoka kwangu ni bada ya mm kujaribu mara kibao kumbadilisha na kumshauri na kumuelewesha pia anachofanya sio kizuri ikishindikana itabidi mm kuondoka kwakuogopa magonjwa sasa kuletewa
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa ni mke, ningeingia chumba cha ndani nianze kufanya maombi ya mfungo...Nilieeeeeee machozi na mauchungu yote. Halafu najipanga namna ya kuendelea, kama nitachukuliana naye, au nitasepa kimya kimya nitajua baada ya hilo zoezi.
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sasa hapo utamkomoa nini wakufua si kasema wapo ofsini? tena wanamnunulia na nguo mpya...kununa haisaidii .....huyo ni shetani na kwa vile kukwepa kuishi na shetani ni ngumu unaishi nae kijanja
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Mantiki ya hadithii ni nini?
   
 12. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii ni hadithi kwani? Mi najua hadithi huanza na 'hadithi hadithi'.........Au!!
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Una akili sana! Afu wknd unampeleka mlimani city mkanunue pasi mpya, ile ya home unampa awapelekee wadada wa ofcn ili wakifua wapasi kabisa! Tena unafungasha na chupi kabisa, na jik!
   
 14. awp

  awp JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  dawa ni kuachana nae kwani uaminifu na upendo umepotea
   
 15. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,681
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Ushahidi haujitoshelezi there is still room for error!
  (FYI: m not a woman)
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nakoleza upendo kwa mume wangu... ili kama kuna kidudu mtu kinataka kuchukua nafasi kisahaulike...
   
 17. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mh, im not surprised,ni lazima mwanaume aone kuwa ushahidi haujitoshelezi
   
 18. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,681
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  WALIMWEUSI, it doesn't necessarily take a man to know that there still error in judgement. Mbona reasons zake ziko very staight n concrete? shati likichafukia kazini ndo aje nalo hivyohivyo? cm ya rafiki yake ikiisha charge ndo asimuazime?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  umeonaa eeeh mungu akupe nini tena
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mtu keshaliwa vyake hapa...sijui shati walilifanyeje hata...daaah au ilikuwa kichakani likatumika kama kilalio
   
Loading...