Ungekuwa ni wewe ma watoto wa huyu jamaa ingekuwaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungekuwa ni wewe ma watoto wa huyu jamaa ingekuwaje

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Apr 13, 2009.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yap! Ni kama kawaida Sikukuu hiyo inapita, lakini haipiti bila vioja na vituko vya hapa na pale. Ni kama saa mbili hivi usiku najirudia nyumbani. Mara kwa mbele naona watu wanabishana, natamani kujua kinachoendelea,,, Du jamaa kalala chini hajitambui, yuko chakari kwa kinywaji. Rafiki zake nao hawawezi kumsaidi maana nao wako bwi. Wasamaria wema wanaazima Mkokoteni kwa jirani wakampakia na safari ya kurudi home ikaanza. Mke kugongewa anafungua mlango anakutana na jamaa yuko juu ya usafiri huu! Haraka haraka anafunga mlango na hakufungua tena hadi tunaondoka hapo kwao. Je ingekuwa ni wewe mke wa huyu jamaa ungefanya nini?
   

  Attached Files:

 2. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jalia wewe ndio mke unaletewa mumeo hali kama hiyo yupo chakari ?pia isitoshe jalia anafikishwa kwako akiwa yupo tepe tepe vijana washamfanyia kweli ,utakuwa na uwamuzi gani ?
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hapo ndo kaazi kweli kweli! Mi cjui ndo maana nauliza humu ili makina mama watujuze
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Eeka Mangi hapo ni Arusha au Sehemu fulani ya Kilimanjaro na huyo jamaa atakuwa amekunywa Banana Wine,Safari au Spirit kama Nyagi au Tyson lakini sio Tusker Bariiidi.
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Huko ni kijijini Knjaro Mkuu. Cjui alikunywa nini ila nilimkuta maeneo wanakouza ze bia, ze nyagi na hizo banana. Cjui alikuwa amekunywa nini hasa.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Niabu aibu....hata kama ni ndugu yako wa karibu! Lol hizi huwa ni pombe za bure ndo maana watu kama hawa hufakamia kama kiama....loooh
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mnacheza mziki wa banana wine na mbege ya kibosho........

  lakini huyu naona kama bwabwa vile hata rangi kwenye vidole kapaka hapo alikuwa anatafuta hisani......
   
 8. Violet

  Violet Member

  #8
  Apr 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nitamfungulia kuondoa aibu zaidi, lkn kesho yake itabidi tukalishane, tuelezane vizuri. lol!
   
 9. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Habari ni kuwa Mama kafungasha kilicho chake na kurudi kwao. Habari ni kuwa,,,,,
  Jamaa alikuwa anafanya kazi kwenye kajishamba ka bwana mmoja anayeishi mjini na alikuwa na malimbikizo ya mshahara kwa huyu mwenye shamba. Basi bosi alipokuja hii Pasaka akampatia jamaa mshiko wake kama kilo moja na nusu hivi. Jamaa akachomoka asubuhi kwa kigezo kuwa anawahi Kanisani! hakurudi mpaka aliporejeshwa na huo usafiri. Nilipouliza kama alikubakiwa na kitu mfukoni? Nikaambiwa hata senti moja hakuwa nayo.
  Huko baa, tunaambiwa jamaa alikuwa kimwaga, kila aingiae anapata anachohitaji.
  Wakati tunaondoka huko kijijini tumemwona jamaa kashika jembe anaelekea kibaruani na ana ngeu kadhaa kichwani.
  Hatukumuuliza ya mke kama karudi ama la!
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hilo ndio tatizo la kunywa pombe bila chakula tumboni! Pombe hupanda haraka kichwani na kusababisha maamuzi tata kibao!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kuna mtu ameninong'oneza eti huyo jamaa ni mwanaJF mwenzetu looo!
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  We Masanilo weee,,, waombe radhi waJF wote,,,,lol
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahaha huyo inasemekana ni Tusker baridiiiiiiiiii hahahahah am kidding!
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya mi sianutani nao.
  Tusker Baridiiiiiiiiiiiii unayasikia hayo! Utani wa ngumi huu. Simo
   
 15. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Kweli huyu jamaa atakuwa maeneo yaliyotajwa hapo juu, kielelezo ni mambwa (viatu alivyovaa) & toroli. Atakuwa kachanganya zote..,MBEGE, VALUE, BANANA,BINGWA bila kusahau KONYAGI MWITU a.k.a MACHOZI YA SIMBA. Mhh ila jamaa wa hayo maeneo wakati wa sikukuu hawalegezi kamba! Mkewe alistahili kumfungia mlango!
   
Loading...